Updates: Kesi ya Mpendazoe v/s Mahanga

KIHIYO wa Temeke alibwaga manyanga kabla ya hukumu, inafanana sana na hii. Akatuzawadia msamiati wa vi-hiyo.
 
huu ndo ushahidi wenye akili timamu sasa, sio kama Arusha, utumbo mtupu, mara ooh, mimba ya Lowasa, mara Udini, mara hatuongozwi na mwanamke,
 
Nyantare hatukukuchagua bwana toka kimyakimya. Ndio maana hata kutembelea jimboni unaogopa, unapita kwa kuvizia au kutuma wapambe. Vipi mbona siku hizi kwenye mabonanza huonekani mzee? Segerea umehama, au upo kiaina?
 
Lakini mwisho utaona ........maamuzi ya majaji wetu eti ushahidi wa wadai haujitoshelezi! Mahanga ataendelea kupeta!
Hivi unajisikiaje kuwaongoza watu ambao hawakukuchagua!?

Mkuu huyu jaji aliyepewa hii kesi yuko strictly kishenzi,msimamo wake unajulikanaga hata pale university of Dar es salaam,sijui labda iweje,ila ni likely Makongoro Mahanga anakwenda na maji hii
 
Wana Segerea tunajua mbunge wetu ni F.Mpendazoe,huyo Mahanga ni mbunge wa JK
na Fuime mkurugenzi wa manispaa ya ilala. Keep it up kamanda Mpendazoe,tupo pamoja.
 
[h=2][/h]JUMATANO, 14 MACHI 2012 07:27 NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM


SHAHIDI wa nne katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge, Jimbo la Segerea, Bazil Ng’oholope, jana aliieleza Mahakama kuwa, kilichomsukuma kufika hapo ni kutetea maslahi ya wananchi ili wananchi waongozwe na mgombea waliyemchagua.

Ng’oholope aliyasema hayo Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, alipokuwa akitoa ushahidi mbele ya Jaji, Profesa Ibrahimu Juma, huku akiongozwa na Wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatara.

Alidai kuwa, alitaka kupinga matokeo ya udiwani wa Kata ya Vingunguti, ambako alikuwa amegombea kupitia Chadema, lakini hakufanya hivyo kwa sababu ya matatizo ya kifamilia.

“Mimi nasema ukweli na Mpendazoe kasema kweli, matokeo niliyokusanya katika vituo yalionyesha tulishinda, sijui Diwani wa Vingunguti alitangazwa vipi wakati vituo saba matokeo yake hayakujumlishwa.

“Matokeo ya udiwani hayakutangazwa katika kata, hali iliyowafanya wananchi kurundikana katika ofisi za kata hadi walipotawanywa kwa risasi za moto na askari polisi.

“Nilijua zilikuwa risasi za moto kwa sababu nilimsikia askari mmoja nadhani ni kiongozi wao akiwaonya wasitumie risasi za moto, walimjibu wee mzee vipi, hatuwezi kuacha kutumia, wananchi hawa wengi wanaweza kufanya lolote,” alidai Ng’oholope.

Shahidi huyo alimaliza kutoa ushahidi wake na shahidi wa tano ambaye ni Mwangalizi wa Uchaguzi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Christina Kanani, alipanda kizimbani kuendelea na ushahidi.

Wakati wa ushahidi wake, alidai alikuwa katika Ukumbi wa Arnatoglo, Mnazi Mmoja kwa siku tatu na matokeo yaliyokuwa yakisababisha vurugu yalikuwa ya Jimbo la Segerea, ambapo alikamatwa mama mmoja akiwa na fomu za kupigia kura za jimbo hilo na mwingine alikutwa na mihuri.

Shahidi huyo alidai kuwa, akiwa ndani katika ukumbi wa kufanyia majumuisho ya kura za ubunge na urais, hakumuona mkurugenzi wa uchaguzi akitangaza matokeo ya mgombea kwa kituo kimoja kimoja.

“Matokeo yalitangazwa nje uwanjani saa nane usiku, yalikuwa ya jumla na yalitangazwa kwa dakika tano tu,” alidai.

Shahidi huyo alimaliza kutoa ushahidi wake na kesi iliahirishwa hadi leo. Katika kesi hiyo, Mpendazoe anapinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga.

 
ni kawaida yao hao kuiba kura na kuhonga watu kwa chumvi na sukari, na chaguzi chache sana ambazo ccm hushinda kihalali nyingi ni za kutumia polisi na kuiba kura tu.. kuishabikia sisiemu unapaswa kuwa na akili za maiti.
SISIEMU NI JANGA LA TAIFA.
 
hawa mahakimu, TISS, tume ya uchaguzi na wananchi wanaokubali kupokea hizo tsh 10,000 ndio wanaoredisha nyuma maendeleo ya nchi yetu. Tubadilike
 
SHAHIDI wa kumi katika kesi ya kupinga matokeo ya jimbo la Segerea, yaliyompa ushindi Dk. Makongoro Mhanaga (CCM), James Haule, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CHADEMA, Fred Mpendazoe, ameiambia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa matokeo ya kura katika kata nane yalifichwa.

Shahidi huyo ambaye alikuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2010 kwa tiketi ya TLP, alidai kuwa masanduku ya kura yaliletwa Anatoglou yakiwa tupu bila kuwa na fomu za kupigia kura.

Haule alikuwa akijibu maswali ya wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, pamoja na wakili wa utetezi, Jerome Msemwa, na Wakili wa Serikali (SA) David Kakwaya.

Katika kesi hiyo, Kibatala, anamwakilisha Mpendazoe wakati Msemwa anamtetea Dk. Mahanga.

Mbele ya Jaji Ibrahimu Juma, Haule alidai kuwa matokeo ya kura za kata za Kiwalani, Vingunguti na zingine hayakujumlishwa katika matokeo ya jumla, hali inayoleta shaka katika ushindi wa Dk. Mahanga.

Haule aliiambia mahakama kuwa licha ya matokeo ya kata hizo kufichwa hata fomu ya majumuisho ya matokeo ya kura (21B) hazikuwepo.

Alidai kuwa kukosekana kwa matokeo hayo ni malalamiko ya baadhi ya wagombea ambayo yako kisheria.

Kwa mujibu wa ushahidi wake, alifika majira ya saa 2 usiku kwa ajili ya kufuatilia matokeo ya kura, ambapo alishangazwa na baadhi ya makada wa CCM, kushangilia ushindi wa Mahanga kabla ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo.

Alidai kuwa wakati wakisubiri matokeo kutangazwa Novemba 2, 2010, majira ya jioni, Kinana alifika kituoni hapo kisha akaondoka na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi wa majimbo ya Ilala.

Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa matukio yaliyojitokeza baadaye baada ya Kinana kuondoka kituoni hapo Anatoglou, yalitia mashaka kiasi cha kumhusisha Kinana na mkurugenzi huyo kuwa walikwenda kubadilisha matokeo.

Haule aliendelea kudai kuwa katika uchunguzi wao na mawakala wake waligundua fomu 120 za matokeo ya kura zilifichwa.

Alifafanua kwamba hata kitendo cha kukamatwa kwa Mahanga na masanduku ya kura kiliathiri kiasi kikubwa uchaguzi huo.

Katika kesi hiyo Mpendazoe analalamikia mwenendo mzima wa uchaguzi katika jimbo hilo akidai taratibu na sheria za uchaguzi zilikiukwa katika ukusanyaji ujumulishaji na utaratibu wa kuhesabu na utangazaji wa matokeo. Hivyo anaiomba mahakama hiyo itengue matokeo ya ushindi wa mbunge aliyetangazwa na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo au yeye atangazwe mshindi.


Source; Tanzania Daima
 
Mahanga hawezi kuchomoka kwenye hiyo kesi so cha msingi kwa wapenda mageuzi tujiandae tena kwa uchaguzi mdogo.
 
Mahanga hawezi kuchomoka kwenye hiyo kesi so cha msingi kwa wapenda mageuzi tujiandae tena kwa uchaguzi mdogo.
Dah mzee hizi mahakama zetu nazo zina walakini siku hizi maana nazo kama zimekuwa political arena behind curtains
 
Thatha nadhani huna la kusema hivi kaja kwako kuomba posho au kula??? hivi unadhani yeye ni omba omba omba ???
 
CCM ni wajanja sana katika hili. Walijua kuwa mbinu zao za wizi zimeng'amuliwa na kwamba Mpendazoe akienda kortini lazima Mahanga aenguliwe. Nadhani CCM wameshaanza kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Ukonga na huko pia "WataIgunga" uchaguzi huo. Ni vyema mwizi huyu wa kura akafunguliwa mashtaka ya wizi wa kuaminiwa wa stahili za wananchi wa Ukonga na azuiwe kupigania chaguzi yoyote ile inayosimamiwa na NEC. Hii ndio njia pekee ya kuondokana na mafisadi wa kura.
 
Back
Top Bottom