Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
[TR]
[TD="class: Headline, align: left"]Mpendazoe ashindwa kueleza idadi ya kura
Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 5th March 2012
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: kaziBody, align: left"]
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea mkoani Dar es Salaam, Fred Mpendazoe (Chadema), ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa yeye ndiye mshindi wa jimbo hilo ingawa alishindwa kujibu maswali ya mawakili wa wadaiwa yaliyomtaka kueleza ni kura ngapi alipata katika vituo.
Akiendelea kutoa ushahidi wake jana, Mpendazoe katika kesi aliyoifungua ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo, alidai maswali ya mawakili Jerome Msemwa na David Kakwaya yaliyohusu idadi ya kura katika vituo anavyodai alivitembelea siku ya uchaguzi, alisema kuwa
hakumbuki idadi yake.
Alipoulizwa kama ana nyaraka zozote zinazothibitisha ushindi huo anaodai aioneshe Mahakama ili kuunga mkono kauli zake, Mpendazoe alidai kuwa hakuja nazo na kwamba sio kazi yake kujua kwa sababu wapo watu ambao watakuja mahakamani hapo kutoa ushahidi huo wa idadi ya kura alizozipata.
Inakuwaje unafungua kesi ya makini kama hii ya uchaguzi wakati hujui ni kura ngapi ulipata katika kila kituo unachokilalamikia huoni kuwa unapoteza muda wa Mahakama? Alihoji
Wakili Msemwa.
Mpendazoe alidai kuwa hawezi kuwa na kumbukumbu ya hesabu zote hizo, lakini kwenye hati yake ya madai mahakamani, ameainisha idadi ya kura alizopata ingawa jumla anadai kuwa ni 56,962 kwa jimbo zima.
Anadai Kiwalani katika vituo 120, masanduku yaliyofika katika kituo cha kuhesabia kura cha Anatoglou bila mawakala kuwepo kwenye gari hiyo, jambo ambalo lilimtia hofu, na alipomuuliza mwakilishi wake kama majumuisho yalifanyika, alimjibu kuwa yalifanyika ya udiwani tu na siyo ya ubunge.
Aidha, alidai kuwa fomu nane za kujaza matokeo ya ubunge zilikosekana Vingunguti hata hivyo alikiri kuwa asingeweza kutembelea vituo vyote vya kupiga kura katika jimbo hilo ila alitembelea vituo tisa tu na vituo vingine alipata taarifa kutoka kwa mawakala wake.
Alipoulizwa na Wakili Msemwa ni wapi alipopata matokeo hayo ya kwamba yeye ndiye mshindi wa ubunge katika jimbo hilo, alidai ni mfumo waliokuwa wakiutumia kupata hesabu hiyo ambao ni mawakala wake kuchukua matokeo mara tu yanapobandikwa katika kila kituo cha kupigia kura.[/TD]
[/TR]
[TD="class: Headline, align: left"]Mpendazoe ashindwa kueleza idadi ya kura
Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 5th March 2012
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: kaziBody, align: left"]
| ||
|