Updates: Hukumu kesi ya Prof Mahalu; ashinda kesi dhidi yake!

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
495
Wana JF

Leo mahakama ya hakimu mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi inayomkabili Prof Costa Mahalu aliyekuwa balozi wa Tz nchini Italy na mwenzake.

Mtakumbuka kesi hii ilimfikisha mahakamani Rais Mstaafu Mkapa aliyemtetea Mahalu kwa nguvu zote. Rais Kikwete alitakiwa kupanda kizimbani pia kutoa utetezi wake lakini alikwama kwa mujibu wa katiba yetu.

Hukumu ndio leo. Nikiweza nitakuwapo kutoa updates kama bepari wangu hataleta kauzibe. Vinginevyo wale watakaoweza kuwepo, ruksa kupashana kinachojiri
Leo (Agosti 09, 2012) Mahalu kaibwaga serikali katika hii kesi!

Updates zinafuatia
Mahalu kashinda kesi..

Chanzo: Radio One breaking news!
4.jpg
Waandishi wa habari wakimfuata Balozi Profesa Mahalu akiwa pamoja na Mdogo wake Mirasi Rama wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu Mchana huu mara baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kununua nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Akisoma hukumu iliyosomwa kuanzia Saa sita leo na Hakimu Mfawidhi mkazi wa mahakama ya Kisutu Mh. Ilivin Mugeta imemtoa Balozi Profesa Mahalu katika hatia na kumwachia huru (PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG)
1.jpg

Balozi Profesa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushinda kesi yake katika mahakama ya kisutu leo.
2.jpg

Wakili wa Balozi Profesa Mahalu Bw. Alex Mgongolwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mteja wake kushinda kesili iliyokuwa ikimkabili kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam.

3.jpg

Balozi Profesa Mahalu katikati akitoka nje ya mahaka ya Kisutu huku akiwa ameongozana na mdogo wake Mirasi Rama kulia ni Wakili wa kujitegemea Mabere Nyaucho Marando.

Picha na Full Shangwe Blog
1859130880412241953-8397735442630508199

 
Nasubiri kwa hamu sana kuona jinsi comedy hii nayo itaishaje!!maana hadi mzee mzima BWM aliamua kwenda kusaidia jahazi!kweli fitna mbaya sana,ngoja tusikie leo ni rufaa tu pande yeyote itakayoshindwa,kusogeza muda na kutupumbaza
 
Katika vitu tunavyovikataa hapa JF ni kuanzisha uzi na kisha kutokuwa na uhakika wa ku update!!!!

Uzi mkuu utakuwa ni huu na kuwapa MODS kazi ya ziada ku updade jambo ambalo siyo la msingi.

Hata hivyo nashukuru kwa kuni alerts kuwa ni hukumu ya Prof. Mahalu.
 
Ni mhimu haki itendeke! Hata kama watalaamu watapangua hoja na kila mmoja akaridhika, mi sina shida. Lakini kama upande mmoja utaonekana hauna hoja za nguvu lakini ndo ukashinda basi bado tutakuwa tunahitaji wataalamu zaidi wa sheria.
 
kwa upeo wangu prof. Maharu hii kesi anachomoka ni visasi vya dhaifu tu..ushahidi uliwekwa hapa jf jinsi serikali ilivyoshirikishwa a-z, iweje wamfunge..?
 
Nasubiri kwa hamu sana kuona jinsi comedy hii nayo itaishaje!!maana hadi mzee mzima BWM aliamua kwenda kusaidia jahazi!kweli fitna mbaya sana,ngoja tusikie leo ni rufaa tu pande yeyote itakayoshindwa,kusogeza muda na kutupumbaza

Comedy kweli na atashinda tu, tusubiri tuone. Aliyemuuzia nyumba alisema risiti ile siyo yakwake ( na akaonyesha yakwake electronically) sasa hapo unataka ushahidi gani tena. Subiri uone ubabaishajiwa mahakimu wetu!!
 
Kesi hii ni lazima Mahalu ashinde. Kwa mara nyingine mahakama imeingia kwenye kitendawili au kutoa haki au kusimama na aliyeianzisha mr dhaifu.
Tatizo la kikwete ni mtu wa visasi sana na amehusika sana kuitunga kesi hii na jambo hili ni dhahili wala halina kificho hata chembe.
Kweli kikwete ni dhaifu..
 
Nijuavyo leo ndiyo siku ya Hukumu. Kesi iliyoweka historia ya kumfanya Rais Mstaafu aweze kutinga mahakamani.

Kesi ambayo imeonyesha kwamba matamshi ya Bungeni lazima yatamkwe kwa umakini.

Ushahidi wa kwenye hansard ulikuwa ni htouba ya Jakaya Kikwete akikiri kwamba hakukuwa na makosa katika process ya kununua jengo la Ubalozi huko Italy.

Maneno ya hansard hayo ya Kikwete aliyatamka Benjamin Mkapa mahakamani.

Hivyo, waliopo mahakamani kama wanaweza watupe live update kama zilivyofanyika live updates nyingi na nzuri.

Tuliijadili sana humu kesi hii tunaomba tujue live update yake pia.
 
Back
Top Bottom