Gama
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 13,266
- 4,716
Wana Jf, mtakumbuka kuwa ni miaka sasa imepita tangu wakazi wa Kipawa wahamishwe na wakazi wa kipunguni kutakiwa kutoendeleza makazi yao wakisubiri kulipwa fidia na kuhama ili kupisha upanuzi wa JKNIA, kwa macho ya kawaida utagundua kuwa utekelezaji wa mradi huo uliokuwa umetajwa kufadhiriwa na serikali ya Uchina unasuasua. Kunatetesi kuwa mradi huo huenda hautatekelezwa sasa kwa sababu Uchina ulitegemea kupewa offer ya kuchimba madini ya Urani, hata hivyo marekani nayo ilikinga ubavu hivyo kuilazimisha kupewa offer ya kuchimba madini hayo muhimu. Mabadiliko haya yameifanya serikali ya Uchina isuse kutekeleza mradi wa ujenzi wa teminali ya tatu ya JKNIA. KAMA KUNA MWENYE FUNUNU ZINAZOFANANA NA AU HATA KUTOFAUTIANA NA FUNUNU HII ATUJUZE.