Upandishwaji wa bei ya umeme itatusaidia?

Oct 22, 2011
94
10
Ni siku moja tangu bei ya umeme itangawe kupandishwa kuanzia jumapili kwa malengo ya kuisaidia TANESCO kuweza kuendesha shughuri zake vizuri.1.swali kunawakati ambao umeme utarudi katika bei tunazoziacha au ndo byby,
2. nikweli pesa zitakazopatikana baada ya ongezeko hili ni kweli zitafanya kazi kama ambavo imeongelewa
3.kwakupandisha bei za umeme na mafuta hasa diesel tunategemea nini kwa maendeleo
 
kiukweli serikali hii niyakiuaji kwani sio tu umeme pia mwananchi alipe ada ya mitihani kwa watoto, ajenge shule, umeme juu eti kampuni gharama za uendeshaji zimepanda, Kwani mwananchi kwake gharama hazipandi. Hii ni hatari kwani kila kitu bei juu na serikali inajivua.
 
Upandishwaji wa bei ya umeme itatusaidia katika kuongeza ukali wa umasikini kwa mwananchi wa kawaida.

Sina uhakika kama neno kusaidia hapa lina maana inayokusudiwa. Tuseme kuwa upandishwaji wa bei ya umeme utatunyonga wengi kati yetu tuliopewa ahadi hewa ya maisha bora kwa kila mtamania( mwenye kutamani maisha ya heshima)
 
Yaani sisi watanganyika watu wa ajabu kweli! Juzi imepanda bei ya kivuko tukaja juu kama moto wa kifuu! Wabunge wakatoa maneno mazito dhidi ya waziri magufuli, wananchi wakazomea, JF ikajaa thread za kuzungumzia hilo jambo (acha kauli za waziri). Leo umeme umepanda zaidi ya 40% kwa unit watu hatupigi mayowe. Kwa hiyo ni kawaida tu kwa bei ya umeme kupanda, bei ya vyakula kupanda lakini inapokuja bei ya kuvuka kupanda kidogo watu wanakuja na mabango! Nchi ya watu gani hii? Watu wamejaa makengeza na wengine wamepigwa upofu!
 
gharama za maisha zitapanda mno
mfano

  • bei za kusaga na kukoboa nafaka zitapanda sana - waadhilika ni wote wenye umeme na wasio nao
  • bei za vitafunwa lazima zipande kwani bei za mashineni zimepanda
  • gharama za ujenzi zitapanda eg cement, chokaa, kuranda mbao etc
  • gharama za maji zitpanda na hili limetangazwa leo via magazetini
  • etc

Ninacho kiona uwezo wa viongozi kufikiri namna ya kumpunguzia mwanachi ugumu wa maisha umefikia elastic limit sijui tueleze kwa namna gani ila tunako kwenda ni kubaya zaidi mfumuko wa bei kwa sasa ni doule digit 19.2% kama wanasema ukweli Na wahusika hawana mpango wowote wa kushusha

kifupi TUTAJUTA
 
Yaani sisi watanganyika watu wa ajabu kweli! Juzi imepanda bei ya kivuko tukaja juu kama moto wa kifuu! Wabunge wakatoa maneno mazito dhidi ya waziri magufuli, wananchi wakazomea, JF ikajaa thread za kuzungumzia hilo jambo (acha kauli za waziri). Leo umeme umepanda zaidi ya 40% kwa unit watu hatupigi mayowe. Kwa hiyo ni kawaida tu kwa bei ya umeme kupanda, bei ya vyakula kupanda lakini inapokuja bei ya kuvuka kupanda kidogo watu wanakuja na mabango! Nchi ya watu gani hii? Watu wamejaa makengeza na wengine wamepigwa upofu!

Probably Mch Mtikila was right when he claimed that Tanzanians need mental emancipation
 
Back
Top Bottom