UOTO wa asili kutoweka kutaliangamiza Taifa

pilau

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
1,594
446
Katika hali isiyokuwa ya kawaida watanzania tunatatizo la kuharibu mazingira hasa misitu, imekuwa ni janga la kitaifa kwa wananchi wa vijiji mbalimbali nchini kukata miti na kuharibu misitu kwa sababu ya kuvuna mkaa, mfano viongozi wanawaachia wananchi vijijini wanakata miti mikubwa wenye thamani kubwa kwa ajili ya mkaa gunia tatu ambazo kijijini linauzwa sh. 5,000, uoto wa asili unazidi kupotea, watanzania wamekosa viongozi mathubuti katika vijiji, wilaya hata mikoa wa kuwaelimisha wananchi kuwa uoto wa asili ni kitu muhimu na adimu tulichoachiwa urithi na mwenyezi Mungu, mali asili zetu za misitu mbona tunaziangamiza? Wana JF imefikia hatua mbaya kwa sasa hata sehemu za kuweka mizinga kwa ajili ya kuvuna asali miti yote imekatwa hii imesababisha hata asali iwe adimu na kama ipo kidogo iuzwe bei kubwa kwa kuwa wavunaji wanashindwa kuweka mazingira ya upatikanaji wa asali kwa wingi, sehemu zote zilizokuwa zikitirika maji zinaendelea kukauka na viongozi katika maeneo hayo wapo bila kuficha Taifa hili litaendelea kuwa jangwa
 
Nilitegemea kupatikana kwa gas hapa Tanzania kungeinusuru misitu ya Tanzania badala yake bado gas inaingizwa kutoka nchi za nje na kuuzwa kwa bei mbaya ambapo ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida kumudu. Hii nchi viongozi hawako makini sijui wanalionaje jambo hili wao wamekalia ufisadi tu. Kama tukiendelea hivi nina hakika uharibifu wa mazingira utakuwa mkubwa kiasi kwamba nchi yetu itaingia ktk ukame ambao haujawahi kutokea, na zaidi ya hapo uoto wa asili itakuwa adimu na historia.
 
Back
Top Bottom