Uongozi wa Nyerere na haja ya Katiba mpya

On top of that ametuachia legacy ya wananchi walio wengi kuwa waoga kudali haki zao, wanyenyekevu kwa wageni, wasiojiamini, wanaoamini kupata shida za maisha ni haki yao etc....The ghost and legacy of Nyerere!!!
This Nyerere must have been a demi-god! Yaani hata uwoga na unyenyekevu wa watu viliasisiwa na Nyerere? Damn!
 
Kuhusu Nyerere na mema aliyolifanyia taifa hili despite mapingufu yake, naamini hawa wanao mlaumu na kumshutumu sasa ni wakosefu wa fadhila, watu wasio na shukrani, ni wadhalimu hawa wenye kuweka kumbukumbu ya mapungufu mbele ya dhamira zao na kuyafumbia macho mema lukuki aliyoyatenda.

Wakati wa Nyerere katiba iliyokuwepo ilikidhi haja maridhawa kwa wakati husika hata kama ilipitishwa bila kufuata principles za constitutionalism lakini ndiyo iliyokuwepo na kututoa point A to point B tulipo sasa ambapo sasa tumeshajiridhisha haitufai tena kwa wakati uliopo ili kutufikisha point C ya huko tuendako. Hii haina maana kudisregard tulipotoka.

Nyerere was only human hakuwa semi god wala demi god na not God hivyo kufanya makosa ni kawaida na alikiri wazi kuwa huko nyuma tumefanya makosa na kusisitiza "Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa".
Please mwacheni apumzike kwa amani!.
"Amini nawaambieni, wale wote mnaomlaumu Nyerere kwa kinachoendelea sasa, mtalaaniwa kwa ukosefu wa shukrani!".

Please be aware usije kujijutia mbele ya safari kwa kisingizio cha kutojua because you have been warned before!.

Pasco
 
Mtu akiwa kiongozi mzuri,akilaumiwa kwa mapungufu yake inakuwa kosa? Hata Nyerere alishakiri kwamba aliwahi kufanya makosa,yeye si malaika...Sasa binadamu hajakamilika,kwa hiyo wanaomkosoa wako sahihi,wasiomkosoa pia wako sahihi ila wanaolaumu Nyerere kukosolewa Nahisi wako wako Wrong!
 
Kwa hiyo are u trying to say that watanzania wote walikubaliana na mawazo ya mwalimu na siasa zake?


Ndg Sherrif, Ktk community yeyote ile haiwezi kutokea jambo likakubaliwa na wote , IKIWA HATA MBINGUNI TU MALAIKA LUSIFA ALIMPINGA MUNGU MWENYEWE MPAKA AKASABABISHA VITA itakuwa utawala dhalimu wa duniani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?.
rejea maneno Nabii na mtakatifu, kwa mtazamo wa wengi Wasioyachunguza maandiko ni maneno ya kutisha wakati Neno Nabii ni msemaji tu wa Mungu na kila mwanadamu mwenye kumcha mungu apaswa kuwa mtakatifu Waebrania 12:14.

NI KWELI HATA MABADILIKO YAKIJA KIKWETE HANA CHA KUJISIFIA, KAMA ANACHO BASI NA AFANYE KINYUME CHAKE (AZUIE ) AONE.
 
nakumbuka 1994 wakati ccm wanafanya mabadiliko ya katiba nyerere aliwapinga sana akawaambia mabadiliko ya katiba yafanywe na watanzania wote
Huu ni uongo, mwaka 1994 kulikuwa na vyama vingi, Nyerere angesemaje katiba ya CCM ibadilishwe na Watanzania wote?

na wengine mkimwita ni nabii na mtakatifu aliyekuja kabla

ya muda wake....

Nyerere hakuwa "kabla ya wakati wake," ndio maana utetezi mkubwa wa wanaomwombea msamaha Nyerere wanasema kwamba tujaribu kuelewe mazingira ya enzi za kina Nyerere, hakuwa peke yake, wakati ule hakukuwa na uhuru wa kisiasa Afrika nzima. Wenzake walikuwa kina Mengistu na Samuel Doe. Obote na Babangida. Nyerere hakukubali mawazo huru ya wengi na hakuja "kabla ya wakati wake." Alikuwa kama kina Mugabe, Omar Bongo, Museveni, Hosni Mubarak.
 
wewe hujui kitu
nyerere alikuta nchi ina vyama vingi na katiba nyingine

ni yeye alieleta chama kimoja na katiba hiii tuliyonayo....

Aliikuta Katiba ipi mwenzetu na wakati anaupokea uwaziri mkuu kutoka kwa mkoloni,
Wakoni walichokifanya ni kumuwezesha kutawala kwa kumsaidia aangalau kianzio thru Order in Council na baada ya kuwa jamhuri tukaazima "westminster model" constitution hadi Muungano na zanzibar ndio tukapata Interim constitution ya 1965. Hii iliendelea hadi 1977 baada ya kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ndio tukapata Katiba ya Muungano.UPO HAPO?

Ni mchango wang mdogo kuonyesha ( kwa wenye kupenda kujua) Katiba yetu ilikoanzia.
 
Uongozi wa Nyerere na Haja ya Katiba Mpya
Kuna vitu viwili vinaendelea hapa tanzania
na jf pia..............

Watu wengi wanazungumzia haja na madai ya kuwepo kwa katiba
mpya...
Ambayo itakuwa ya watanzania,ya wananchi.
Itakayowapa uhuru wao na mambo mengi kwa ujumla...

Watu wengi akiwemo issa shivji,mwanakijiji na wengineo

wamedriki kusema kusema au kuunga mkono kuwa

katiba iliyopo sio tu haifai,lakini haijawahi kuwa ya wananchi......


Wakati huo huo,kuna mjadala wa kumkosoa nyerere na utawala wake

mjadala ambao cha kushangaza wale wengi wanaomtetea nyerere kuwa

alikuwa kiongozi bora na wa mfano,
na ambae alikuja kabla ya wakati wake ndio hao hao wanaodai katiba hii tuliyonayo

haifai na haijawahi kuwa ya wananchi......
Ni katiba mbovu,inayowakandamiza wananchi,haiwapi nguvu na uhuru wa kutosha
na kadhalika......

Sasa hapa swali ninalouliza ni hili.............

Inawezekanaje nyerere huyo huyo ambae alikuwa

kiongozi bora sana,na wengine mkimwita ni nabii na mtakatifu aliyekuja kabla

ya muda wake.......lakini leo katiba ile ile aliyoitumia kutawala na kuitengeneza

tuseme haifai kabisa na haina uhalali na sasa tunahitaji mpya?????????????????????????????

Mind you kuwa hatuzungumzii mabadiliko ya katiba tu
tunazungumzia katiba mpya,katiba nyingine inayofaa na sio hii ya nyerere...
Like
 
Sina hakika na Shivji lakini Mwanakijiji atakuwa kwenye wakati mgumu sana hasa akifikiria kwamba katiba iliyopo ni zao la utawala wa awamu ya kwanza. Angetamani leo atamke kwamba katiba hii ilitengenezwa na Kikwete ili amtwishe mzigo huo kwa chuki tu. Thanks God ni Kikwete huyo huyo ndiye sasa aliyeamua ku-midwife upatikanaji wa katiba mpya.

Hapo bold... Katiba ni zao la siasa za wakati uleee hata kama siyo Nyerere bado ingekuwa jinsi ilivyokuwa ukizingatia historia ilivyokuwa wakati ule.

Hivyo tusitafute wachawi bali tuone ni vipi wananchi "washiriki" na siyo "washirikishwe" kwenye mchakato wa Katiba mpya.Kutafuta mchawi nani haitasaidia sana sasa hivi.

Makosa yalitendeka kwa vile wananchi nao walikuwa siyo waelewa sana na mwamko tunaouona sasa haukuwepo enzi hizo kutokana na tunavyosoma historia ya Tanzania kabla ya uhuru, baada, kabla ya Muungano na baada, wakati wa vyama vingi- pre 1964 na baada kipindi ambacho Katiba ya 1965 ilivifuta hivyo vyama vingi na hata ugombea binafsi;bila kusahau uingizwaji wa haki za binadamu ndani ya katiba 1984.

Tujenge uelewa zaidi wa kilichojiri enzi hizo hadi tukajikuta na katiba iliyo na mapungufu, yenye kuakisi zaidi matakwa ya watawala badala ya watawaliwa.
 
BOSS, hajui kwamba katiba ni kama vazi inapaswa kulingana na umri wa Taifa kama nguo kwa binadamu. Katiba ya wakati wa mwalimu ilfaa kwa kipindi hicho.Kuna mabadiliko mengi yaliyotokea toka wakati huo yanayotakiwa kuingizwa katika katiba. Km, mabadiliko ya sera za uchumi wa kijamaa hadi sera za sasa za ubepari uchwara.Mabadiliko ya sasa ya kisiasa, chama kimoja hadi demokrasia ya vyama vingi, uongozi safi,siasa safi kwenda uongozi wa ovyoovyo usio na mwelekeo, utawala wa sheria hadi utawala wa kuwalinda wezi nk nk.Yote haya ndiyo sababu ya wananchi kudai katiba mpya ili watetezi na makuwadi wa mafisadi,kama wewe kama sikosei wasulubiwe.
 
Boss

Naona wachangiaji wengi humu ni kama wamekurupuka, hawaelewi dhana yako ya tofauti kati ya "Katiba kufanyiwa marekebisho kwenda na wakati", na "kudai katiba mpya ya watu altogether".

The U.S constitution ina miaka zaidi ya 200, lakini ina amendmendments zaidi ya 20. Ina maana society ya U.S imebakia stagnant for over 200 years au the changes zilikua taken care na hizo amendments?

Tuendelee kujuzana.
 
Boss

Naona wachangiaji wengi humu ni kama wamekurupuka, hawaelewi dhana yako ya tofauti kati ya "Katiba kufanyiwa marekebisho kwenda na wakati", na "kudai katiba mpya ya watu altogether".

The U.S constitution ina miaka zaidi ya 200, lakini ina amendmendments zaidi ya 20. Ina maana society ya U.S imebakia stagnant for over 200 years au the changes zilikua taken care na hizo amendments?

Tuendelee kujuzana.

Katiba ya US imefanyiwa 26 amendments na ina umri wa miaka zaidi ya 200.Imeweza kuhimili Vita kuu mbili za dunia,Anguko la Uchumi,Ukomoshwaji wa biashara ya Utumwa,Mapinduzi ya viwanda Ulaya,Anguko kuu au mtikisiko wa kiuchumi Duniani mara Mbili 1930,late 2008.....Pia ilweza kustahimili Cold war,Mbio za silaha za maangamizi(Arms Race),chipuko la Utandawazi nk.
 
Kila mtu ana mapungufu yake, Nyerere akuna zuri alilofanya, yote ilikuwa ni kuwakandamiza na kuwanyima haki watanzania katika
nchi yao. Uzuri alioufanya si wa kudhamiria bali watanzania tulijikuta hivyo tunaishi pamoja bila ukabila baada ya kuondoa Uchifu.
na huo ukabila ukaondoa tofauti za dini. kwa hilo alikuwa na maana ni yeye pekee wa kutawala na asitokee mwingine mpaka
atakaposema basi kachoka. Na aliwazuia wazalendo wasiwe na utajiri kwani wangeweza kumuondoa madarakani. Lakini aliwaruhusu
watu wenye asili za kiasia kuwa na utajiri kwa sababu sio hatari kwa uongozi wake. na kuzuia utajiri ilikuwa sio nia njema kwake.
kwa sababu aliamini kama raia wakiwa maskini ndio angeweza kuwatawala kirahisi. na ndio maana ya kuweka ujumbe wa nyumba
kumi ili sauti za wanyonge zikandamizwe kupitia wajumbe matawi ya ccm na mpaka kufikia kwake. Kifupi alikuwa Dikteta.
Katiba ya nchi tulirithi ya mwingereza na yeye akatia nyongeza ya viraka vya ukomunisti. Na ambayo tunaendelea nayo mpaka leo
nayo kwa mfumo wa ukomunisti, Kitu ambacho kimepitwa na wakati na sasa ni wakati wa katiba mpya. yeye alichojitahidi ni kuondoa
rushwa ingawaje akuimaliza., na mapungufu haya yanatakiwa yawemo kaika katiba mpya.
 
Mtu akiwa kiongozi mzuri,akilaumiwa kwa mapungufu yake inakuwa kosa? Hata Nyerere alishakiri kwamba aliwahi kufanya makosa,yeye si malaika...Sasa binadamu hajakamilika,kwa hiyo wanaomkosoa wako sahihi,wasiomkosoa pia wako sahihi ila wanaolaumu Nyerere kukosolewa Nahisi wako wako Wrong!
Ben,'
Kumkosoa Nyerere si kosa. Nyerere mwenyewe alikuwa his own best critic. Lakini tunachoshuhudia hapa si ukosoaji. Kuna upindishaji mkubwa wa facts mpaka watu kusema kuwa Nyerere was a failure. Hapo ndipo sisi tunaojua ufanisi wa Mwalimu tunaposimama na kupambana na wale wanaotaka kulazimisha kuwa Nyerere was a failure. Ukiweka mapungufu yake kwenye mizani na upande mwingine uweke ufanisi wake, ufanisi ni mkubwa zaidi kuliko mapungufu. That is all we are saying. Mtu anadiriki kusema kuwa Nyerere ndiye aliyewafanya Watanzania wawe waoga. Can u imagine?
 
ukitazama sijawahi kusema nyerere hakufaa kuwa kiongozi
ninachokipinga ni ile hali ya kumfanya nyerere kuwa hana kosa lolote
na ni mtakatifu na mtukufu......wakati hata hili tatizo la katiba hii limeanzia kwake.....

na nashindwa kuelewa wanaomwita nyerere mtakatifu na kusema alikuja kabla ya wakati wake

wakati huo huo wanasema katiba hii haijawahi kuwa halali....

sasa nyerere alitawala kihalali?????

halafu mbona tukiwakosoa akina mwinyi,mkapa na jk ni sawa tu...

lakini nyerere hatutakiwi kum gusa kabisa....
 
Hapo bold... Katiba ni zao la siasa za wakati uleee hata kama siyo Nyerere bado ingekuwa jinsi ilivyokuwa ukizingatia historia ilivyokuwa wakati ule.

Hivyo tusitafute wachawi bali tuone ni vipi wananchi "washiriki" na siyo "washirikishwe" kwenye mchakato wa Katiba mpya.Kutafuta mchawi nani haitasaidia sana sasa hivi.

Makosa yalitendeka kwa vile wananchi nao walikuwa siyo waelewa sana na mwamko tunaouona sasa haukuwepo enzi hizo kutokana na tunavyosoma historia ya Tanzania kabla ya uhuru, baada, kabla ya Muungano na baada, wakati wa vyama vingi- pre 1964 na baada kipindi ambacho Katiba ya 1965 ilivifuta hivyo vyama vingi na hata ugombea binafsi;bila kusahau uingizwaji wa haki za binadamu ndani ya katiba 1984.

Tujenge uelewa zaidi wa kilichojiri enzi hizo hadi tukajikuta na katiba iliyo na mapungufu, yenye kuakisi zaidi matakwa ya watawala badala ya watawaliwa.


tausi mchango wako mzuri sana..

nafikiri umeona hapo ninachojaribu kuonesha na kuuliza......

tukisema katiba hii haijawahi kuwa halali.......ni lazima tuulizane

je waliotawala kwa katiba hii je?walikuwa halali????????

na kama nyerere ndie mhusika wa kuweka foundation ya taifa

na foundation hiyo kwa maana ya katiba sio halali....

je hatupaswi kuulizana maswali???????????
 
mkandara nakuheshimu sana
lakini naona hujaelewa maana ya katiba mpya......

unayoyasema nafikiri una maanisha mabadiliko ya katiba......

katiba mpya ni kitu kikubwa mno.kina ondoa uhalali wa katiba iliyopo...

nimesema hapo juu

kuifanyia mabadiliko katiba,ni kitu kingine kabisa
na kudai katiba mpya......

ni vitu viwili tofauti mno..........

wamarekani hawajawahi kudai katiba mpya,
lakini wameifanyia mabadiliko katiba yao mara nyingi mno...
Shukran kwa heshima hiyo maana sii rahisi kuipata bila mimi kuwa na heshima hivyo, ikurudie nawe pia.

Swala la Katiba sio swala la Chadema pekee, Hilo kwanza lazima ufahamu. Chadema inawakilisha mawazo ya wananchi walio wengi ambao wanatambua umuhimu wa katiba hivyo wamepita toka katiba iliyopo na maendeleo tunayokusudia kuyajenga. Labda niseme tu kwamba Katiba mpya sio Itikadi bali ni MWONGOZO wa Taifa letu, hivyo ujenzi wa itikadi utafuata malengo hayo.

Kwa nini tunahitaji Katiba mpya? labda ndilo swali kubwa zaidi kwa sababu katiba iliyopita ilikuwa ilkitumikia siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA (CCM) na ingawaje imefanyiwa marekebisho mengi bado haipotoshi dira ya kulijenga taifa la Ujamaa na KUJITEGEMEA ambayo ni itikadi ya wanaCCM. Na kwa maana hiyo taifa letu bado linatumikia itikadi ya chama hicho pamoja na kwamba tunataka kujenga Taifa la Kibepari.

Labda nitumie tena mifano yangu kujenga hoja zaidi..
Mwanzo wakati wa Nyerere kama ilivyokuwa desturi ya wazazi wetu, tulitaka kujenga nyumba ya vyumba sita (nyumba ya familia) na tukawa na ramani ya ujenzi wake, tukajenga msingi na hadi nyumba kusimama lakini tumegundua nyumba hiyo haifai tena kufanyia biashara hata baada ya kujengea vibanda vya biashara pembeni (marekebisho).

Sasa akitokea mtu na kusema tunahitaji kuvunja nyumba hiyo na kujenga la ghorofa (highrise) ambalo litaweza kuhudumia both accommodation, offices na business, bila shaka ni busara sana kwanza ku suggest we need a new building plan!. Na itachekesha zaidi kudai plan iliyokuwepo zamani inatosha isipokuwa tuendelea kuifanyia marekebisho hata kama tunajenga ghorofa.

Ni akili ya mwendawazimu kufikiria kwamba ramani na msingi wa nyumba ya vyumba sita unaweza kusimamisha ghorofa ama kama tunavyofanya sasa hivi, ati tunaweza kuboresha nyumba ya vyumba sitai kufikia kutoa huduma sawa na jengo la ghorofa..unless mtu huyu hajui anachokizungumza au hajui malengo tunataka kujenga nini? Lakini pia elimu ya ujenzi wa nyumba ya vyumba sita au ghorofa hazipishani kiasi kwamba tunambeza alochora ramani ya vyumba sita hakuwa na elimu au alikosea.

Kwa mantiki hiyo Chadema wanachokifanya ni kusema HATUWEZI kufanikiwa kulijenga Taifa la leo kwa kutumia ramani na msingi ulowekwa, hii haina maana Nyerere alifanya makosa na katiba yake haitufai bali Katiba ya Nyerere na msingi aloweka ni sawa na ujenzi wa nyumba ya vyumba sita kwa ajili ya makazi ya familia.. Je, alikosea? ndio nasema laa hasha, malengo yetu yamebadilika hivyo ni muhimu sana tukubali kwamba kabla ya kubomoa msingi ulokuwepo ni lazima tuwe na ramani mpya (Katiba).

Marekani hawajawahi kubadilisha Katiba kwa sababu hakuna mabadiliko ktk malengo ya ujenzi wa nchi hiyo. Toka wapate Uhuru wamekuwa wakitumikia mwongozo ktk ujenzi wa Ubepari hivyo itikadi zilizopo zinatofautiana tu ktk matumizi ya jengo hilo ktk kuongeza pato la Taifa na maisha bora kwa wananchi wake. Hivyo sii vizuri kujifananisha na Marekani kuiga vitu kwa sababu Marekani au mataifa makubwa hawajafanya hivyo kama hufahamu tunachokusudia kujenga.
 
Mtu akiwa kiongozi mzuri,akilaumiwa kwa mapungufu yake inakuwa kosa? Hata Nyerere alishakiri kwamba aliwahi kufanya makosa,yeye si malaika...Sasa binadamu hajakamilika,kwa hiyo wanaomkosoa wako sahihi,wasiomkosoa pia wako sahihi ila wanaolaumu Nyerere kukosolewa Nahisi wako wako Wrong!

Huyu Nyerere alikuwa haambiliki, hashauriki, haongeleki, haelimiki....nachokiona yeye ni bora basi it was either his way or the highway. Hapo ndipo alipokuwa akichemsha.
 
Kweli hujafa hujaumbika ! Hata hivyo wengine wetu hatushangai sana. Kikwete kaingia madarakani mwaka 2005 iwe kihalali au hapana lakini ni ukweli Watanzania walikuwa na matumaini makubwa naye wakati huo. Ili kuwaondoa hofu waliokuwa bado wana wasi wasi naye, katika hotuba yake ya kwanza alikuwa na haya ya kusema kuhusu Baba wa Taifa;


Hayo aliyasema wakati huo, lakini leo hii anasita hata kumwita Mwalimu Baba wa Taifa. Badala yake baada ya kutambua kuwa kumbe uongozi wa taifa si lelemama na kwamba hana uwezo wa kusimamia utawala wa sheria, kaamua kwa makusudi kuzitikisa zile nguzo alizozisifia wakati anaingia madarakani. Kwa makusudi ameamua kuunda mtandao ambao kwa kukosa busara anaamini utamnusuru kumbe una hatari ya kuusambaratisha umoja wetu ambao tumejivunia tangu uhuru. Anafikiri anaweza kufunika mapungufu yake kwa kumtupia lawama Baba wa Taifa ambaye siyo tu aling'atuka miaka 26 iliyopita bali kwa sasa ni marehemu asiyeweza kujitetea.

Huu mtandao ambao hivi sasa tunaushuhudia kila leo hadi hapa JF, ni mtandao ambao kwa vyovyote vile hauwezi kufanikiwa kwani ni za kutapatapa kama za mtu anayezama huku kasi ya maji ikizidi. Mitandao yenye malengo maovu ya aina hii huwa haidumu na Kikwete mwenyewe ni shahidi kwani anashuhudia jinsi mtandao uliomwingiza madarakani mwaka 2005 kwa hila unavyomtafuna bila huruma. Amejaribu kuwagawa Watanzania kikabila ameshindwa, amejaribu kidini hakufanikiwa na sasa anajaribu kutugawa kuhistoria. Kama alivyowahi kukiri yeye mwenyewe asithubutu kujaribu kuvaa viatu vya Mwalimu, haviwezi na asipoangalia vitamwangusha chali !

Utafiti kidogo tu unaonesha kuwa wote wanaojaribu kumdhihaki Mwalimu (RIP) ni hao hao wanamtetea huyu Kiongozi aliyekimbilia Ikulu bila kujua atafanya nini akifika hapo. Shuhudia katika hii hotuba yake ya kwanza kabisa Bungeni baada ya kuchaguliwa mwaka 2005 kuhusu Nishati;


Baada ya hotuba hiyo tukaingia mkataba na Richmond na leo hii miaka sita baadaye, ndio hali inakuwa ngumu zaidi na mgao wa umeme ndio hivo tena. Halafu kuna watu wanathubutu kumtetea Kikwete kwa kujaribu kuuandika upya historia ya taifa kwa simulizi za uwongo na zilizojaa chuki. Hapana, mapungufu ya Kikwete yawe ni mzigo wake na awe tayari kuubeba bila kukwepa na bila kumsingizia Baba wa Taifa. Je yawezekana hii yote inasababishwa na Mwalimu mwaka 1995 kuzima mbio za Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumsoma sawa na kuuona udhaifu wake ? Sifa anazopewa Mwalimu iwe ndani au nje ya taifa letu hazitapungua eti kwa sababu ya wivu na chuki za watu wachache wanaotafuta umaarufu bila sifa.
I liked it, logical analysis.
 
[h=2]By The guardian reporter[/h]

28th June 2011

Father of the Nation Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

With the 50th anniversary of the independence of the then Tanganyika (now Mainland Tanzania) being marked on December 9 this year, a researcher from a university in the UK is embarking on a journey to trace the very early years of Father of the Nation Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Dr Thomas Molony, Senior Research Fellow at the Centre of African Studies at the University of Edinburgh is looking for those who knew Mwalimu Nyerere in the first 30 years of his life, a significant period with enormous implications for post-independence Tanzania.
The researcher said in a recent interview at the Dar es Salaam offices of The Guardian that his interest in Nyerere's life is for the period from 1922-1952, adding: "Those were his formative years, when he's beginning to get a world view."
"This history is important because it's obviously the foundations for the nation of Tanzania. It's a part of Tanzania's history which hasn't been much explored," he said.
He explained that a lot is known about Mwalimu Nyerere's time with TANU (Tanganyika African national Union), his subsequent tenure as the first Prime Minister and later as the first President of an independent Tanganyika as the country was then known and his legendary oratory skills.
"He was a phenomenal debater but there is very little biographical data from the early period (which is) very important to where this peaceful nation is now," notes Molony.
He wants to hear from those that knew Nyerere as a child and a young boy at his native Butiama village in Mara Region, as a student at Tabora Boys and later at Uganda's Makerere University and much later at Edinburgh University.
"It's a real insight to hear from people who actually knew him at a time when evidence suggests he was getting political," he said, referring to Nyerere's time from 1949 to 1952 as a history and economics student at the University of Edinburgh, when he had entertained thoughts of joining the Holy Orders before being nudged towards Fabian thinking and socialism.
Molony is working to turn Nyerere's formative years into a book "for the people of Tanzania", whose release he hopes will coincide with Tanganyika's Independence Day celebrations in December.
He is asking that Tanzanians that knew Nyerere personally during this period to contact him at thomasmolony@gmail.com (and cc tics82@yahoo.com), or to call +255(0)767 501602 or +255(0)717 068515.
"I'd like to get all sorts of perspectives from all sorts of people" he said in the exclusive interview.

SOURCE: THE GUARDIAN




 
huyu nyerere alikuwa haambiliki, hashauriki, haongeleki, haelimiki....nachokiona yeye ni bora basi it was either his way or the highway. Hapo ndipo alipokuwa akichemsha.

very true..................
 
Back
Top Bottom