UONGOZI WA MUHAS, HOSPITAL YA MUHIMBILI, WIZARA YA AFYA, NA VYOMBO VYA DOLA: CHUNGUZA TAPP

chhatbhai

Member
Apr 12, 2016
8
1
Wiki mbili zilizopitia niliona humu malalamiko dhidi ya shirika hili la Tanzania AIDS Prevention Programme (TAPP), kuhusu linavyodhulumu watendaji/wafanyakazi kwenye miradi linayosimamia.

Nimejaribu kufuatilia nikagundua kuwa hata wale wa makao makuu yake, nao wanaonja shubiri. Dr. Mbwambo aliwahidi kuwapa shilingi laki mbili kila mwezi lakini masharti yake magumu ya kurpoti kila siku Muhimbili na baada ya hapo kwenda kwenye asasi ya MEFADA iliyo Kindondoni. Ukipiga mahesabu ya nauli tu kila siku, utagundua ugumu. Pia mtoa mada alivyosema kuwa kuna uwezekano mkubwa wafadhili wakubwa , kama Centre for Disease Control-Tanzania, Open Society Foundation na PEPFAR, kusitisha ufadhili wao kwa kuwa kuna ubabaishaji mwingi Ghuluma na Ufisadi), ni kweli kabisa.

Wakati umefika vyombo na wadau husika wafanye uchunguzi ili ukweli ujuliakane, kama kuna watu wanadai basi waweze kupata haki yao.

Suala hili lifuatiliwe kwa umakini sana kwani wafanyakazi waliyokuwa kwenye asasi, zilitajwa na mtoa post, yawezekana wakadhulumiwa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom