TEMILUGODA
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 1,389
- 285
Kwanza naomba MOD waiache hii thread isomwe na ichangiwe.Wana Jf mimi naona kitendo cha CCM kumpitisha Siyoi kitachangia sana kuwa na utitiri wa watoto wa vigogo kurithi nyadhifa za baba zao au wazazi wao maana busara asilia haikutumika kumsihi Siyoi juu ya nafasi hii.KWA KAWAIDA KATIBA YA NCHI HUTOA HAKI KWA KILA RAIA KUCHAGULIWA NA KUCHAGUA, WELL AND GOOD lakini busara au wisdom hutangulia kutoa maamuzi kichama ndiyo maana Nec zipo kusaidia kulinda tamaduni zote kwa kutumia busara za hali ya juu,vinginevyo Nec zikileta maamuzi yenye kigugumizi kama hii ya CCM ya kumleta Siyoi anayenung'unikiwa mpaka,basi tujue watoto hawa wa vigogo watafumuka kama uyoga kwani ni haki yao na hatimaye UKABILA kisha tutaanza kulana kama nyama maana wengine watakataa tawala za kifalme hata kama ni wana chichiem.CHAMA CHENYE NGUVU KITALIONA HILI NA KUISAIDIA CCM KURUDI KATIKA NJIA INAYOZIBWA NA NYASI(MAGAMBA) NA HATIMAYE UMOJA KUTOWEKA MUDA SI MREFU UJAO.