Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,695
- 1,696
Maxence na Mods Wote Wa JF;
Kipindi hiki cha Uchaguzi ongezeko la wanaotembelea na kujiandikisha kuwa members JF bila ya shaka limekuwa kubwa. Hii inashabihiana na ukweli kuwa JF imekuwa mstari wa mbele na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupiga vita maovu na hata kuchangia katika siasa za Tanzania.
Waliomsikia JK bila ya shaka wanafahamu kuwa Rais pia anapata taarifa ya nini kinaendelea katika mitandao. Ni wazi pia Dr. Slaa, Zitto na wanasiasa wengine wengi ni Wanachama wa JF ama wanatembelea JF kupata habari. Ni katika maantiki hii nashauri ni vema JF Uongozi na Mods wakaonyesha uzalendo wa hali ya juu kuliko wakati wowote kwa kuwa stricts kwa kuwa heavy weights wote wa vyama mbalimbali katika kipindi hiki cha Uchaguzi wanapitia posts nyingi. Tusipokuwa makini, JF inaweza kwa namna fulani fulani kuwa source ya mema au mabaya. (NB: Wote mnakumbuka Zeutamu ilivyoleta sokomoko). Sasa hivi JF ina wanachama 10,000 (+ or -).
Ushauri wangu ni kama ifuatavyo:
- Thread na Posts Zozote zisizo na muelekeo wa ukweli zaidi ya Ushabiki, na Uzandiki zisiruhusiwe ama zifutwe mara tu zikijulikana.
- Wale wanaobadili ID mara nyingi na kuendeleza pumba na ligi zisizo na msingi wala tija, wapewe "pumziko la amani".
- Wanaochichea debate za chuki za namna yoyote wapewe ban haraka sana na IP zao ziwe monitored.
- Wana JF washindane kwa hoja na facts bila kukebehiana na katika yote haya Uzalendo wa Nchi na Maslahi ya Taifa yapewe kipau mbele.
Katika hili, niko tayari kutoa mchango wangu wa ziada na Maxe, bila ya shaka nitakuona.
JF inayo nafasi katika siasa za Tanzania, ni wakati sasa iwe na msimamo na kutake advantage ya kuweka vipaumbele vyake.
Wasalaam
Superman!