Uongozi wa Chuo cha Ualimu Kabanga, Kigoma uchukuliwe hatua kwa matumizi mabaya ya fedha za Umma

mwakanga

Member
Sep 2, 2016
6
0
Uongozi wa Chuo cha ualimu Kabanga kilichopo Mkoa wa Kigoma uchukuliwe hatua kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali.

1.Mnamo mwaka 2011 ulipitisha mchango wa shilingi 20000 kwa kila mwanachuo kwa ajili ya ujenzi wa maktaba haikujengwa pesa zikaibiwa.

2.mnamo 2013 mchango ulichangishwa pia kwa Mwanafunzi waliokuwa wanaanza mwaka wa masomo shilingi 20000 kwa ajili ya ujenzi wa maktaba hiyo haikujengwa pia hela zikaibiwa.

3.mwaka 2014 Chuo kupitia uongozi wake kiliingia mkataba na shirika lisilo la kiserikali la EQUIP linalofanya kazi ya kuinua ubora wa elimu kupitia mafunzo ya waalimu wa Shule za msingi, uongozi ulisaini mkataba wa shirika hilo ili wakufunzi shirika liwe linawatumia kutoa mafunzo kwa waalimu wa Shule za msingi na Chuo kitakuwa kinalipwa asilimia 50% ya malipo atakayopewa mkufunzi kila anapowezesha bila makubaliano kati ya shirika na wakufunzi.

4.mwaka 2016 serikali kupitia waziri Mkuu imesitisha michezo kama umiseta .uongozi wa Chuo hicho umechangisha kila mwanachuo 20000 kwa ajili ya michezo ya kanda na zimeibiwa.

Serikali chukueni hatua juu ya Chuo hiki.
 
weka viambata ueleweke vinginevyo ungeweza waona wahusika
viamba gani? Hv kazi ya TAKUKURU na TISS ni ipi katika habari kama hizi? Wanaotukana tu ndo hufuatiliwa? Nina mfano mmoja pia shule ipo mondul wamechangishwa sh elfu 60 kwa kila mtoto tangu 2011 hadi mwaka jana, mara watoto wanaofikia 800 lakini hizo fedha hazijafanyia kazi iliyolengwa. Watu walikuwa wanakusanya fedha za kampeni through jasho la masikini, leo hii ukiripoti unasema weka vielelezo! Ni vielelezo gani vinapaswa kuwekwa kama siyo kuchunguzwa kwa madai hayo? Ina maana ukiripoti jambazi polisi ni kazi ya msamaria mwema kwenda kumshika?
 
Huu ndoo upuuzi wa Tanzania hii badala ya kuchukua hatua za kiuchunguzi unadai vielelezo nini maana ya TAKUKURU NA TISS.
Hawa ndoo wanatakiwa wafuatilie sasa. Au tuache watu waendelee kupiga dili.
 
Hapa ndoo utaona uhuni wa Takukuru badala ya kufanya kazi yao na wao watabugia dili
 
Uongozi wa Chuo cha ualimu Kabanga kilichopo Mkoa wa Kigoma uchukuliwe hatua kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali.

1.Mnamo mwaka 2011 ulipitisha mchango wa shilingi 20000 kwa kila mwanachuo kwa ajili ya ujenzi wa maktaba haikujengwa pesa zikaibiwa.

2.mnamo 2013 mchango ulichangishwa pia kwa Mwanafunzi waliokuwa wanaanza mwaka wa masomo shilingi 20000 kwa ajili ya ujenzi wa maktaba hiyo haikujengwa pia hela zikaibiwa.

3.mwaka 2014 Chuo kupitia uongozi wake kiliingia mkataba na shirika lisilo la kiserikali la EQUIP linalofanya kazi ya kuinua ubora wa elimu kupitia mafunzo ya waalimu wa Shule za msingi, uongozi ulisaini mkataba wa shirika hilo ili wakufunzi shirika liwe linawatumia kutoa mafunzo kwa waalimu wa Shule za msingi na Chuo kitakuwa kinalipwa asilimia 50% ya malipo atakayopewa mkufunzi kila anapowezesha bila makubaliano kati ya shirika na wakufunzi.

4.mwaka 2016 serikali kupitia waziri Mkuu imesitisha michezo kama umiseta .uongozi wa Chuo hicho umechangisha kila mwanachuo 20000 kwa ajili ya michezo ya kanda na zimeibiwa.

Serikali chukueni hatua juu ya Chuo hiki.
Takukuru Kasulu waichukue tip hii
 
Takukuru ya huko kasulu ni wapiga dili tu labda kamanda mkuu,VALENTINO MLOWOLA mwenyewe.
 
Hii ndoo Tanzania ya CCM kamanda wa TAKUKURU VALENTINO MLOWOLA atapotezea tu.wanajuana.
 
Back
Top Bottom