Uongozi na michezo!!

Dec 7, 2008
14
3
Hizi ni data chache tu za mtazamo wa mkuu wa nchi anavopenda michezo.

  1. Kama mkuu kabisa wan chi alisema lazima awalete Real Madrid 2010 wacheze uwanja wa Neshno, sijajua watacheza na Yanga, Simba au Azam…tunawasubiri
  2. Akiwa Spain, alikwenda uwanja wa Real Madrid, akapiga picha pale, akaomba jezi, wakampa (zipo kibao pale)…kwa kweli sijui kama ilikuwa ni ofisho tripu pale au aliamua tu kupiga site tour!!
  3. Kijana wetu mtanganyika anayecheza kikapu cha kulipwa Marekani akaja home vekesheni, nadhan na kujitangaza kidogo, mkuu wa nchi kuonyesha anavyopenda michezo akamualika Ikulu, likapigwa bonge la dinner, dogo akauza sura magazetini, then akasepa…..Tusisahau ni dogo huyu huyu alitemwa kwenye kikosi cha kwanza kwenye timu yake, ikalazimu aende mchanagni ya kule (nasikia ame-bounce back, yupo kwa nba tena…ingawa sijabahatika kumuona kwenye luninga yangu…nadan ni ya kinyumbani zaidi! Well, nawakumbusha tu, star huyu, aliyeuzisha sura hadi Ikulu akaja Dar vekesheni nyingine, akatuonyesha kuwa ana fani nyingine pia..Ndondi za kitaa!! Kisa? Eti yeye mtoto wa Sinza….Ok, tuyaache hayo….hii iliyofuata ndiyo kali
  4. TFF wakaalika Brazil, nadhani mkuu wetu akawapiga tafu, Benki zikaacha cubana, bilioni kadhaa zikatoka, chama linalopendwa sana likaja uswazi, tukapigwa 5, Tanzania ikaonekana dunia nzima, mkuu wa nchi (Na wapambe ofkoz) wakauza sur ana wachezaji wa timu pinzani………game izi ova!!

Mimi najiuliza maswali mengi sipati majibu…hivi SIRIKALI hii inao washauri wazuri kweli?? Tumeshindwaje kuyatumia mabenki kupata hela za kuwaleta mastaa wetu wote ulaya watusaidie kuiondosha Rwanda tunapoteza hela kwa mechi ya kuuza sura?

Kwa mtazamo wangu, YES NI MDOGO/FINYU, Tanzania inaelekea ulimwengu wa peke yake katika kila sekta!! Nakubali sasa Tanzania bila kiongozi/viongozi inawezekana!!
 
Kujibia swali lako la mwisho....mechi ya Taifa Stars na Rwanda ilikuwa ni kwa wachezaji wa ndani (yaani wasiocheza soka nje ya nchi zao or rather nje ya bara la Afrika).... Hivyo wachezaji wa kulipwa hawa qualify kushiriki.
 
Kujibia swali lako la mwisho....mechi ya Taifa Stars na Rwanda ilikuwa ni kwa wachezaji wa ndani (yaani wasiocheza soka nje ya nchi zao or rather nje ya bara la Afrika).... Hivyo wachezaji wa kulipwa hawa qualify kushiriki.

Nimepata kifungu cha katiba ya CAF kinachotoa ufafanuzi wa mashindano ya CHAN

Article 2
The African Nations Championship is open to the national representative teams of
the associations affiliated to CAF, composed exclusively of national players playing
in the national championship, each association being entitled to enter one team.
 
Back
Top Bottom