Uongozi mpya UVCCM: Mwenyekiti ni JUMA SADIFA; Makamu Mwenyekiti ni MBONI MHITA

HAWA VIJANA WAKAE MTAZAMO WA KUJENGA UCHUMI NA SIO KUIMALISHA CHAMA. Inabidi wafanye study tour nchini marekani, Israel na Uingereza waone vijana wenzao wanatoa mchango gani katika kufuta ukosefu wa ajira ktk nchi zao na wao wataibanaje serikali ku create more jobs kuliko kugharimia vikao vya NEC.

waje USA, halafu watembelee financial district pale low mnhatan,. Hapo watafika mpaka new York stock exchange. Pale new york stock exchange pana maktaba ambamo kuna watu wa kila rika, wanajua uchumi karibia wa dunia nzima na ushauri wao husisimua sana.. ni vizuri wajifunza Ulaya magharibi na USA walifanikiwaje mafanikio makubwa ya kiuchumi kuliko kwenda China na Urussi kujifunza propaganda za kulaghai umma. Maneno kama magamba, Kubobea na mengine ni propaganda za kuchezea akiri za watu tuu uawtawalao. Hivyo nyie vijana badilikeani.
Kama safari za Marekani zingekuwa zinafundisha wa kwanza kuelimika angekuwa JK lakini wapi, Alikwina.

Hao unaotaka waje kufanya study tour USA sana sana watakuja kupiga picha kwenye maeneo yanayovutia na kufanya shopping tu hakuna la ziada. kitendo cha wao kuwa UVCCM tayari ni ishara kwamba wapo kwenye Training ya Ufisadi.
 
Inakuwaje kwenye nafasi nyingi kwenye hizi chaguzi za CCM wanaochaguliwa wanahusika na vyombo vya habari (Mainstream Media)? Na ni kwa nini tunaambiwa hao wote wanamuunga mkono Lowassa?!
Swali la kitoto kabisa hili, mtu ambaye hajafikia hata level ya kujimudu yeye binafsi kimaisha anapata wapi pesa za kuhonga kila mpiga kura tsh 200,000/=? Media zinamilikiwa na wanasiasa hakuna la kushangaza hapo.
 
Kama safari za Marekani zingekuwa zinafundisha wa kwanza kuelimika angekuwa JK lakini wapi, Alikwina.

Hao unaotaka waje kufanya study tour USA sana sana watakuja kupiga picha kwenye maeneo yanayovutia na kufanya shopping tu hakuna la ziada. kitendo cha wao kuwa UVCCM tayari ni ishara kwamba wapo kwenye Training ya Ufisadi.
Pia watakachojifunza kingine ni kupiga picha na kina 50-Cent, Boys II Men, na labda kujifunza "batter trade" mfano suti kubadilishana na kigamboni, n.k.
 
jonas Nkya kutwa yuko kona bar anakamata micangudoa eti leo mjumbe wa NEC ..hivi hiki chama kiko serious kweli
 
Swali la kitoto kabisa hili, mtu ambaye hajafikia hata level ya kujimudu yeye binafsi kimaisha anapata wapi pesa za kuhonga kila mpiga kura tsh 200,000/=? Media zinamilikiwa na wanasiasa hakuna la kushangaza hapo.
Utoto wa swali uko wapi. Wewe nawe umetoa jibu la Kitoto kabisa! unadhani kila media hapa tanzania inamilikiwa na wanasiasa? Halafu wewe ulihongwa hizo 200,000? Tusidhani kila wakati tuko sahihi kwani sisi si watengeneza Usahihi!! Mimi sijauliza wanaochaguliwa kama ni wamiliki wa vyombo vya habari bari waaandishi wa habari hapo kuna tofauti kubwa sana kati ya mmiliki na mwandishi wa habari kama wewe unaona wanafanana basi jua una tatizo kwenye kufikiri kwako.
 
Mkt- SADIFA JUMA KHAMIS
M.Mkt- Mboni M. Mhita.

WANEC
1. Jerry Slaa
2. Deo Ndejembi
3.Anthony Mavunde
4. Jonas Nkya
5. Petro Magoti (mlemavu wa viungo)
6. Fatma Jumbe (mlemavu wa Ngozi)

Chezeya LAIGWANANI weye! Bado na wazazi akamilishe wale wanafki safari ya CCJ imewadia, MJINI MIPANGO KIJIJINI KILIMO Maskini kuna vijana wameondoka Dodoma usiku wameropoka sana, hayawi hayawi.. azimio la Pwani chali mh. Ulega aibuuu! Kama Rizone anawapenda sana awape ukuu wa wilaya coz kila NAFASI ya kugombea hamtashinda coz hamchaguliki HAPPI and the team muulizen Musiba analia maumivu haaahaaaa Olivia Sanare! Chaliiiii. Jamani siku zote mwenye nguvu Mpishe NAPE upooooo! Ooooh eeeeeh Sijui nini chaliii Sasa it's official T2015EDO. SKY IS THE LIMIT


Watu kama wewe huwa najiuliza mnapata wapi akili za kumsifia mtu anayetumia pesa kupata madaraka? hivi kwa akili za shule ya msingi kwako ni sawa? hivi mtu akitumia hela visivyohalali kukuharibia malengo yako binafsi utafurahi?
 
Umoja wa vijana wenye nacho na wahaidiwa vyeo. Kazi ipo sijui watoto wamaskini wataambulia kuwapigia kura mafisadi na makuwadi wao!
 
Utoto wa swali uko wapi. Wewe nawe umetoa jibu la Kitoto kabisa! unadhani kila media hapa tanzania inamilikiwa na wanasiasa? Halafu wewe ulihongwa hizo 200,000? Tusidhani kila wakati tuko sahihi kwani sisi si watengeneza Usahihi!! Mimi sijauliza wanaochaguliwa kama ni wamiliki wa vyombo vya habari bari waaandishi wa habari hapo kuna tofauti kubwa sana kati ya mmiliki na mwandishi wa habari kama wewe unaona wanafanana basi jua una tatizo kwenye kufikiri kwako.
Aisee sijawahi kutilia shaka upeo wako hapa JF lakini leo unanishangaza sana, labda tuanze na media 4 kubwa hapa Tanzania ili unielewe vizuri.

IPP Media - Mmiliki Mengi, yuko tayari kutumia media zake pale alipo na maslahi napo.

Freemedia - Mmliki ni Freeman Mbowe, kama kuna habari zenye maslahi ya Chadema ni lazima zipewe kipaumbele.

Habari Corporation - Mmiliki Rostam Azizi, Mkurugenzi Hussein Bashe, hapa habari yoyote ya kumshambulia Lowasa haina nafasi.

Mwananchi - Mhariri Mkuu Zitto Kabwe, hapa habari za Urais wa Zitto ndio nyumbani kwake na mwandishi maalum aliyekodiwa kwa kazi hii ni Ramadhani Semtawa.

Al Nuur, Al Huda, hapa habari za kigaidi na uchochezi ndio first priority na siyo current issue za kisiasa.

Je bado unadhani uko sahihi kwa unachokiamini? unafahamu kwamba kila kampuni ina Policy zake? ukitaka kufukuzwa kazi Star Tv basi unesha picha ya tukio lolote la Mbunge wa Ilemela , basi ujuwe na kazi huna.
 
Mbona Wajumbe wa NEC uvccm hakuna waislam?huyo mwenyekiti katoka zanzibar.waislam bara mpo wapi na ccm yenu?

CCM nacho ni chama cha kidini siku hizi? Hata hivyo, nawafahamu Wakristo kadhaa wenye majina ya Kiislamu.
 
Gari la Waziri lahusishwa kwenye wizi *
Tuesday, 18 January 2011 21:38

Sadick Mtulya *

JESHI la Polisi Mkoani Morogoro, limekamata gari la Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya likihusishwa kubeba tani 30 za* madini* ya shaba iliyoibwa mkoani Morogoro.

Shaba hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh 300 milioni* iliyoibwa wakati ikisafirishwa kutoka nchini Zambia kuelekea jijini Dar es Salaam.* Pia, jeshi hilo limemtumia mtoto wa waziri huyo, Jonas Nkya kumtia mbaroni mmoja wa watuhumiwa ambaye alikuwa ni meneja wa hoteli inayomilikiwa na waziri Nkya.* *

Gari* hilo aina ya Toyota Surf lililokamatwa Jumamosi iliyopita, linashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro.** Taarifa ambazo zilipatikana* jana* na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Adolpine Chialo, zilisema gari hilo lilitumiwa na mtuhumiwa* (jina linahifadhiwa) ambaye ni meneja wa hoteli moja , inayomilikiwa na Waziri Nkya. *

“Tumelikamata gari aina ya Toyota Surf inayomilikiwa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Nkya kutokana na kuhusika kubeba madini ya wizi Januari 11 mwaka huu majira ya saa 3 usiku eneo la Madafu barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam,’’ alisema Chialo.

*Akaongeza: “ Gari hili lilitumiwa na meneja wa hoteli inayomilikiwa na Dk Nkya.’’* Kamanda huyo alieleza kuwa , kabla ya tukio kufanyika, mtuhumiwa aliidanganya* familia* ya Nkya kuwa gari hilo lilikuwa bovu na kwamba lilitakiwa kufanyiwa matengenezo. *

“Ndipo huyu mtuhumiwa akatumia mwanya huo kubeba madini haya,’’ alisema.* Hata hivyo, Kamanda huyo alisema polisi walilazimika kumtumia* mtoto wa waziri, Jonas Nkya ili kufanikisha kumpata Meck kutokana na kukimbia baada ya kufanya tukio hilo. *

“Si kweli kwamba polisi inamshikilia Jonas kwa tuhuma za kuhusika* katika tukio hilo ila* tulimtumia kufanikisha kumpata mtuhumiwa* na si vinginevyo,’’ alisema. *

Mbali na mtuhumiwa huyo,watu watatu pia wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo huku watuhumiwa wengine tisa wakitafutwa.* Juzi Kamanda huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa shaba hiyo ilikuwa imepakiwa kwenye gari aina ya lori Scania lililokuwa likiendeshwa na mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa ambaye ni mkazi wa Mafisa Manispaa ya Morogoro. *

Alisema* baada ya polisi wa kikosi cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha kupata taarifa za kutelekezwa kwa gari hilo ambalo ni mali ya Dhandlo Road Haulage T. Limited eneo la madafu walilifuatilia na kulikuta na shaba pamoja na nyaraka za shaba hiyo na kwamba baada ya uchunguzi wa haraka alikamatwa dereva wa gari hilo jina limehifadhiwa ambaye alitoa ushirikiano kwa polisi na kufanikiwa kukamatwa kwa wenzake.* *

Katika mahojiano na polisi watuhumiwa hao waliweza kuonyesha mahali ilikofichwa shaba hiyo eneo la Forest Hill na hivyo polisi kufika katika eneo hilo ndani ya nyumba ya mtu mmoja jina limehifadhiwa* ambaye kwa sasa yuko masomoni mkoani Dodoma na kwa kipindi kirefu nyumba hiyo aliachiwa mmoja wa watuhumiwa hao jina limehifadhiwa* ili kuishi.* *

Alisema madini hayo yalikuwa yamefichwa katika nyumba hiyo kwa kufukiwa ardhini na juu kumwagwa mchanga na kwamba yaliweza kufika katika nyumba hiyo baada ya mmoja wa watuhumiwa hao jina limehifadhiwa ambaye ni dereva wa winji kuyatoa huko porini lilipoachwa gari hilo na kuyashusha katika eneo hilo.* *

Kamanda Chialo alisema polisi wanaendelea na zoezi la kukagua eneo la nyumba hiyo pamoja na kuimarisha ulinzi wa saa 24 ili kubaini mali na vitu vingine ambavyo vinaweza kuwepo katika nyumba hiyo na kwamba tayari mmiliki halali wa madini hayo ameshatambulika na uchunguzi zaidi kuhusina na tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wengine waliohusika katika tukio hilo kwa namna moja ama nyingine ili waweze kufikishwa mahakamani.
 
Waacheni wajipange; haya ni mambo yanayoendelea CCM na CCM inajipanga kuelekea 2015. Swali kubwa nii je mabadiliko yote ya uongozi yanayofanywa ndani ya CCM sasa hivi yatakisaidia vipi chama kuendelea kutawala 2015?

Kwa ninachokishuhudia hapa Dodoma tangu uchaguzi wa UWT na sasa UVCCM naoma hatari mbele si kwa UWT, UVCCM na CCM tu, bali wka taifa. Kama CCM ndio wanajipanga hivi, kwa kutumia rushwa kuupata uongozi, basi tusitarajie mabadiliko yoyote ya maana kama nchi iwapo viongozi hawa wanaochaguliwa ndio watakaokuwa na jukumu la kuunda serikali 2015. Zamani ilikuwa inasemwa kuwa ni vigumu kukamata watoa na wapokea rushwa kwa sababu jambo hilo hufanywa kwa siri, lakini hapa Dodo, na hata kwenye Chuo cha Mipango ambako chaguzi hizo zinafanyika, rushwa kutolewa na kupokelewa si siri tena. Kinachoshangaza ni kwa nini wanaohusika kupiga vita rushwa wanashindwa kuwakamata. Au labda kwa sababu fedha zinatolewa hadharani basi imekoma kuwa rushwa.
 
duh, si mchezo, hongereni sana washindi! Jonas Nkya ndani ya nyumba!
 
Yawezekana! Ningemuona Paul Makonda ndani, hapo ningesema EL kapigwa chini.
Mkuu wimama, Makonda amepigwa dafrau la hguvu jana jioni wakatio wa uchaguzi wa marudio kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti. Kura zilirudiwa wakishindanishwa yeye na Mboni. Ilipotangazwa kuwa kura zinarudiwa ilikuwa wakati wa uchaguzi wa wajumbe wa NEC lakini ghafla ukumbi ulibaki mtupu. Bashe na timu yake walitoa wajumbe nje kuwaweka sawa. wapo wajumbe kutoka mkoa mmoja ambao walishindwa kukubaliana na ngumi zilifumka kwenye ukumbi usiku wakati wanapiga kura baada ya wajumbe ambao hawakutaka kumpigia Mboni kuwagomea wenzao ambao walishakama mkwanja
 
Last edited by a moderator:
Hawa wote ni wafuasi sugu wa Lowassa. Ushindi wao umetokana na nguvu na ushawishi wa Lowassa. Hongera Lowassa, rais mtarajiwa wa Tanzania 2015.
Endelea kujidanganya we mnyisanzu wake alikuwa JAMALI aliyeytoswa, baada ya hapo akatapatapa Kama kawaida yake mzee fisadi. Halafu usikurupuke kuandika usoyajua.
 
MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe. JUMA SADIFA - 2012-2017
MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe.MBONI MHITA

HONGERENI SANA!!! UVCCM HOYEEEE

WAJUMBE NEC

Jerry Silaa
Deo Ndegembi
Anthony Mavunde
Jonas Nkya

OOH jaman Jembe langu Salum Hapi wamemkaanga? kweli CHICHI EM chi mchejo!
 
Back
Top Bottom