Uongozi mpya UVCCM: Mwenyekiti ni JUMA SADIFA; Makamu Mwenyekiti ni MBONI MHITA

Acha kuipotosha akili yako, hao wote ni dini moja nayo ni ufisadi. Ukristo na Uislamu unaujuwa wewe. uliza hirizi nyekundu zilivyookotwa ukumbini utadhani kama condom zinavyookotwaga unapolala mwenge.

dini yao ufisadi, na mungu wao ibilisi
 
gazeti la jana la mwananchi lilimtaja mboni na juma sadifa kwamba wanaungwa mkono na kambi ya lowassa kwa maana hiyo ushindi wao unaashiria kwamba Lowassa hakamatiki ndani ya ccm.
 
Mboni utaweza? kwa jinsi CCM ilivyochafuka (nuka) Rushwa? na kwa wanaokulinganisha na Malema wanakosea maana katika CCM hakuna kijana anaeweza kusimama hadharani na kusema kama Julius Malema. Wewe kula maisha miaka yako iishe uende zako.
 
Inaelekea UVCCM wapo smart na hawajajihusisha na makambi nini, mbona hakuna mtu anayeongea kwa uhakika kuwa huyu ni kambi ya huyu? Tujuzeni, kati ya hawa nani yupo kambi ya nani?
 
kama Nape yamemshinda sina hakika kama Juma na Mboni watayaweza. in short wameongeza idadi ya wajumbe watakao isindikiza ccm kifoni
 
Mhhh, Mboni????

Mtoto wa Zabein??

Na Sadifa mshua wake nae si mbunge au???

hongereni, na karibuni kitaa

ILA NAHISI UVCCM HAMKO SIRIAZ KABISA KUMPA MBONI

sure, hawako sirias kumpa mboni, kwa staili hii naanza kukubali kweli vichekesho claudstv kwamba itafikia siku rais(president) akawa mteja(mvuta madawa ya kulevya)
 
Safi sana ccm kwa kuchagua timu nyepesi ambayo haiwezi kusimama kwa hoja dhidi ya Bavicha. Sasa kazi kwako John Heche kuwavuna vijana toka kona mbalimbali za nchi hii kwa ajili ya kuunganisha nguvu na Bavicha kwa ajili ya mustakabali wao na nchi yao.
 
Inaelekea UVCCM wapo smart na hawajajihusisha na makambi nini, mbona hakuna mtu anayeongea kwa uhakika kuwa huyu ni kambi ya huyu? Tujuzeni, kati ya hawa nani yupo kambi ya nani?
Shirikisha ubongo wako kabla ya kuposti kitu, uchaguzi wa UVCCM ni Big Victory kwa Edward Lowasa na kama unajuwa Football ni kwamba amepiga Hat trick. Pasco msaidie huyu raia hajui kwamba mko serious.
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji, jibu ni kwamba hawana jipya wote hao maana wameingia madarakani kwa ajili ya kumsaidia mtu kufikia malengo yake na siyo kukisaidia chama kushinda chaguzi, hivi Mhe. Sadifa anaweza kumshawishi nani amchague mtu? Hata hao akina Lowasa waliohangaika kumuweka huyo Sadifa na huyo Mboni wao wamepoteza pesa zao na muda wao bure tu, hatoweza kujenga hoja yoyote ile popote pale hivyo wametumia pesa nyingi sana kuweka maboya tu

If that is the case then you have to relax and wait to take over. Wao CCM wanaamini hiyo ni safu ya kuendelea kuwaweka madarakani.Kila watakachofanya ni katika kuhakikisha uhalali wa kutawala unaimarika zaidi na zaidi.Yule anayetaka kutake over sasa aoneshe zaidi ya hawa.
 
Ivi kwa nini hata uchaguzi wa ndani wa CCM unapata followeres wengi, wakati tumeaminishwa kwamba hiki chama kimejifia, wakuu hatuoni kwamba tunavyokipa kipa kipaumbele tunaki-popularise at the expence ya chama chetu CDM?

Mkuu, Msiba na harusi, yote ni matukio yanayovuta umati wa watu, hasa Msiba kwasababu hakuna kadi za mwaliko.
 
Umeambiwa hizo nafasi zilikuwa zinagawiwa kama za viti maalum?

....Be a Great Thinker, Comrade.
Kipaumbele kwa akina mama hakiji kwa kugawiwa Viti Maalumu vya Dezo tu.
Chama Kinachotekeleza Sera kinazojiwekea lazima kingehamasisha wanachama wake wanawake Kujitokeza kwa Wingi ili kugombania nafasi za Chama zilizopo.
Hii ingewezesha kwa Mfano, nafasi ya Uenyekiti kuwa na Wagombea wengi wakina mama na kwa maana hiyo Uwezekano wa Kuchaguliwa Mwanamke kuwa mkubwa na hivyo kutekeleza Sera ya Chama husika ya kuwapa Kipaumbele akina mama kwenye nafasi za Uongozi za Chama kwa vitendo badala ya Bla bla za Majukwaani
tu.
Hili mbona hata mwanafunzi wa Darasa la Kwanza angeweza kulielewa tu bila mimi kulazimika kumtafunia kila kitu Yeye aje Kumeza tu, Comrade.


 
Hawa wote ni wafuasi sugu wa Lowassa. Ushindi wao umetokana na nguvu na ushawishi wa Lowassa. Hongera Lowassa, rais mtarajiwa wa Tanzania 2015.
HAWA VIJANA WAKAE MTAZAMO WA KUJENGA UCHUMI NA SIO KUIMALISHA CHAMA. Inabidi wafanye study tour nchini marekani, Israel na Uingereza waone vijana wenzao wanatoa mchango gani katika kufuta ukosefu wa ajira ktk nchi zao na wao wataibanaje serikali ku create more jobs kuliko kugharimia vikao vya NEC.

waje USA, halafu watembelee financial district pale low mnhatan,. Hapo watafika mpaka new York stock exchange. Pale new york stock exchange pana maktaba ambamo kuna watu wa kila rika, wanajua uchumi karibia wa dunia nzima na ushauri wao husisimua sana.. ni vizuri wajifunza Ulaya magharibi na USA walifanikiwaje mafanikio makubwa ya kiuchumi kuliko kwenda China na Urussi kujifunza propaganda za kulaghai umma. Maneno kama magamba, Kubobea na mengine ni propaganda za kuchezea akiri za watu tuu uawtawalao. Hivyo nyie vijana badilikeani.
 
Hii kweli shughuli asee haya na tuone watafanya nn ila kama alivyoseba Robson kweli Lowasa dume la mbegu hakika hapo hata Dr.Slaa aanze kujipanga ishaanza onesha he is unstoppable vyovyote vile lazima Lowasa apite kama mgombea Uraisi CCM na akipita tuu tayari ameingia Ikulu ngojeni muone na iwapo hatasimama CCM basi Slaa atapeta 2015
 
Inakuwaje kwenye nafasi nyingi kwenye hizi chaguzi za CCM wanaochaguliwa wanahusika na vyombo vya habari (Mainstream Media)? Na ni kwa nini tunaambiwa hao wote wanamuunga mkono Lowassa?!
 
MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe. JUMA SADIFA - 2012-2017
MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA NI Mhe.MBONI MHITA

HONGERENI SANA!!! UVCCM HOYEEEE

WAJUMBE NEC

Jerry Silaa
Deo Ndegembi
Anthony Mavunde
Jonas Nkya

ila mkuu, nafasi za wajumbe bara si zipo sita, mbona hapo na
ona 4 tu?
 
"Wapiga kura wamenunuliwa kwa mpaka 200,000, Upepo umebadilika dakika za mwisho ila watu wengi wanamkomoa JK kwa kumpa mboni ambaye hafai kwa kuwa mtu walietaka awe makamu jina lake lilikatwa kwa interest zao ambaye ni mavunde"

Mwisho wa kunukuu!!
 
Back
Top Bottom