Uongozi mpya CHADEMA Ukonga wapatikana - M. Aweda Ndani

Fund raising ya kesi ya Mpendazoe.

Hii ni dalili kwamba huifahamu jiografia ya jimbo la ukonga. Mpendazoe yuko jimbo la segerea lakini hiyo haituzuii kumfanyia fund raising kama hitaji hilo maadam ni mpiganaji mwenzetu.

Hii ni dalili kwamba huifahamu jiografia ya jimbo la ukonga. Mpendazoe yuko jimbo la segerea lakini hiyo haituzuii kumfanyia fund raising kama hitaji hilo maadam ni mpiganaji mwenzetu.

Du kweli, hapo mimi nilikuwa najua ni yale yale tu. Lakini fanyeni nusra msaidieni huyu mpiganaji aendeshe kesi yake.

Kwanza kabisa kwa nafasi ya upekee kabisa ninaomba niwapongeze makamanda tuliowapa ridhaa ya kukiongoza chama huku jimboni Ukonga. Kimsingi CDM kimekuwa chama chenye nguvu katika maeneo yetu lakini tulikosea sana katika kumsimamisha mgombea wa Ubunge Jimbo la Ukonga mwaka 2010, Mzee Binagi ambaye naweza kusema hakupiga kampeni kabisa na kura alizozipata ni kwa sababu wananchi walikuwa wanahitaji mabadiliko yalioletwa na CDM karibu nchi nzima. Mbunge wetu aliyepo hakuna anachokifanya zaidi ya kusinzia Bungeni wananchi wanapata tabu za barabara husuani wale wanaokaa Mombasa kuelekea Moshi Bar, Kivule Mpaka Msongora, watu wa Mongora Ndege hawana daraja la uhakika lakuvukia Mto msimbazi wakati wa Mvua ni baraa tupu. Wahanga wa mabomu wa Gongolamboto mpaka leo hawajafidiwa mpaka leo wanabaki kuhangaika. Migogoro ya Ardhi katika maeneo ya Chanika na Kivule kuelekea Msongora, kutokuwa na soko la uhakika katika eneo letu la Ukonga.

Pamoja pia na kuwa na diwani aliyechaguliwa kuwa Meya wa Ilala Mh Jerry Slaa hamna chochote anachotusaidia zaidi ya kuonekana kwenye TV na kusafiri kwenda nje ya nchi na amebakia kuleta majibu ya kebehi na dharau kwa wananchi. Na anajiandaa kugombea ubunge 2015 kupitia Magamba. sasa basi CDM tunahitaji kujipanga kwa nguvu kuhakisha tunapata Mgombea mwenye nguvu na utashi wa kuongoza na kutuletea maendeleo jimboni. So vijana tupo tayari kwa mapambano na kutengeneza mtandao wa ushindi 2015, kazi kubwa tuliyonayo ni kufungua matawi jimboni na kupata wanachama wengi. Kwa ushauri na lolote tuwasiliane makamanda kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya kukistawisha chama.

Mkazi wa Ukonga na Mwanachama hai wa CDM-Ukonga Madafu

Wapiga kura ndio wamekwisha amua, hawawezi kukichagua cha kingine zaidi ya CCM, ukonga ni CCM tu.
sasa wewe ni mpiga kura au wapiga kura?
Tuna majanga mengi ya kitaifa, mojawapo ni watu kama huyu.
Mungu akusaidie!

maana ukonga ni ya mali ya CCM. Pia huu muundo kuwa na viongozi wa majimbo unafanana na ule wa wilaya kama wa CCM au huu ni muundo mpya?
wewe na watu kama wewe ni janga la kitaifa. Unahitaji maombi, uwe mzalendo. Una tatizo kubwa sana kama hiki ndicho kikuwekacho mjini...

WanaCHADEMA tuondoe ndoto ya kuwa na mbunge au rais kipitia CHADEMA kama hatufikirii jinsi gani hizi nafasi za chini kabisa kama ujumbe na m/kiti wa serikali za mtaa, wajumbe na m/kiti wa kijiji n.k Ila nafasi hizi kuwa za CHADEMA tutausiklizia urais, ubunge na udiwani. Chukua mfano mrahisi sehemu nyingi ambazo CHADEMA imepata uwakilishi ni maeneo yale tu ambayo mwitikio wa wananchi ni mkubwa kwa CHADEMA mfano kuwa na wanachama wengi ngazi za chini na pia uwakilishi kwenye ngazi hizo

Rai yangu kwa uongozi wa CHADEMA popote pale tuanze sasa kabla ya uchaguzi wa serikali za mtaa wa 2014, tuhakikishe kuwa nafasi hizi za chini (mtaa, tarafa, kijiji n.k zinapata wawakilishi kutoka CHADEMA ili kuimarisha ustawi wa chama.

M. Aweda,
Nafahamu uwezo wako, natambua ndoto yako na ninahaidi mshikamano katika kuhakikisha tunaboresha maisha ya Wana-Ukonga. Lengo letu si Uongozi bali hali nzuri ya masiha na maendeleo ya Watu wetu.
Hongera sana

hongera maranya, tunategemea mabadiliko jimbo la ukonga, binafsi nakukubali maranya kwa mambo yako!

Mwita Maranya toa jina lako kamili, nilikuwa mmoja wa wapiga kura jina la Mwita Maranya halipo kati ya walioshinda. Kama jina lako halisi si jingine jitambulishe sasa tukujue. Kati ya wajumbe wanne wa kamati ya utendaji jina wewe ni nani? Hilo jina halikukuwepo.

mkuu naheshimu mtazamo wako lakini tukubaliane kwamba nimeleta taarifa hapa kwa wadau, sijui kujisifia kunatoka wapi. Ama kung'ara imekukwaza? Tunaomba support yako mkuu tuikomboe hii nchi.

Mbona list ya viongozi wote niliyotumiwa na rafiki yangu jana jina la mwita Maranya sijaliona. Maranya aache uwoga atuambie yeye aligombea uongozi kwa jina gani? Jina la Aweda nililiona na nimesikia ameshinda kwa karibu 80% dhidi ya mkiti wa Zamani. Kama wewe ni mwoga hivyo utaweza mapambano ya Chadema? tuambie ulitumia jina gani?

mkuu kwenye website ya chama(cdm) kuna form ya kujiunga na chama tunawaelekeza watu wenye nia ya dhati kujiunga na on line lakina majibu hayapatikani kama form imeshafika makao au mtu anaye shughulikia website ajitahidi kurespond ilitupate wanachama wengi
n;b viongozi wetu wapya hakikisheni mnafungua matawi mengi mapya mf; majohe hatuna tawi la cdm kama lipo naomba nijulishwe hapa jamvini na sehemu zote za jimbo letu la ukonga

Mwita Maranya toa jina lako kamili, nilikuwa mmoja wa wapiga kura jina la Mwita Maranya halipo kati ya walioshinda. Kama jina lako halisi si jingine jitambulishe sasa tukujue. Kati ya wajumbe wanne wa kamati ya utendaji jina wewe ni nani? Hilo jina halikukuwepo.

Muhimu ni kwamba kati ya hayo majina manne Mwita Maranya yumo. kutaja jina lake halisi ni uamuzi wake atakapoona inafaa kufanya hivyo.

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom