Uongo wa Mwanamke wa Daraja la Sarenda.

Njia hii ni nzuri kwa kuwafukuza omba omba, mkuu wa mkoa anaweza kuitumia hii hata kwa wamachinga, pia na takukuru watafute njia kama hii ktk kuwatisha wote wanaopokea na kuomba rushwa, watafute uvumi kama huu,
 
Nasisitiza dawa pekee ni DAMU ya YESU

Dawa ya umaskini au dawa ya "watu kupotea katika mazingira ya ajabu"?

Kama ni kuhusu umaskini soma Kumbukumbu la Torati 15:11.

Sina biblia ya kiswahili hapa lakini kwa kiingereza Deuteronomy 15:11 - "There will always be poor people in the land. Therefore I command you to be openhanded toward your brothers and toward the poor and needy in your land."
 
Uzushi wapi?
Maana hili halikuanzia hapa JF kumbuka limeanzia mtaani hukohuko kabla ya kuja JF.
Unadhanije kwamba ni uzushi? kwani nini uanadhani haiwezi kuwa kweli?

Mkuu,

Mimi nadhani ni uzushi katika njia hizo hizo ulizo tumia wewe kudhani hii issue inaweza kuwa kweli.
Unamkumbuka aliye leta habari hii hapa JF?mwambi basi atetee hili kwa vithibitisho ili sisi wengine tukubari ni ukweli tufanye maombi.
 
Uvumi wa mwanamke aliyeota manyoya na kisha kupotea umeleta athari nyingi sana.
miongoni mwa athari hizo ni kwamba wale watoaji sadaka kwa ombaomba wa maeneo ya daraja hilo na ombaomba wengine waliozagaa kwenye mitaa mingi ya jiji hili wamekuwa wazito kutoa hizo sadaka na kupelekea kipato cha maomba omba kupungua.
Mwanangu anayesoma Olympio amekuwa akiweweseka usiku kwa kuongea maneno yasiyoeleweka. Ukimwamsha na kumuuliza alikuwa anaota nini, anakwambia kuwa ameota konda kamteremsha Sarenda darajani halafu kakutana na mtu mwenye manyoya ya paka kampeleka kuzimuni.
Mwanangu amekuwa akikosa raha na amekuwa mwingi wa mawazo, kula yake imekuwa ya taabu na hana raha kabisa.

Pole sana Kaka..
ila kaka hii post yako nadhani haikupaswa kuwa katika hili jukwaa (la siasa),this is a political forum,so me nawashauri wana JF, tuwe tuna post thread zetu kwenye apprpopriate forums.
Nawakilisha
 
Ukweli wale Omba omba huwa waanikwaza sana. huwa kila siku najiuliza inawa kweli hawana hata ndugu wa mbali ambao ana uwezo kidogo kuwasaidia? sisi wengine mbona tuna ndugu huko vijijini mbao wengine ni wazee sana na wengine hawajiwezi, tunajitahidi kuwasaidia? ukweli wanakera sana. Natamani sana siku niamke nisione hata ombaomba mmoja

Ombaomba ni sehemu ya matokeo ya malezi mabaya, elimu mbaya ya kijamii, huduma mbaya za kijamaii na siasa mbaya za nchi zinazofukia matumaini na haki za binadamu.
Hivyo ukiona ombaomba ni wengi basi jua jamii ama nchi yetu ni ya aina gani na ukiona wanakukwaza basi jua hao ombaomba na sehemu kubwa ya jamii yetu ni desperate kuliko ulivyo kimaisha pia inaashiria umeeimika ama ulipata malezi mema kibinafsi.
 
Habari ya mtoto inaendeleaje mzee, I hope umemfanyia cancelling kwanihilo sio tatizo la hospital. kama anaendelea na ndoto mpeleke ktk maombi na afanyiwe cancelling yatosha, kisha mueleze asipendelee kukaa ktk story za aina hiyo zitampatia matatizo at the end.
 
Ikiwa wazazi ndio tunaanzisha na kuendeleza uvumi wa vitu kama hivi leo mnategemea ati maombi,maombi gani hasa tunategeea yataponya watoto wetu?
Tunawafundisha uongo wenyewe wakikua na tabia hizi za uongo na uzushi tutalaumu nani?
 
Hivi ombaomba haezi kusaidiwa kwa utaratibu mwingine mpaka wakae majiani?

Hata najiuliza hivi JK ataacha lini safari za ng'ambo kuombaomba. Hivi hawezi kuishi bila kuombaomba.
Juzi tu katangaza kua kwa mapenzi aliyonayo kwa waTZ, serikali yake ina mpango mkubwa wa kutokomeza malaria kwa kutumia vyandarua vya dawa, lakini bila aibu akamlizia kwa kusema 'viandarua atatoa Bush'.

Ombaomba hana haya, kaziuza zote pamoja na utu wake.
 
Muda sio muda yule dada aliye leta habari hii humu Jf,atasema Kikwete kamuotesha MANYOYA Bush pia,atasema alimwona Bush na alipotoka kuhijj Vatican Italy
 
Hizo zote kama serikali ni ombaomba kwanini watu wake wasiwe ombaomba?? hapa ndio kuna tatizo kubwa sana maana kuna kila sababu ya kuona jinsi ya kufanya kusaidia maeneo yao wanakotoka huko na kuboresha maisha yao

Enyi wa imani haba na kutupia kila shutuma kwa serikali! Mbona kila nchi duniani ina ombaomba? Marekani wamejaa ombaomba, Canada ombaomba ni wakuoga, Ulaya ndo usise? Je serikali za nchi hizi nazo ni ombaomba? Tunasafari ndeeeeeeefu sana kifikra!!
 
Dawa ya umaskini au dawa ya "watu kupotea katika mazingira ya ajabu"?

Kama ni kuhusu umaskini soma Kumbukumbu la Torati 15:11.

Sina biblia ya kiswahili hapa lakini kwa kiingereza Deuteronomy 15:11 - "There will always be poor people in the land. Therefore I command you to be openhanded toward your brothers and toward the poor and needy in your land."
Kwa tatizo la mtoto wa mtoa mada (Kiranja mkuu) Hayo mengine ni sawa kabisa maana Neno la Mungu ni kweli na amina.
 
Ukweli wale Omba omba huwa waanikwaza sana. huwa kila siku najiuliza inawa kweli hawana hata ndugu wa mbali ambao ana uwezo kidogo kuwasaidia? sisi wengine mbona tuna ndugu huko vijijini mbao wengine ni wazee sana na wengine hawajiwezi, tunajitahidi kuwasaidia? ukweli wanakera sana. Natamani sana siku niamke nisione hata ombaomba mmoja
Aisee
 
Back
Top Bottom