Uongo unaugharimu ubongo

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,648
Salaam wanaJF!

Wengi wetu huishi kwa kusema uwongo. Uwongo ndiyo chakula chetu kikuu. Uongo ndiyo taaluma yetu. Ukiingia kwenye siasa unafuzu na kuwa profesa wa uongo.

Dr Daniel Langleben wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania (limeandika gazeti la JamboLeo, Alhamisi Septemba 26, 2016)katika utafiti wake amegundua kwamba ubongo unalazimika kufanya kazi kubwa na kwa bidii zaidi unaposema uongo kuliko unaposema ukweli.

Dr Daniel, kwa kutumia mashine ya MRI (Magnetic Resonance Imaging)amegundua kwamba mtu anaposema uongo, ubongo unahitaji kuanza kazi ya uchakataji, kisha kwa kutumia silika (mazoea)msema uongo uanza kufikiria jibu la kweli kwanza kabla hajafikiria kusema uongo.

Anaongeza "katika ubongo huwezi kupata kitu cha bure. Mchakato wa kusema uongo ubongoni ni mgumu zaidi kuliko mchakato wa kusema ukweli, kiasi unasababisha matumizi nakubwa zaidi ya nyuroni (seli za neva)".

Huku kwetu tuna msemo "ukiwa mwongo, basi uwe na kumbukumbu ya kile ulichosema". Kitendo hicho hugharimu uwezo wa ubongo kiasi unashindwa kufanya mambo mengine ya msingi. Lakini kila unaposema ukweli huitaji kukumbuka chochote. Kwa maana hiyo MWONGO anaupa ubongo wake mzigo mkubwa.

TUISHI KWA KUSEMA UKWELI SIKU ZOTE ILI UBONGO USILAZIMIKE KUKUMBUKA UONGO TUNAO UTUNGA

Wikiendi njema nawatakia kwa kuambizana ukweli tu.
 
mtu anayesema uongo nampenda sana maana anatumia ubongo ipasavyo kitu ambacho walevi hawawezi
 
Kusema uongo ni lazima utumie akili, kwani inakubidi kila penye sentensi ya ukweli utoe neno moja la ukweli na uwwke neno moja la Uongo.

Hii itakufanya pindi unapodanganya basi uwe unafahamu na ukweli wake.

Huwa napenda sana kusikiliza uongo maana napata ukweli mwingine kuhusu uongo huo.
 
Fanya utafiti mdogo, kwa wale mabingwa wa uongo unaowajua, kama akili zao ziko sawasawa.
Japo ukweli humuweka mtu huru ila kuongopa utadhan ndio mtu hueleweka
Kwa.mfano ili kupata girls ..wanawake huwa wanaelewa uongo n.balaaaa

Basi wacha tuendelee kutumia ubongo wetu.si fresh fresh
 
mtu anayesema uongo nampenda sana maana anatumia ubongo ipasavyo kitu ambacho walevi hawawezi

Kusema uongo ni lazima utumie akili, kwani inakubidi kila penye sentensi ya ukweli utoe neno moja la ukweli na uwwke neno moja la Uongo.

Hii itakufanya pindi unapodanganya basi uwe unafahamu na ukweli wake.

Huwa napenda sana kusikiliza uongo maana napata ukweli mwingine kuhusu uongo huo.

Mawazo kinzana hayo! Lakini ukweli unabaki kwamba wasemao uongo wengi wao wayasemayo ni uongo na akili zao ni fyatu. Wanaposema uongo hawamwangalii mtu usoni. Hupepesa macho kana kwamba yameingiwa kitu!

Wakati wa kusema uongo, ni sehemu tatu kuu ya ubongo husisimuka. Sehemu ya mbele ya ubongo, ambayo mchango wake katika mchakato wa kazi ukandamiza ukweli. Mfumo wa fahamu hujiandaa kutokana na wasiwasi kwamba kinachotokea ni udanganyifu. Kujiandaa huko kwa fahamu, ni ukweli kwamba sehemu hiyo ubongo hujiandaa kwa sababu ni wajibu wake kutunza kwa ajili ya kurejesha kumbukumbu na kujenga picha ya akili.

Hivyo kusema uongo husavabisha ubongo kila mara kutunza uongo huo na kamwe msema uongo atasema ukweli. Tafiti zilizofanywa na wataalamu, zinaonesha kuwa 15% ya watu walikubali kuwa husema uongo katika sehemu zao za kazi. Kati ya hao, 59% huwa hawaoni aibu/hatia kuhusu hilo. Mmojawapo alisema "Mimi nilikuwa na kitu cha kufanya na uongo huo"!

Utamaduni wa kusema uongo hutegemea na kazi yako, kama vile: 94% ya wanasiasa ni waongo, kinyume na 27% kwa madaktari.

Nadhani 99% ya wanaJF ni waongo!
 
Kusema uongo ni lazima utumie akili, kwani inakubidi kila penye sentensi ya ukweli utoe neno moja la ukweli na uwwke neno moja la Uongo.

Hii itakufanya pindi unapodanganya basi uwe unafahamu na ukweli wake.

Huwa napenda sana kusikiliza uongo maana napata ukweli mwingine kuhusu uongo huo.

Kama utafiti ulivyobainisha, kabla ya kusema uongo unaanza na ukweli, kisha unatafuta jibu la uongo. Km una shida ya hela na njia pekee ni kukopa. Kabla ya kukopa unajiuliza utakayemkopa unamwingiaje! Unajiuliza hivyo kwa kuwa unamujua vilivyo. Hivyo, baada ya kujua ukweli huo, unatunga uongo wako.

Lakini kumbuka kwamba unapotunga uongo, ubongo wako unaweka kumbuku ili usisahau. Kitendo hicho cha ubongo kinaulazimisha kufisha uwezo wake wa kuweka yaliyo ya kweli. Mwisho unaishia kuwa mwongo daima.

Hakuna mtu mbaya kama mwongo maana ni mbea, mnafiki, mchonganishi na tabia za aina hiyo.

OGOPA MTU MWONGO KAMA UKOMA
 
Salaam wanaJF!

Wengi wetu huishi kwa kusema uwongo. Uwongo ndiyo chakula chetu kikuu. Uongo ndiyo taaluma yetu. Ukiingia kwenye siasa unafuzu na kuwa profesa wa uongo.

Dr Daniel Langleben wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania (limeandika gazeti la JamboLeo, Alhamisi Septemba 26, 2016)katika utafiti wake amegundua kwamba ubongo unalazimika kufanya kazi kubwa na kwa bidii zaidi unaposema uongo kuliko unaposema ukweli.

Dr Daniel, kwa kutumia mashine ya MRI (Magnetic Resonance Imaging)amegundua kwamba mtu anaposema uongo, ubongo unahitaji kuanza kazi ya uchakataji, kisha kwa kutumia silika (mazoea)msema uongo uanza kufikiria jibu la kweli kwanza kabla hajafikiria kusema uongo.

Anaongeza "katika ubongo huwezi kupata kitu cha bure. Mchakato wa kusema uongo ubongoni ni mgumu zaidi kuliko mchakato wa kusema ukweli, kiasi unasababisha matumizi nakubwa zaidi ya nyuroni (seli za neva)".

Huku kwetu tuna msemo "ukiwa mwongo, basi uwe na kumbukumbu ya kile ulichosema". Kitendo hicho hugharimu uwezo wa ubongo kiasi unashindwa kufanya mambo mengine ya msingi. Lakini kila unaposema ukweli huitaji kukumbuka chochote. Kwa maana hiyo MWONGO anaupa ubongo wake mzigo mkubwa.

TUISHI KWA KUSEMA UKWELI SIKU ZOTE ILI UBONGO USILAZIMIKE KUKUMBUKA UONGO TUNAO UTUNGA

Wikiendi njema nawatakia kwa kuambizana ukweli tu.
kweli asee
 
Hata ID yako Mwanapropaganda maana yake ni Mwanauongo, Proganda ni Uongo unaotengenezwa kuwa Ukweli.

Umetisha Mkuu,Mwanga Lutila.

Hata kutumia Username ambayo siyo majina yetu ni uongo wa KUOGOPWA KAMA UKOMA.Mtu una jina zuuri tu lakini unaona hakufai kulitumia humu,Kwanini uandike Mara Lizaboni,Kisu cha Ngariba,Nyani Ngabu,Fundi chupi,Bajeti ya Kunguru nk??

Dhambi kubwa inayoongoza kwa sasa ulimwenguni ni UONGO.Tumekuwa watumwa wa dhambi hii na wengi tutaenda motoni kwa ajili ya uongo.

SAY NO TO "UONGO".
 
Eti mleta mada anaitwa mwengeso! Ndo nn!? Acha uongo ww"
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom