Uoga wenu wa nini?

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Nina amini kuwa, members wote wa Jf ni wasomi, na labda mwenye kiwango cha chini kabisa atakuwa kidato cha 4. Tumekuwa tukifundishwa na hata kufundisha kuwa "no research, no right to publicize/speak". Watu wa social science wanaamini ktk research, na hata wa natural science wanaamini ktk research kama njia pekee ya kupata ukweli. Serikali yetu na taasisi za umma na binafsi, vimekuwa vikitueleza kuwa katika Tanzania, wakristo ni wengi zaidi kuliko waislam. Na muda wote huo waislam wamekuwa wakipinga kwa madai kuwa hakuna utafiti uliofanyika kujua idadi ya watu. Website ya wizara ya maliasili ilikuwa inaonesha kuwa wakristo ni 45%, waislam ni 30% na dini nyinginezo 25%. Kitabu cha fact find kinaonesha wakristo ni 35%, waislam ni 30% na dini nyingine ni 35%. Sensa imefika, waislam wanataka kipengele cha dini kiwemo ili kupata taarifa rasmi na za kweli, badala ya hisia tu. Serikali na mawakala wao wanapinga. Wanaogopa nin? Hesabuni, ijulikane. Muongo na mkweli wabainike. Vinginevyo, nauliza: mnaogopa nini?
 
Back
Top Bottom