UOA yamtimua mhadhiri mwanasiasa

Teh Teh Teh

Member
Nov 13, 2009
41
9
Viongozi wa Chadema bado waendelea kushughulikiwa. Ya Baregu. Dr. Kitila naye yupo njiani kutimuliwa UDSM kwa kujihusisha na harakati za chadema.

na Grace Macha, Arusha.

CHUO Kikuu cha Arusha (UOA) kimekusudia kutompatia ajira ya kudumu mhadhiri wake wa lugha na taaluma ya maendeleo, Dadi Igogo, ya kuendelea kufundisha chuoni hapo kwa madai kuwa amekuwa akijihusha na siasa.

Makamu mkuu wa chuo hicho Dk. Torres aliliambia Tanzania Daima kwa njia ya simu juzi kuwa tayari ameshamtaarifu mhadhiri huyo kuwa baada ya kumalizika kwa muhula huu wa masomo katikati ya mwezi Machi mwaka huu hawatamhitaji tena hivyo watampatia mishahara yake ya miezi mitatu kama sheria za kazi zinavyotaka.

Alisema kuwa Igogo amekuwa akihamasisha wanachuo kufanya vurugu ambapo hivi karibuni wanachuo wa mwaka wa kwanza waligoma wakidai kupatiwa fedha za kujikimu zinazotolewa na bodi ya mikopo nchini ambazo walicheleweshewa kupatiwa.

Alisema kuwa sababu nyingine ya kuamua kutomuajiri ni kuwa hakidhi vigezo vya kufundisha vyuo vikuu vilivyowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) hata hivyo alishindwa kufafanua ilikuwaje akampa ajira ya muda tokea mwezi Novemba mwaka jana wakati akijua hakidhi vigezo.

Dk. Torres alisema Igogo alikuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la CHADEMA lililofunguliwa mwanzoni mwa wiki hii na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho , Freeman Mbowe, jambo alilosema kuwa linathibitisha kuwa ni kweli anajihusisha na siasa wakati wa masomo.

Kwa upande wake Igogo alisema kuwa ni kweli amepatiwa taarifa za mdomo na makamu mkuu wa chuo Alhamisi ya wiki iliyopita kuwa hawatampatia ajira ya kudumu kwa kuwa anajihusisha na siasa ndani ya eneo la chuo ingawa mpaka sasa hawajampatia barua rasmi ya kumueleza hilo.

Mhadhiri huyo alisema kuwa alimweleza makamu mkuu wa chuo kuwa taarifa hizo si kweli hivyo akamshauri suala hilo lipelekwe kwenye kamati ya nidhamu itakayochunguza suala hilo na kupata ukweli kama anatumia madarasa kueneza siasa za CHADEMA jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Hata hivyo alielezea kushangazwa na taarifa hizo zilizotolewa na makamu mkuu huyo wa chuo kwa kile alichosema kuwa hajawahi kujihusisha na siasa akiwa ndani ya maeneo ya chuo kwani anaelewa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kusisitiza yeye ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na si kiongozi.

Igogo alisisitiza kuwa sheria hiyo inawanyima watumishi wa umma kujihusisha na siasa lakini chuo hicho si cha umma bali ni cha kanisa la Sabato (SDA) hivyo ana haki ya kujihusisha na siasa akiwa nje ya mazingira ya chuo.

Hata hivyo alisema kuwa inashangaza kwa yeye kuhukumiwa kwa kipengele hicho ambapo alidai anawafahamu wahadhiri wengine ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wanaendelea kufundisha chuoni hapo huku mmoja akiwa ni mthamini wa tawi la CCM la wanachuo lililoko karibu kabisa na lango kuu la kuingia UOA lakini haguswi.

Alisema kuwa suala la kutokidhi vigezo vya elimu nalo halina ukweli kwa kile alichodai kuwa kwenye masomo yake ya shahada ya uzamili alipata wastani wa alama (GPA) 4.0 ambazo zimevuka kiwango kilichowekwa na TCU ambacho kinataka uwe na wastani wa alama kuanzia 3.5.

Hata hivyo alisema kuwa suala hilo linaonekana kupata msukumo kutoka nje ya uongozi wa chuo kwa kile alichosema kuwa Ijumaa ya wiki iliyopita aliitwa na mkuu wa polisi wilayani Arumeru ambaye hakumtaja kwa jina ambapo alihojiwa kwenye kituo hicho kwa zaidi ya saa nne kuwa ana mpango wa kuendesha mgomo wa wanafunzi ingawa baadaye aliachiwa huru.

Tukio hilo linakuja ikiwa imepita takriban mwaka mmoja tokea serikali ikatae kumuongezea mkataba aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Saalam, Profesa Mwesiga Baregu, kwa madai ya kuegemea zaidi kwenye siasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema kuwa kwa mujibu wa waraka wa mkuu wa utumishi namba moja wa mwaka 2000, maelekezo kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi na unaelekeza mambo yanayoruhusiwa na yale yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma.

Alitaja miongoni mwa mambo yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma kuwa ni kugombea nafasi yoyote chini ya katiba au uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa akiwa mtumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema kitendo hicho cha Profesa Baregu kugombea na kushikilia nyadhifa kadhaa ndani ya CHADEMA kilimsababishia akose sifa ya kuendelea kuwa mtumishi wa umma.

Hata hivyo Chuo Kikuu cha Mt Agustine (SAUT) walimwajiri Profesa Baregu muda mfupi baada ya kumaliza mkataba wake UDSM na anaendelea kufundisha mpaka sasa.
 
nguvu ya umma itawafundisha adabu hawa viongozi wa vyuo wasioijua tanzania ya kesho yenye asali tamu!!! siku zimekaribia watajutia maamuzi waliyoyatoa!!!!!!!!
 
Hawa viongozi wanafikiri wanaifurahisha si si em lakini wanatengeneza maisha mabaya mbele yao.......
 
tunajua mkuu wa chuo uoa dk.tores ni personal friend wa jk na baadhi ya vigogo wa ccm so hatushangai ndo maana last year kuna test ziliahirishwa coz kuna baadhi ya madent hawakuwepo walikuwa kwenye mkutano wa ccm afu huyo mmarekani mkuu wa chuo ana jazba mbaya
 
Mshaanza tena, hata kama mtu anakosea ndiyo hatuwa zisichukuliwe?
 
Mchukulieni pia hatua Dr. Benson Banna wa UDSM. Au yeye ni untouchable kwasababu yuko CCM?
Banna ni mshauri wa uchumi wa mwenyekiti wa CCM
 
Viongozi wa Chadema bado waendelea kushughulikiwa. Ya Baregu. Dr. Kitila naye yupo njiani kutimuliwa UDSM kwa kujihusisha na harakati za chadema.

na Grace Macha, Arusha.

CHUO Kikuu cha Arusha (UOA) kimekusudia kutompatia ajira ya kudumu mhadhiri wake wa lugha na taaluma ya maendeleo, Dadi Igogo, ya kuendelea kufundisha chuoni hapo kwa madai kuwa amekuwa akijihusha na siasa.

Makamu mkuu wa chuo hicho Dk. Torres aliliambia Tanzania Daima kwa njia ya simu juzi kuwa tayari ameshamtaarifu mhadhiri huyo kuwa baada ya kumalizika kwa muhula huu wa masomo katikati ya mwezi Machi mwaka huu hawatamhitaji tena hivyo watampatia mishahara yake ya miezi mitatu kama sheria za kazi zinavyotaka.

Alisema kuwa Igogo amekuwa akihamasisha wanachuo kufanya vurugu ambapo hivi karibuni wanachuo wa mwaka wa kwanza waligoma wakidai kupatiwa fedha za kujikimu zinazotolewa na bodi ya mikopo nchini ambazo walicheleweshewa kupatiwa.

Alisema kuwa sababu nyingine ya kuamua kutomuajiri ni kuwa hakidhi vigezo vya kufundisha vyuo vikuu vilivyowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) hata hivyo alishindwa kufafanua ilikuwaje akampa ajira ya muda tokea mwezi Novemba mwaka jana wakati akijua hakidhi vigezo.

Dk. Torres alisema Igogo alikuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la CHADEMA lililofunguliwa mwanzoni mwa wiki hii na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho , Freeman Mbowe, jambo alilosema kuwa linathibitisha kuwa ni kweli anajihusisha na siasa wakati wa masomo.

Kwa upande wake Igogo alisema kuwa ni kweli amepatiwa taarifa za mdomo na makamu mkuu wa chuo Alhamisi ya wiki iliyopita kuwa hawatampatia ajira ya kudumu kwa kuwa anajihusisha na siasa ndani ya eneo la chuo ingawa mpaka sasa hawajampatia barua rasmi ya kumueleza hilo.

Mhadhiri huyo alisema kuwa alimweleza makamu mkuu wa chuo kuwa taarifa hizo si kweli hivyo akamshauri suala hilo lipelekwe kwenye kamati ya nidhamu itakayochunguza suala hilo na kupata ukweli kama anatumia madarasa kueneza siasa za CHADEMA jambo ambalo mpaka sasa halijafanyika.

Hata hivyo alielezea kushangazwa na taarifa hizo zilizotolewa na makamu mkuu huyo wa chuo kwa kile alichosema kuwa hajawahi kujihusisha na siasa akiwa ndani ya maeneo ya chuo kwani anaelewa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kusisitiza yeye ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na si kiongozi.

Igogo alisisitiza kuwa sheria hiyo inawanyima watumishi wa umma kujihusisha na siasa lakini chuo hicho si cha umma bali ni cha kanisa la Sabato (SDA) hivyo ana haki ya kujihusisha na siasa akiwa nje ya mazingira ya chuo.

Hata hivyo alisema kuwa inashangaza kwa yeye kuhukumiwa kwa kipengele hicho ambapo alidai anawafahamu wahadhiri wengine ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wanaendelea kufundisha chuoni hapo huku mmoja akiwa ni mthamini wa tawi la CCM la wanachuo lililoko karibu kabisa na lango kuu la kuingia UOA lakini haguswi.

Alisema kuwa suala la kutokidhi vigezo vya elimu nalo halina ukweli kwa kile alichodai kuwa kwenye masomo yake ya shahada ya uzamili alipata wastani wa alama (GPA) 4.0 ambazo zimevuka kiwango kilichowekwa na TCU ambacho kinataka uwe na wastani wa alama kuanzia 3.5.

Hata hivyo alisema kuwa suala hilo linaonekana kupata msukumo kutoka nje ya uongozi wa chuo kwa kile alichosema kuwa Ijumaa ya wiki iliyopita aliitwa na mkuu wa polisi wilayani Arumeru ambaye hakumtaja kwa jina ambapo alihojiwa kwenye kituo hicho kwa zaidi ya saa nne kuwa ana mpango wa kuendesha mgomo wa wanafunzi ingawa baadaye aliachiwa huru.

Tukio hilo linakuja ikiwa imepita takriban mwaka mmoja tokea serikali ikatae kumuongezea mkataba aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Saalam, Profesa Mwesiga Baregu, kwa madai ya kuegemea zaidi kwenye siasa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema kuwa kwa mujibu wa waraka wa mkuu wa utumishi namba moja wa mwaka 2000, maelekezo kuhusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi na unaelekeza mambo yanayoruhusiwa na yale yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma.

Alitaja miongoni mwa mambo yasiyoruhusiwa kwa watumishi wa umma kuwa ni kugombea nafasi yoyote chini ya katiba au uongozi wa ngazi yoyote katika chama cha siasa akiwa mtumishi wa umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, alisema kitendo hicho cha Profesa Baregu kugombea na kushikilia nyadhifa kadhaa ndani ya CHADEMA kilimsababishia akose sifa ya kuendelea kuwa mtumishi wa umma.

Hata hivyo Chuo Kikuu cha Mt Agustine (SAUT) walimwajiri Profesa Baregu muda mfupi baada ya kumaliza mkataba wake UDSM na anaendelea kufundisha mpaka sasa.

CHUO KIKUU cha Ausha ndio Chuo gani? au unatak kupandisha chati wau tuu bila sabbu?
 
Hawa viongozi wanafikiri wanaifurahisha si si em lakini wanatengeneza maisha mabaya mbele yao.......

hawa wasanii wa chadema watawaponza watu wengi mambumbumbu! wenyewe wanakula good time bungeni wao wanaendelea kuhangaika tuu! ama kweli wajinga ndio waliwao!
 
CHUO KIKUU cha Ausha ndio Chuo gani? au unatak kupandisha chati wau tuu bila sabbu?

mkuu kipo kiliwakilisha vizuri sana mashindano ya zain challenge mwaka juzi,back to the topic huyu mhadhiri anafukuzwa kwa sababu kajihusisha na siasa au kwa sababu hakidhi viwango?
 
Dady Igogo ni classmate wangu pale UDSM.Ni mtuwa misimamo Mukandala anamfahamu sana. Mara baada ya kuhitimu Bachelor yake aliajiriwa na CDM kama Afisa Mafunzo. Baadaye alijiunga na M.A Programme pale UD then akaajiriwa hapo UOA. Ni ajabu sana kwa jinsi nilivyososma hiyo habari kwa sababu wanaobanwa ni viongozi/ wanachama wa upinzani tu.Sheria iko wazi mtumishi wa umma anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama chochote ila asifanye siasa wakati wa kazi. Anyway imeniumiza sana
 
Mshaanza tena, hata kama mtu anakosea ndiyo hatuwa zisichukuliwe?

Ni hatari sana,tunahitaji uhuru wa kweli,ni watumishi wangapi wa serikali wanagombea madara ndani ya CCM na haachishwi kazi,hatua zichukuliwe kwa wote sio tu wale wanao kwenda upinzani ndio wamekosa,Lazima tuwe na uhuru wa kweli katika maamuzi ya maisha yetu nikiamua kufanya chochote katika nyanja ya siasa nifanye ka fikra zangu zinavyo nituma sio kubagua wa CCM wengi tunawajua na isiwe kwenye Elimu pia,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na mashirika ya umma zote hizo ni sehemu za utumishi wa umma,isitoshe huyu jamaa yupo sekta binafsi kwa nini ?CCM inatapatapa sasa wanaamrisha dola kufinyanga haki za watanzania popote wanako kwenda,hii si haki,waache mara moja.hata Prof.Baregu wanatamani kumfuata huko aliko lakini taasisi yenyewe wanaiogopa.
 
Back
Top Bottom