Fadhili Paulo
JF-Expert Member
- Sep 1, 2011
- 3,211
- 988
Kila mara ni mpya bali ujumbe wake ni mmoja kila wakati - maji.we paulo mbona kila siku unaileta ikiwa mpya wakati ni ileile au nakosea.
Kila mara ni mpya bali ujumbe wake ni mmoja kila wakati - maji.we paulo mbona kila siku unaileta ikiwa mpya wakati ni ileile au nakosea.
kila mara ni mpya bali ujumbe wake ni mmoja kila wakati - maji.
maji ni uhai hakika.
je mtu ukiwa unakunywa zaidi ya lita 3 kwa siki ni kosa?
mimi huwa napata bia 3 kila siku jioni. asubuhi huwa naanza na lita 2 za maji ya vuguvugu baada ya kutoka jogging, then nikiwa ofisini ni mwendo wa lita 2-3 tena mpaka saa kumi.
Ni kweli mkuu maji ya vuguvugu ni therapy tosha sababu ya kwanza huongeza mzunguko wa damu na kufanya oxygen kusambaa kwenye kila tissue ya mwili vizuri na kufanya kuwa na afya na nguvu. Pili maji ya uvuguvugu husambaza na kuzuia mkusanyiko wa mafuta kwenye damu ambayo yanaweza kusababisha ateriosclerosis ambayo inaweza kuresult kwenye ischemia, myocardial infarction ,heart attack kwa hiyo hot water ni muhimu . Tatu husaidia kupunguza sumu kwenye damu na kuzui magonjwa ya ini na figo
Faida gani hasa zinazopatikana?Hata kama utakunywa hayo maji ya Uvuguvugu glasi moja huku ukichanganya kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali Asali itakuwa vizuri zaidi hayo maji ya Uvuguvugu na asali mbichi ya nyuki ni dawa ya kila maradhi ikiwa utazoea kila siku unapo amka Asubuhi kabla ya kula kitu mdomoni ukanywa hayo maji yaliyochanganywa na Asali utapata faida kubwa katika kulinda afya yako.
ahahahaha...hapa mmekuja anga zangu..yani nakunywa mimaji mpaka watu wananiogopa...si nimeamua kusitisha kwa muda uhusiano wangu na hawa wahindi wa sbl..sasa nikaamia kwa mzee mengi na kitu ya kilimanjaro kubwa...kwa kiwango cha chini..everyday ni maji 1.5ltrs chupa 4...kiasi ya lita 6 kila siku inayogonga kwa mungu...siku naamua kukaa na wananchi baa...ni mwendo wa kila raundi na mie yangu ya maji..mpaka kieleweke...ishu inakuja kuwa sijisikii hamu ya kullaaaa..yani mie nagusa menu kidogo tu nimeshiba...nadhani inabidi kuanza kuvuna pia faida za mazoezi ya viungo
Nimejiskia furaha sana mkuu, siku yeyote mtu akiulizia lolote kuhusiana na maajabu ya maji katika kukinga na kutibu magonjwa, mwambie afunguwe www.maajabuyamaji.net ili kujua namna ya kunywa na kuyatumia maji kama dawa bonyeza hapa: jitibu kwa kutumia maji | maajabu ya majiMkuu kila kitu kina ukomo wake. Kunywa maji mengi kupita kiasi pia siyo nzuri,niliwahi kusoma thread ya member mmoja humu JF (somebody Fadhili kama sikukosea),hapa hapa JF doctor kuwa kiasi cha maji unachokunywa kwa siku kina uhusiano na uzito wako ( unfortunately sikumbuki ile formula) ila kinatakiwa kisizidi 3litres/day na/au 1 litre at a time kinyume na hapo utakuwa unasababisha kutoka kwa minerals mwilini wakati utakpolazimika kukojoa too often.Jaribu kutafuta ile thread ina elimu nzuri sana kuhusu matumizi ya maji.
Mkuu BAK Umoto wa Maji ya kunywa unatakiwa uwe sawasawa na umoto wa chai au Maji ya Uvuguvugu pia inatosha. Hata kama huna MaradhiSasa Mkuu MziziMkavu moto wa hayo maji ya kunywa inabidi uwe kama wa chai au uvuguvugu tu unatosha? Wachina nasikia ndio zao hizi za kunywa maji ya moto lakini kuhamia kwenye nchi za magharibi kumewafanya wengi wao waachane na utamaduni wao huu, kama tunaweza kuita ni utamaduni.