Unywaji pombe kali unaweza ukufanye ushindwe kupumua

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,772
Ningependa kuwaeleza juu ya experience yangu binafsi, hasa katika kipindi hiki ambacho kuna utata juu ya kifo cha kanumba. Ukweli ni kwamba katika mazingira fulani, unywaji wa pombe kali unaweza ukasababisha ukashindwa kupumua (suffocation). Na hali hii ni hatari hata zaidi unapokuwa kwenye mazingira ya hewa nyepesi, na zaidi ndani ya ndege inayosafiri.

Ilinichukua muda mrefu kugundua kwamba nyakati fulani taabu kubwa ya kupumua iliyokuwa ikinipata ilitokana na kunywa pombe hasa kali, na mara nyingi ilitokea si kwa sababu nilikunywa sana bali hata kiasi kidogo. Ukinywa sana ni mbaya hata zaidi. Si watu wote wanapata tatizo hili, na linaweza likakuanza wakati wowote. Huko nyuma sikuwa na hili tatizo.
 
Jack Daniels?
 
Back
Top Bottom