Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
Bangusilo ndio nini? Nimesahau kidogo....
Hii si aliitoa mhashimiwa Msabaha akimaanisha mbuzi wa kafara kwa kizaramo!
Bangusilo ndio nini? Nimesahau kidogo....
Kama kuna neno ambalo leo tunaliogopa kuligusa ni neno "unyonyaji". Kimsingi neno hili lilitokana na dhana ya jinsi kupe anavyoishi kwa kunyonya "host" wake kama ng'ombe, mbwa n.k Kwa maneno mengine mnyonyaji ni mtu ambaye anatumia kila mbinu kujitajirisha kwa kutumia "migongo" ya wengine.
Mwanzoni mwa jamhuri yetu wanyonyaji tuliwaimba na kuweka misemo kama "usiwe mnyonyaji kama kupe" tukiwahimiza watu wafanya kazi au wale kutokana na jasho lao. Tukasema kuwa watu pekee ambao wanastahili kuishi kwa jasho la watu wengine ni watoto, wagonjwa, na wazee ambao wameshachumia juani. Tukawakatalia watu wengine wote ambao wanataka kuishi "kwa njia za mkato".
Hata hivyo baada ya mabadiliko ya kiuchumi yaliyotokea tabaka la wanyonyaji limeanza kujitokeza kwa kiasi kikubwa ambapo kuna watu ambao pasipo kufanya kazi (biashara au kuchakarika kihalali) wanatumia nafasi zao na vyeo vyao kutengeneza fedha ya haraka haraka.
Ni hapo ndipo tumeanza kuona kundi la watu tuwaitao "mafisadi". Wakati neno fisadi linatumika kuelezea kila aina ya uovu katika utumishi wa umma (rushwa, wizi, ubadhirifu, matumizi mabaya ya cheo, ofisi au jina n.k) neno "mnyonyaji" lilikuwa linatumika kuelezea mtu ambaye kimsingi anavuna asichopanda na anameza asichotafuna.
Mnyonyaji ni mtu ambaye hana wasiwasi wa maisha yake kwa sababu ametegesha mirija yake kwenye mabenki, ofisi, n.k ambapo hata akiwa katika ziara ya Rais au akikaa kwenye kiti chake cha ngozi nyeusi mirija hiyo inaendelea kufyonza kama ina kichaa. Mnyonyaji haitaji kufanya kazi yoyote isipokuwa kuweka mrija huo mdomoni na kama mtu anayefyonza ulanzi au mzee aliyekalia kibuyu cha chimpumu au yule anayepulizia mbege basi anajinoma taratibu huku mashavu yake yakitanuka kama chura apigaye mluzi!
Tunachoona sasa hivi ni kuwa wanyonyaji ambao tuliwakatia mirija mwaka 1967 ili angalau na wengine tuweze kunenepa ndio wamerudi kwa ari na nguvu mpya na sasa hivi wananyonya huku wameinua miguu juu kwani wanajua hawanyonyi peke yao. Wakati umefika wa kuchora katuni ya "wanyonyaji mambo leo" ambao wamemzunguka Mtanzania na mirija yao mdomo wakimfyonza kama vile mbu anavyonya damu kama anatumia drill ya kufyonza mafuta!
Wanyonyaji hawa weusi, leo wanasimama wakijua kuwa wanalindwa na hakuna mwenye ujasiri wa kuifyeka mirija yao na kuwakatisha uhondo wao huo. Cha kuudhi ni kuwa sisi Watanzania ndio tumekaa pembeni na kupiga kelele lakini ni kelele za kushangaa siyo kukasirika na kutaka kuikata mirija hiyo. Ndio maana hadi leo hii tunaendelea kuwalipa dowans, Mkapa ameendelea kushika mrija wa Kiwira, na wengine wameshikilia mirija yao huku baadhi yao wakishikilia mirija kwenye kila kidole huku wakicheka cheka na kucheua mafuta yanukayo!
Kinachoendelea si ubepari jinsi unavyoeleweka Magharibi ambapo unajitahidi kuonesha angalau huruma kwa wanyonywaji; wa kwetu ni unyonyaji unaojifanya ni ubepari! Ni nani atakayethubutu kukata mirija hii na kuwakatisha wanyonyaji hawa uhondo wao! Ni nani ambaye yeye mwenyewe si mnyonyaji atakayeona uchungu wa kile kinachoendelea?
Je, mfanyabiashara na mwekezaji anaweza kufanya biashara yake vizuri na akapata faida bila kuwa mnyonyaji wa kutupwa. Je tunaweza kuwaacha watunyonye ilimradi wanatulisha na tunanenepa kidogo kuliko wakitunyonya tukiwa kimbaumbau!? Tufanye nini ili tuwanyang'anye mirija hiyo au tufanye nini ili tuweke machujio kwenye mirija hiyo ili wanapofyonza basi wasivyonze vyote!?
Au tukubali tu kuwa wanyonyaji wana haki ya kutunyonya kwa sababu tumeweka wenyewe migongo yetu wazi ili watunyonye huku tumeipakaa mafuta ili kuitamanisha? Je tuwaache watunyonye kwa sababu wanaweza na jaribio lolote la kutishia kukata mirija hiyo litakutana na upinzani kuwa tunataka kurudia "utaifishaji" na tunataka kutishia wawekezaji?
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu Unyonyaji sasa hivi ni RUKSA!.. kwa tafisri fupi Unyonyaji lazima uwe na mirija ya kufyonzea uchumi wa nchi kama vile kunguni ama imani ya Mumiani (vimpare) wanavyonyoinya damu za watu pale unapoamua kufumba macho..
Kulingana na mfumo mzima wa Ubepari mirija ni lazima iwepo na process nzima haitegemei pakacha kujazwa isipokuwa kuwepo kwa njia mbili za kuingiza na kutoa..Hivyo balance ya malipo yake inategemea zaidi bomba kubwa linalojaza.
Mkuu, kama hutaki kunyonywa basi usilale wala kutembea kizani maanake vitanda vyote vimejaa kunguni hata Benki zetu zinaendeshwa kwa na damu yako, isikuzuie kulala hata kidogo utakuja zoea.
Ufisadi on the other hand ni Uharibifu kama vile nguchiro na nzige wanavyoweza haribu mazao, hawa wanafuata the base ya uzalishaji na kuharibu taratibu zote za kupata mazao bora ama kuharibu pato la mavuno. Hawa pia inaonyesha wanaanza kuhalalishwa kwa sababu huyo nguchiro ni pet wetu wenyewe ndani ya nyumba...
Mkuu Bob,Rev. Kishoka,
Sina la kuongeza mkuu umemaliza darasa!duh ukiamua wewe mchafu sana ktk maswala haya..
Mkuu Bob,
Watanzania tulikimbilia kuimba wimbo wa kupiga vita Unyonyaji na hivyo kuua kabisa matumaini ya kuwepo mfumo wa Kibepari maana tuliambiwa ubepari ni Unyama.
Yes ubepari una unyama, na hata Ujamaa, lakini hukumu ya kuwa Ubepari ni Unyonyaji ilikuwa ni upotofu.
Hawa kina Chenge na Mafisadi wao si Mabepari! Wao ni Wahujumu Wanyonyaji, Mijizi!