Unyanyaswaji wa watoto Tanzania wabainika

The Emils

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
568
124
Ripoti ya kunyanyaswa watoto Tanzania 10 Agosti 2011 13:10 Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika linaloshughulikia maslahi ya watoto la UNICEF karibu theluthi moja ya watoto wa kike nchini Tanzania wanakabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa bila hiari kabla hawajatimia umri wa miaka 18. Shirika hilo linasema kuwa watoto wa kiume idadi yao inafika asili mia 13.4.

Kinachotumika sana katika unyanyasaji huu ni kuwatomasa watoto ambako baadae hufuatiwa na jaribio lakutaka kuwaingilia. Afisa mmoja wa shirika hilo Andy Brooks amesema uchunguzi huu ndio uliokamilika zaidi na umeonesha kuwa serikali iko tayari kukabiliana na tatizo hili. Uchunguzi huu pia uligundua kuwa wale ambao wamejihusisha na mapenzi kabla ya kutimia umri wa miaka 18, asili mia 29.1 ya watoto wa kike na asili mia 17.5 ya wale wa kiume wamesema kuwa mara ya kwanza wao kujihusisha na ngono haikuwa kwa hiari yao.

Unicef inasema hii ina maana walilazimishwa ama kushawishiwa kujihusisha na ngono. Waziri wa Elimu wa Tanzania Shukuru Kawambwa amesema kuwa serikali imejitolea kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na kuingiliwa watoto. Bw Brooks amesema uchunguzi sawa na huo utafanywa nchini Kenya, Rwanda, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kusini..

source:BBC SWAHILI

 
Hakuna hata mtu mmoja aliyechhangia hii topic jamani hivi wanajamii mna uelewa wa namna gani ndugu zangu, hii ni issue nzito sana lkn hakuna hata mchango wa watu.

Watoto wananyanyasika sana kwa vile uelewa wetu ni wa wastani ila tujjue sasa hivi watoto wetu wanafuraha tupo nao think about tommorow umekufa dunia itawanyanyasa na kuwa abuse watoto wako. Iwe changamoto tujali watoto wote bila kuangalia kuwa ni wako au la!. . . Kukua bila wazazi ni ngumu sana.
 
Waziri Sophia Simba kama sikosei ndiye aliyepewa dhamana ya kuangalia maswala ya watoto. Lakini cha ajabu sijamsikia huyu waziri akisema lolote la maana kuhusu welfare ya watoto wa nchi hii. Kila siku tunasikia kwenye vyombo vya habari watoto waliobakwa lakini yeye kama hayupo.

Sina hakika kama bajeti ya huyu mwanamama imeshapita, lakini kama haijapita nadhani wabunge wambane maana hana cha maana anachofanya.
 
sofia simba yupo bize na mambo mengine bwana hawezi kukaa na kuwaza watoto wa kiswahili yeye anafikiria ni jinsi gani ataiba raslimali ya umma...
 
Watoto wengi wanaishi katika mazingira magumu na hakuna mpango thabiti ya kuwaondoa huko
 
Back
Top Bottom