Unyanyapaa wa Chadema

Chadema inaonekana kuwa makini sana pale bungeni na hata kwenye mahojiano na vyombo vya habari na wamekuwa hawasikii ,wakiambiwa wakielekezwa wanakuwa na misimamo isiyoambilika.Wanajiona wao ni wao hizi ni kasumba za Mwalimu Nyerere kiasi kufika kuitwa baba haambiliki ,jina ambalo alilichukia sana.

Safu hii ya Chadema iwapo watafanikiwa kuongoza dola hii,(Inshaallah wafanikiwe) tumeichoka CCM,kuna uwezekano kuiendesha au kuiongoza Tanzania kama itakuwepo kwa kutumia utawala wa kidikteta ni kushinda CCM ,bila ya shaka kutaiweka nchi katika woga na uhuru wa mwananchi utakuwa finyu.

Sioni busara yeyote ile wanayoitumia pale bungeni ,sioni hekima yeyote ile wanayoitumia katika lugha dhidi ya vyombo vya dola ,hivi wanataka kutuambia watakapo ingia katika duru ya kuiongoza Tz watavunja vyombo hivi wanavyovidharau na kuona haviwatendei haki.

Unyanyapaa huu wa kuvikomalia vyombo vya dola na kuvibeza ni jambo linalotia hofu sana.

Unayejiita MWIBA! Salam ama baada ya salam sisi huku hatujambo hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa mach yetu.

Nimepitia comment za watu wengi ambao unataka wa comment kama unavyotaka na baada ya wewe pia kuzipitia comment hizo umediliki kusema kuwa "KAMA UNGEKUWA MOD UNGEWAKATA VIDOLE NA KUWATOBOA MACHO" wachangiaji wote.

MY TAKE: Wewe ni mmojawapo wa waliomteka Dr. Ulimboka na kumfanyia kama unavyotuthibitishia humu JF. Na ole wako tusikie katekwa mwingine tunaanza na wewe.
 
Mwiba, busara za CCM unaziona? Kuwafokea wabunge wenzao, kaa chini! Toka nje? Mwone alivyo kituko?
 
Last edited by a moderator:
Kidogo umenisifia hapo hapo ukanigonga kirungu.
Mimi ni mfuasi wa Jf kwa muda sasa na kuna wakati natamani kujitoa kwani inaelekea kuna baadhi ya watu kwa maksudi wanalishushia hadhi jamvi letu.
Naamini ya kuwa mtu anayepost kitu hapa angalau ana uelewa wa computer na pia ana access na internet na kwa nchi yetu idadi hiyo ni ndogo hivyo basi washiriki ni class kidogo tofauti na most of the people.
Inasikitisha kuona watu wanavyomwaga ***** humu.
Tuvumilie nahisi ni transition na mwisho tutapata cream ya wachangiaji.

huwezi amini burn aliomba muongozo wa spika na akaomba shughuli za bunge zisitishwe ili kujadili kifo cha mwenye kiti waccm! Unajua kilichotokea?
Tulianza kusikia mwongozo spika,mwongozo spika,mwongozo spika. Sijui nini kiliendea tena ana ye kumbuka atukumbushe.
 
great makina xana mwandishi ya2pasa wote kufikiri kwa makini co kushabikia c a sa,2nadumazwa fikra na wa2 wachache.2nakataa u2mwa wa fikra wa wa2 wa nje ndani 2nakubali 2ondoe dhana ya kwamba cc na wafinyu ktk fikra!

Sijaambulia kitu!
 
Siku zote hesabu zangu mimi ni katika Chadema 10 mwenye akili timamu anaweza kupatikana mmoja tu na hii ni kuanzia Viongozi,Wanachama,hadi mashabiki....unaweza mwenyewe kupanga safu ya Viongozi wa Chadema unaowaona mashuhuri(siyo lazima iwe in a positive way) wa'list katika 10,timamu anaweza kuwa mmoja tu....kati ya Wa'CDM 10 waliochangia katika thread hii wewe ndo yule mmoja out of those 10,yaani wengine wanasikitisha kabisa...hoja imewekwa badala ya kuchangia vitu vya maana wao wanaonyesha ulevi,na hivihivi ndo Viongozi wao walivyo ndo maana utasikia mara "funga mlango tupigane" nitamzuia Rais asije Arumeru" na ***** mwingine mwingi tu,kwakweli inaogopesha sana kama hawa ndo tunaotaka kuwakabidhi dola mwaka 2015

Hapo kwenye red, umesahau kutaja yafuatayo:-
"...Liwalo na liwe..."
"... Tutatukana..Kudadadeki..."
"... yaliyompata Dr. Ulimboka aliyastahili, maana yeye ndio kinara wa migomo ya madaktari..." ,
nk. !!!
Hao nao waweke kwenye 'mahesabu' - maana hao ndio walioshika dola kwa sasa !!!
 
Jambo moja ambalo linasababisha CHADEMA wapate wafuasi ni kuzungumza mambo kwa ushahidi.Kuna wakati wametetereka lakini most of the time wanatoa hoja ambazo zina mashiko.
Kuhusu vyombo vya dola ni wazi vina double standard na hili ni jambo la hatari.Kada wa CHADEMA kauawa Igunga lakini mpaka leo hatujasikia viongozi wa CCM wakihojiwa.
Usalama wa Taifa unaangalia maslahi ya viongozi walioko madarakani na ushahidi uko wazi kwani wangefanya kazi yao vizuri EPA na madudu mengine kama kuweka vijisenti abroad yasingekuwepo au wahusika wangekuwa behind the bars.
Kwa ujumla kuna ombwe na mkanganyiko mkubwa na wanachofanya chadema ni kuwazindua Watanzania.
Nakuomba utafute gazeti la raia mwema la wiki hii kuna jamaa kachambua vizuri jambo la vyombo vyausalama.
Tujadiliane kwaamani.

Siyo tu Igunga Mzee, Mapanga ya akina Kiwia Mwanza, Marehemu wa Arumeru Mashariki, hatuoni wabunge wanaoitwa kuhojiwa. Na jana nimesikia mpaka kikundi cha wpelelezi toka Dar wameenda huko Singida kusaidia upelelezi. Actually mtoa mada anajua yote hayo ndiyo maana umeona wachangiaji wengi wameamua "kumgaya" tu ! unajua wakati fulani inasikitisha sana kuona watanzania wanajua ukweli, lakini wanaupindisha maksudi kwa manufaa yao binafsi. Mimi nimeona nguvu inayotumika Singida kupeleleza na kutafuta ukweli, ambayo ni nzuri. Masawali tu ya kuendelea kujiuliza ni pale tu juhudi hizo hazifany kazi maeneo mengine. WATU WAMEZIBA MASIKIO NDUGU YANGU. Any way, tujadili kwa amani, maana inasaidia kupunguza huzuni, japo mh !
 
Mwiba, busara za CCM unaziona? Kuwafokea wabunge wenzao, kaa chini! Toka nje? Mwone alivyo kituko?

Unadhani hawajui ndugu yangu, wanajua yote hayo, but lazima wafanye kazi waliyotumwa. I believe, they know the reality. wanajarubu kupindisha ukweli, NA SIJUI NI KWA FAIDA YA NANI.
 
Kwa nini mwiba umemchoma aliye utegesha na amekimbia badala ya kusikia watu wana omba muongozo kuhusu mada mfu zinazo letwa jamvini?

Kweli makinda hajamtendea haki mwiba kwa kukubali mada yake hipuuzweeeeeee!
 
Wacheni ulimbukeni yaani mnajificha kwa kutafuta yasiyohusika,najua nimewagusa vibaya sana ,na zaidi nyie wafuata upepo na wapiga debe mna tabu sana hapa JF,yaani kama mimi ndio mode hawa wenye majibu yasioeleweka,ningewavunja vidole na kuwatia upofu ,wasiione JF kama mwezi hivi.

Suali lipo wazi ,ni kujibu tu hii Nchi mnaipeleka wapi ikiwa leo hamjui mtendalo,magwanda mazito ,mnatuonyesha ubabe au sio ,CCM yao ya kijani nyie yenu makaki mnataka kuifanyia makeniki na ukarabati hii nchi.

hayo magwanda huvaliwa na madikteta na sera za unyanyapaa pale bungeni na kuvikandia vyombo vya dola ni ishara mbaya za utawala wenu,hivi mtaunda jeshi jipya na usalama mpya ,mmewaahidi wangapi pale usalama wa Taifa kuwapa ulaji ,mnaipeleka nchi hii kubaya zaidi ya hapa tulipo.
liwalo na liwe.
 
Huwezi ukataka kumfurahisha mpinzani wako alafu bado ukafikria kumtoa madarakani.unapaswa kluichagua moja.cdm wamechagua hilo.
 
Vyombo vya dola vyenyewe vinamatatizo makubwa wala usitake kuvitetea sana!!! cha msingi nikuambie kwamba "Ukiwa msafi we ni msafi tu!! na ukiwa mchafu basi we ni mchafu tu!!" Sioni lugha mbadala ya kutumia zaidi hapo na chamsingi wabadilike wafanyekazi kwa mujibu wa katiba na sheria!! Hii itapunguza maswali mengi yasiyokuwa na majibu kwa vyombo vya dola na kuongeza uwazi na kuaminika kwa wananchi maana imani imepungua saaanaaaa!!!
 
Si huyu Hemed Rashid! yeye akainuka akasema "Mh.Spika...kwa busara yako naomba .................."

nashangaa jana alikuwa pamoja na cdma kuvunja kanuni za bunge ambazo cuf wanasema zina vunjwa na cdm kila siku.

Nashukuru wameona rafiki mwema ni yupi!

Hivi baada ya Ahmadi rashidi spika makinda alisemaje?
 
kwa hiyo unataka kuniambia kwamba ccm wana busara sana,amini amini nakuambia kama ccm ingekuwa na busara nchi isingekuwa hivi ilivyo sasa.yale yale akitukana mchemba au lusinde sawa akiongea mccm sawa.kwa uzoefu wangu mdogo kuhusu chadema tabia waliyonayo sasa imesababishwa na kugundua kwamba ccm sio chama cha kujihusisha nacho kibusara busara.we fikiria kila kitu unachomwambia baba yako anapinga tena kwa njia iliyojaa manyanyaso, kutoka moyoni naamini siku moja utamvunjia heshima tu ndicho wafanyacho cdm kwa sasa.
 
Nina hakika ungetumia walau robo tu ya akili yako ungelisema hizi taasisi za serikali zitafanya vipi kazi na CDM itakapokua imechukua Dola 2015? maana hizi taasisi za umma ndizo zinazonyanya paa CDM,
 
Mwiba, busara za CCM unaziona? Kuwafokea wabunge wenzao, kaa chini! Toka nje? Mwone alivyo kituko?

Watu wanasema mtaka cha uvunguni ,sasa kufanya ukaidi si jambo jema ,mnaweza kutumia lugha nzuri na mkafahamika ,wanasema maneno mazuri yanamtoa nyoka pangoni ,unaweza ukamuuliza mtu suali akashindwa kukujibu ,na akakosa pa kukimbilia. Ila ujuba mnaotumia pale mnawarahisishia wengine na wanakuwa wepesi kuwaumbua.
 
Wana wa mungu nawaambia asiyeyaon matatizo ya nchi hii iwe kwa lazima,makusudi,kutokujua na au kwa uzembe hakika mtu huyo ni kipofu au ananyemelewa na upofu.mimi nafikiri wanaopinga hawajawahi kutendwa na dola wacha waongee tu.
 
Hata ccm wakiamua kutawala kwa kufuata sheria kanuni na taratibu wapo watakao ona ccm ni madikteta, Uelewa unahitajika miongoni wa umma, Tunacho kishuhudia sasa ccm kila kitu ni Ruksa kama hakuna uongozi nchi ipo ipo 2 kama haina mwenyewe, Muhimu ccm haikubaliki tena ccm kwa manufaa ya nchi ni muhimu kuisambaratisha kabisa
 
nashangaa jana alikuwa pamoja na cdma kuvunja kanuni za bunge ambazo cuf wanasema zina vunjwa na cdm kila siku.

Nashukuru wameona rafiki mwema ni yupi!

Hivi baada ya Ahmadi rashidi spika makinda alisemaje?
Bibi kiroboto akachomoa kimagamba....ati oh.. kanuni inatumika vibaya....., bunge liendelea mpaka serikali sikivu ya CCM itakapokusanya taarifa za kutosha kuhusu ushiriki wa chadema kusababisha ajari! baadae kidogo waziri wa serikali sikivu akaja na hoja ya kuchomoa hoja ili bunge liahirishwe! bi kiroboto akaingia mkenge !
 
Wacheni ulimbukeni yaani mnajificha kwa kutafuta yasiyohusika,najua nimewagusa vibaya sana ,na zaidi nyie wafuata upepo na wapiga debe mna tabu sana hapa JF,yaani kama mimi ndio mode hawa wenye majibu yasioeleweka,ningewavunja vidole na kuwatia upofu ,wasiione JF kama mwezi hivi.

Suali lipo wazi ,ni kujibu tu hii Nchi mnaipeleka wapi ikiwa leo hamjui mtendalo,magwanda mazito ,mnatuonyesha ubabe au sio ,CCM yao ya kijani nyie yenu makaki mnataka kuifanyia makeniki na ukarabati hii nchi.

hayo magwanda huvaliwa na madikteta na sera za unyanyapaa pale bungeni na kuvikandia vyombo vya dola ni ishara mbaya za utawala wenu,hivi mtaunda jeshi jipya na usalama mpya ,mmewaahidi wangapi pale usalama wa Taifa kuwapa ulaji ,mnaipeleka nchi hii kubaya zaidi ya hapa tulipo.
Hapo kwenye red umesema kweli hawajui kuwa wewe una Phd ya chuo cha MABWEPANDE?
 
futa kauli yako kwanza kumsema mtu aliyefariki kwa ubaya badala ya kumuombea unakuwa hujamtendea haki .
 
Back
Top Bottom