Unyang'anyaji wa Hoja!! Mashiko ya Hoja!!

Moseley

Senior Member
Jul 10, 2010
187
94
Ndugu zangu inasikitisha sana pale ambapo unakuta viongozi wa serikali wanabaki kubwabwaja kuwa hoja hii hatuaitaki maana imeanzishwa na wapinzani.. Au unakuta mwingine anasema hoja hii ilikua yetu upinzani wametunyang'anya..

Hivi kuna umhimu wowote wa kujadili nani kaanzisha hoja?? Kwa nini tushijadili mantiki ya hoja??

Kwa kweli nasikitika sana, kuona viongozi wanashindwa kuzichukua hoja za msingi kwa kusema, eti watampa umaarufu mtu flani!! Huu ni ujuha...

Yaani mtu anaziacha hoja za msingi ambazo zingeleta maendeleo kwa taifa, kisa eti hawataki kumpa umaarufu mtu flani, ambaye yuko upinzani.. Swala la umaarufu wa mtu sie halitusaidii, tunachotaka ni hoja hiyo kushughulikiwa bila kujali imetoka wapi..

Ninakereka sana pale napoona kila mahala siasa tu.. Hivi kweli, kwa nchi maskini kama Tanzania, watu wanaingia bungeni na kuingia na itikadi zao za kivyama?? Tutafika kweli!! Kwa hali iliyopo mie naona ni heri kutokua na bunge, kuliko kuwa na Bunge lililo mzigo kwa wananchi..

Bora mhimili mmojawapo kati ya mihimili mitatu Uvunjwe kuliko kuwa na mhimili chini ya Kinda maana kwa sasa hauna tija kwa taifa na ni mzigo kwa wananchi..
 
Back
Top Bottom