Unyama wodini!

Jeni

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
200
12
Unyama wodini!

2008-10-23 19:35:11
Na Emmanuel Lengwa, Mwananyamala.


Hassan Salum, mume wa mwanamke aliyeripotiwa juzi kupoteza maisha kutokana na kuchelewa kupewa huduma katika hospitali ya Mwananyamala Jijini, ametoa madai mazito dhidi ya wauguzi hospitalini hapo akidai kuwa, mkewe alichelewa kuhudumiwa baada ya kukosa shilingi alfu kumi ya kuwahonga.

Bw. Hassan alitoa madai hayo mazito wakati akizungumza na Alasiri hospitalini hapo, ambako yeye na ndugu zake walikwenda kufuata mwili wa marehemu mkewe na wa kichanga.

Bw. Hassan amedai kuwa alipokwenda hospitalini hapo kumsalimia mkewe Salma Salum, alimvuta pembeni na kumuambia kwamba, manesi wa wodi ya wazazi alimokuwa amelazwa kwa siku kadhaa, walimuomba fedha ili waweze kumpeleka kwa madktari wamhudumie fasta fasta.

``Mke wangu alikuwa na shilingi 3,000 tu...alisema alipowapa hizo lakini wakagoma kuzichukua huku wakimuambia, bila wekundu hapa, hakieleweki kitu,`` akadai Bw. Hassan.

Amedai kuwa mkewe alimwambia kwamba licha ya kuwabembeleza huku akilia machozi kutokana na maumivu aliyokuwa nayo, walimkatalia kata kata wakisema hawapokei pesa pungufu ya alfu kumi.

Sakata hilo tangu mwanamke huyo alipofikishwa hospitalini hapo hadi Mungu anamtwaa liko hivi:
Jumanne Oktoba 14, mama huyo mjamzito alihisi uchungu wa kujifungua na akapelekwa haraka haraka hospitalini hapo kwa ajili ya huduma za uzazi.

Alipofikishwa hospitalini hapo, akapelekwa chumba kujifungulia almaarufu kama `leba` lakini akarejeshwa tena wodini kwa maelezo kuwa njia ya uzazi ilikuwa haijafunguka.

Jumapili Oktoba 19, hali ikawa mbaya na ikagundulika kuwa hata kiumbe kilicho tumboni kilikuwa hakichezi tena kama ilivyo kawaida.

Usiku wa Jumapili hiyo akapelekwa kwa daktari ambaye baada ya kumuona aliona hakuna namna nyingine zaidi ya kumfanyia upasuaji ili kutoa mtoto aliye tumboni.

Hata hivyo wakati akifanyiwa upasuaji, mwili wa mama huyo ukaanza kubadilika na kuwa wa bluu na hatimaye akafariki wakati akiwa huko huko ndani ya chumba cha upasuaji.

Akizungumzia madai hayo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Suleiman Muttani amesema hana taarifa kwamba wauguzi wake walimuomba fedha mama huyo ambaye hivi sasa ni marehemu.

Akasema tangu juzi amekuwa pamoja na ndugu wa marehemu huyo hospitalini hapo wakishughulikia suala la kuchukua miili lakini hawakumweleza madai hayo ya kuombwa fedha na wauguzi.

Alasiri ilipomuuliza chanzo cha kifo hicho, Dk. Muttani alisema hawezi kujua kwa vile ndugu wa marehemu jana walikataa mwili wa mpendwa wao kufanyiwa uchunguzi.

``Tulipowaambia tufanye uchunguzi, walikataa na kukuuchukua kwenda kuzika,`` akadai Dk. Mutani.

Alasiri ilipomtaka Dk. Mutani kueleza sababu za mama huyo kukaa hospitalini hapo kwa siku sita bila kupewa huduma, alisema hawezi kujibu swali hilo.

``Hilo siwezi kulijibu,`` akasema Dk. Mutani na kisha akakata simu.

Mwili wa mama huyo ulichukuliwa hospitalini hapo na ndugu zake jana mishale ya saa 9:00 alasiri na kuzikwa jana hiyo hiyo katika makaburi ya Tandale uzuri, Jijini.

Hii ni mara ya pili kwa hospitali ya Mwanayamala kukumbwa na kashfa ya kusababisha kifo cha mama mjamzito katika kipindi cha mwaka mmoja.

SOURCE: Alasiri

Hivi jamani haya matatizo yataisha lini??
 
Du hii inasikitisha sana, kwa kweli kama hali ndo imefika hapa inatakiwa waziri wa Afya ajiuzulu mara moja. Mjamzito anakaa siku 5 akisubiri njia kufunguka? hii mpya kwa kweli. Hali inatisha.

On the other side kwa upande wetu na sisi wananchi tuwe tunaangalia jamani, kujiandaa wakati mama anatarajia kujifungua, any thing can happen na tunajua hapa kwetu bila pesa mambo hayaendi na hii hali haitabadilika mpaka hapo CCM itakapoondoka madarakani. tusiwajaze mimba wake zetu kama hakuna uwezo
 
mbona wameweka record wala hawashituki wala kujali .. wananini??? wameshaundiwa tume lakini situation bado ni ile ile hamna hatua inaechukuliwa .. jamani eeh maybe kwa kuokoa maisha ya wapendwa wetu tusiende kutibiwa huko .. maana hawa wamekuwa si nunda tu bali ni machinjachinja na wachawi watatumaliza
 
mbona wameweka record wala hawashituki wala kujali .. wananini??? wameshaundiwa tume lakini situation bado ni ile ile hamna hatua inaechukuliwa .. jamani eeh maybe kwa kuokoa maisha ya wapendwa wetu tusiende kutibiwa huko .. maana hawa wamekuwa si nunda tu bali ni machinjachinja na wachawi watatumaliza

....Naima, laiti kungekuwa na uwezekano wa kuwagomea hao jamaa kwenda kutibiwa huko ingekuwa wazo zuri sana ili angalau watakapokuwa idle bila kazi watatia akili maana watasinzia mpaka wakome. Lakini wenzetu wengi si unanua tena uwezo mdogo so lazima wataenda huko..But kwa kweli wahudumu kwenye hii hospitali kuna haja ya kuwachukulia hatua angalau kutoa fundisho....
 
Hawa jamaa hawakomi . Mimi nadhani ni Mganga mfawidhi wa hiyo hospitali inabidi awajibishwe ikiwezekana ajiuzulu.
 
Unyama wodini!


Hivi jamani haya matatizo yataisha lini??[/QUOTE

Kwa mara ya kwanza nilipoandika thread yenye Subject "HOSPITALI YA MWANAYAMALA YAGEUKA KUWA MACHINJIO YA WAJAWAZITO NA WATOTO" kuna watu walikuja juu wakinitaka nitoe ushahidi wa tuhuma zangu, nikagundua kuwa mjadala niliouanzisha hautafika mbali kwa sababu umegusa kwenye mfupa wa mtu. Na kwa kubaini hilo sikutaka kubishana kwa sababu kama mtu hajui maana, usimwambie maana.

Tatizo la Mwananyamala halitakwisha kwa sababu wahanga ni masikini wa Manzese, Tandale Kwa Mfuga Mbwa, Mwananyamala kwa Tumbo na kwingineko ,ambao hawana wa kuwatetea wala kuwasemea. Matatizo katika Hospitali zetu hapa nchini ni matokeo ya wanaoyajua kuyafumbia macho na hata wenye uwezo wa kuyasemea, hukaa kimya kwa imani kuwa hayawahusu.
Lakini watu wakumbuke kuwa "MWENZIO AKINYOLEWA WEWE, TIA MAJI KICHWANI" kwani kama hayatokea kwako, yatatokea kwa ndugu yako, jirani au hata mwanao.
 
Mwananyamala this is too much sasa,Wizara ya Afya isafishe hiyo hospitali,wawajibishwe kuanzia mganga mkuu na waliohusika wote, kuna manesi hapo naona wameshakuwa manunda na hamna hatua zinazochukuliwa. Inasikitisha sana kwakweli.
 
Heee jamani M/nyamala asiejua nani kama nimachinjioni pale nashindwa kuelewa inakuaaje Wizara husika imelifumbia macho swala hili nahali inaendelea kuwa mbaya jamani,hospitali hii inaongoza kwakuwa na matukio mabaya ikifuatiwa na Temeke niliwahi kuwa na mgonjwa temeke nilitaka kulia ilibidi tutafute dr mwingine kwa msaada zaidi.
 
Ili wizara ianze kufanya kazi kimaadili na kisayansi inabidi wasomi waiongoze. Naibu waziri ni assistant medical officer, atajua wapi jinsi hospitali zinatakiwa ziwe?kwa exposure ipi? Halafu tafadhali huyu mama asiwakilishe wizara kwenye scientific conferences, aende mtu anaejua anaongea nini. Anatia aibu..., nothing personal, just stating facts.
 
Back
Top Bottom