Unyama wa serikali Urambo waanikwa bungeni na Sakaya-CUF

MANGI MASTA

Senior Member
Jul 14, 2011
175
56
Mbunge wa viti maalum CUF-Urambo, Magdalena Sakaya ameeleza jinsi polisi,askari wa wanyamapoli na maliasili walivyochoma nyumba za wakazi wa Urambo, walivyopiga risasi na kuuwa wananchi 23 wa Urambo mwaka 2010 mwezi 9.

Wakazi walichomewa nyumba zao kwenye kijiji cha Pandamlohoka, askari walichukua mtoto wakamweka juu ya kaburi la mama yake.

"Mheshimiwa spika unyama kama huu unafanyika serikali iko wapi..?"

Kwa aliyekuwa akimsikiliza Sakaya lazima machozi yalikuwa yakimlengalenga. Hii ndo serikali ya chinjachinja na chama chinjachinja. Mhe Sakaya alikuwa akichangia bajeti ya wizara ya maliasili.
 
Hapa namsikiliza waziri Maige wa maliasili bungeni akijibu michango mbalimbali ya wabunge amehaidi kuunda Tume ya kushughulikia tuhuma za unyanyasaji dhidi ya wakazi wa URAMBO tabora.

Tuhuma hizo ni zile za mauaji ya wafugaji urambo,kuchoma moto nyumba za wakazi wa Urambo,kuua m ifugo nk.Tuuhuma hizi ziliwasilishwa leo asubuhi na Mbunge viti maalum CUF urambo.

Mh Magdalena Sakaya
 
tume tume mpaka mwisho na majibu watupe sio inaishia kuwekwa kabatini inakula vumbi
 
Ni kweli huyu mbunge amenitoa machozi. Wakati nikimsikiliza, machozi yalinilenga, alipoelezea ule unyama wa mama anayeyonyesha kuuliwa kwa risasi, mtoto alipolia njaa, wakampeleka kumlaza kwenye mwili wa mama yake, mtoto bila kufahamu mama kauliwa, akawa unagangaika na mwili wa mamaye kusaka maziwa huku analia, polisi wauawaji wakiangalia kama horor film!. Machozi yalinitirika!.
 
Msitake kunambia Spika hakuomba iundwe kamati haraka ya kuchunguza janga hilo?
 
waziri mkuu kupitia waziri maige wamedai wataunda tume ya kuchunguza hayo.Cjui ni janja ya kupitishia bajeti?
 
Ni kweli huyu mbunge amenitoa machozi. Wakati nikimsikiliza, machozi yalinilenga, alipoelezea ule unyama wa mama anayeyonyesha kuuliwa kwa risasi, mtoto alipolia njaa, wakampeleka kumlaza kwenye mwili wa mama yake, mtoto bila kufahamu mama kauliwa, akawa unagangaika na mwili wa mamaye kusaka maziwa huku analia, polisi wauawaji wakiangalia kama horor film!. Machozi yalinitirika!.
<br />
<br />
Upande mmoja: askari mmoja nchini Kenya alitoa mshahara wake wote wa mwezi mmoja kusaidia watu wlioathirika na njaa baada ya kuguswa na kisa cha mama mmoja wa Somalia aliyekufa kwa njaa akiacha mtoto mdogo asiyejua lolote aking'ang'ania matiti ili kutibu njaa kwa masaa kadhaa. Upande wa pili: askari wanafanya yaliyoelezwa hapa juu!!!
 
Ni kweli huyu mbunge amenitoa machozi. Wakati nikimsikiliza, machozi yalinilenga, alipoelezea ule unyama wa mama anayeyonyesha kuuliwa kwa risasi, mtoto alipolia njaa, wakampeleka kumlaza kwenye mwili wa mama yake, mtoto bila kufahamu mama kauliwa, akawa unagangaika na mwili wa mamaye kusaka maziwa huku analia, polisi wauawaji wakiangalia kama horor film!. Machozi yalinitirika!.
Mkuu Pasco hii kweli inatisha, huyo Bwn Six alikuwa wapi??????????? Kazi ya maghambas ni kuu tuu kila kona ya Tanzania ehee Mungu Okoa taifa la Tanzania!!!!!!!!!!!!
 
Sakaya chama chake kinamuangusha mf angalia jinsi alivyo fungwa lakini chama kikawa kimya kama hawamfahamu vile
 
makinda kamtaka waziri achunguze pia kitendo cha DC wa urambo kunyang'anya raia mbuzi kwa ajili ya kitoweo.SHAME ON ALL THIS KIND OF LIDERS
 
Ni kweli huyu mbunge amenitoa machozi. Wakati nikimsikiliza, machozi yalinilenga, alipoelezea ule unyama wa mama anayeyonyesha kuuliwa kwa risasi, mtoto alipolia njaa, wakampeleka kumlaza kwenye mwili wa mama yake, mtoto bila kufahamu mama kauliwa, akawa unagangaika na mwili wa mamaye kusaka maziwa huku analia, polisi wauawaji wakiangalia kama horor film!. Machozi yalinitirika!.
Ooooh No!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom