Unyama huu wa serikali mpaka lini?

naggy

Member
Apr 27, 2011
97
152
Serikali mkoani Shinyanga jana imetimiza azima yake ya kwenda Makao wilayani Meatu kuwafukuza kwa NGUVU (kama kawaida yake) kaya zaidi ya 600 kama ilivyotangaza. Huwezi amini, gari za polisi zaidi ya 20 zimepitisha mapolisi wakiwa na siraha zao na wameweka kambi maeneo tofauti karibu eneo la tukio. Wameamua kuongeza nguvu ya kuwafanyia unyama hawa wananchi raia halari wa Tanzania kwa kuchukuwa wanajeshi wa JKT, sijajuwa ni kutoka kambi gani. Lori la halmashauri ya wilaya ya Meatu lilionekana jioni saa moja likiwa limebeba magodoro kwa ajiri ya askari wanakambi.

Kama hiyo haitoshi, serikali imeamua pia kutumia raia walio tayari kushirikiana na polisi kwenye operation hiyo kwa malipo ya fedha za kitanania laki moja na nusu. Lakini mwitikio wa raia umekuwa mdogo sana kwa sababu kila mwananchi anakerwa na kitendo cha kinyama kinachofanywa na serikali kwa watu wake na kuthamini wawekezaji. Wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya wilayani hapa jana hiyo walihamishiwa kwenye wodi za zamani ili kuandaa sehemu ya kufikishia majeruhi kwenye operation hiyo, hii ni ajabu kweli.

Maswali mengi wananchi wa Meatu tunajiuliza: kwa nini nguvu nyingi inatumika kunyanyasa wananchi? Kwa nini serikali inatumia gharama kubwa hivi kunyanyasa wananchi wake? Kwa nini serikali inathamini sana wawekezaji kuliko wananchi wake? Kila mwananchi hapa anailaumu serikali, je hiyo serikali iko kwa ajiri ya nani kama haiwathamini wananchi wake? Tutakosea tukitumia nguvu ya umma kuipinga serikali hii kandamizi?

Ombi kwa vyombo vya habari

Angazieni jicho kwenye Operation hii ili watanzania tuone unyama unaofanywa na serikali kwa wananchi wake.
 
Busara zaidi zinahitajika. Kwa hapa tulipo tuna bora viongozi na si viongozi bora.
 
Jamani vingozi wetu mnatupeleka wapi? Hivi mwekezaji ni muhimu kuliko mwananchi? Hivi ni nchi gani inaweza kuwafanyia wananchi wake duniani kama siyo Tanzania pekee; kwakweli inaniuma sana haya yanayotokea na inanifanya nisisahau kamwe yaliyonikuta Oktoba 2005. Ipo siku nitawafahamisha kinachonifanya nisisahau hiyo siku kamwe ktk maisha yangu.
 
Wa Meatu na wana Shinyanga kwa ujumla kama mnaona serikali haiwatendei haki kataeni kama wana Mbeya walivyofanya,kubalini kupambana na hao vibaraka,na msipoangalia watawapora hata ng'ombe wenu.kwa serikali ya CCM wao mwekezaji ndio mwenye haki na anastahili kuliko mtanzania mwenye nchi yake,kataeni kama walivyokataa wana nchi wa Babati kwa muwekezji wa mashamba ya miwa.
Nchi hii inataka nguvu ya umma tu na wala si vinginevyo
 
jamani kikwete kweli ni binadamu au ni sanamu mbona anaingiza nchi kwenye migogoro ya kipuuzi sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! jamani naona kama ccm wataingiza nchi kwenye vita si muda
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom