Unyama Geita (Niger Delta ya Tanzania): Picha hizi ndiyo Taswira halisi ya Ufisadi na Dhuluma

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
Tarehe 7 Mwezi August mwaka 2011, ITV walitangaza kuhusu unyama wa kutisha wanaofanyiwa wananchi wa Geita .Serikali imeshindwa kuchukua hatua madhubuti kumaliza tatizo la watu waliostahili kulipwa fidia baada ya kuhamishwa kwenye makazi yao na Mgodi wa Geita Gold Mining.

Hadi sasa hali ni mbaya,wananchi wanaishi katika mazingira magumu vifo na udhalilishaji wa hali ya juu.Geita sasa haina tofauti na Niger Delta (iliyokuwa na utajiri mkubwa wa mafuta nchini Nigeria,huku wananchi wake wakiteseka kutokana na uwekezaji wa makampuni ya mafuta kutoka nje).

Ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa nchi yenye serikali iliyoridhia mkataba wa haki za binadamu wa mwaka 1948 na pia kwa serikali yenye uwakilishi katika idara na ngazi zote. Ingawa serikali mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu iliyoruhusu wananchi kubakia katika makzi yao hadi kesi ya msingi kuhusu fidia itakaposikilizwa,mkuu wa Wilaya ndugu Shelutete alisimamia zoezi la kuhakiksha wananchi wanaondoka maaeneo hayo pasipokujua wanaelekea wapi wengine wakiwa wajawazito,wagonjwa na wazee.Picha za mahema unazoona hapa chini ni msaada kutoka mashirika ya Dini.Wananchi hawa wako katika eneo hili tangu mwaka 2004 na hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha.

Hii ndiyo taswira halisi ya uwekezaji uliofanywa na serikali ya CCM kupitia sera zake za uwekezaji zilizoasisiwa na chini ya Uongozi wa Mh.Benjamini Mkapa (Wakati Rais wa Sasa Jakaya kikwete akiwa waziri wa mambo ya nje),wote kwa pamoja kwa kushirikiana na Wageni (kutoka Afrika Kusini) walisimamia zoezi hili lillilozaa wakimbizi ndani ya Ardhi ya Geita.

Jana ilikuwa tufanye mkutano wa hadhara uliohujumiwa katika mazingira ya kutatanisha,tulitembelea kwenye kambi ya wakimbizi hawa nikiwa na Kamanda Grayson Nyakarungu,Kamanda Otto-Mwenyekiti wa BAVICHA Geita,Diwani Machachari Vitimaalum kata ya Kagu Kamanda Marceline Simbasana na Viongozi wengine wa BAVICHA






IMG_3824.jpg IMG_3810.jpg IMG_3811.jpg IMG_3813.jpg IMG_3801.jpg IMG_3808.jpg IMG_3799.jpg IMG_3803.jpg IMG_3812.jpg IMG_3814.jpg IMG_3817.jpg IMG_3819.jpg IMG_3796.jpg IMG_3805.jpg IMG_3821.jpg
 

Attachments

  • IMG_3816.jpg
    IMG_3816.jpg
    53 KB · Views: 55
Ben bahati mbaya hujaattach picha yoyote hapo
Asante kwa taarifa ila jua kwamba hii ni tanzania bana
mahakama inaweza kuamua hivi watawala wakaamua kivingine kabisa
 
hongereni kwa kuwaamsha walio usingizini.ngoja tuongee na uongozi wa juu tuje tuongeze nguvu
 
hongereni kwa kuwaamsha walio usingizini.ngoja tuongee na uongozi wa juu tuje tuongeze nguvu

Wakuu wangu JF na wanaharakati wengine tuungane katika kupambana na suala hili, Hali ni mbaya sana Geita,watanzania wenzetu wanaangamia kutokana na ukandamizaji na unyanysaji unaosababishwa na wageni kutoka nje.Wazee unaowaona hapa kwenye picha watoto wao wawili walifia hapa kwa magonjwa na njaa,wamebaki na wajukuu ambao hawawezi kuwalea.Pia Kuna wajane ambao wamefiwa na waume zao hapa kwa matatizo yanayotokana na frustration za suala hili.

IMG_3804.jpg
 
Halafu huyu Shelutete kwa wale waliopita Usagara late 70's sio yule aliekuwa anafundisha chemistry form ii & iii kama ndie siwezi kusema lolote .
 
Mimi naona Tatizo hapa ni serikali na sio kampuni hizo pesa zinaenda wapi kama haziwezi kusaidia wanakijiji wa pale. Kila siku wanasema pesa inaenda serikalini- je serikali ni nani kama sio watu! serikali ni Dar!!!!
 
Geita ilikuwa ya enzi hizo bana kulikuwa na ardhi nzuri sana ya kilimo cha pamba, muhogo, maharagwe, matunda etc lkn siku hizi wasumbwa wamebaki walevi wa pombe za kienyeji, wengine wamekuwa security guards wa mgodi na wengine wengi ni vibarua ambao ni pay per day na hawana mkataba wowote ule na kampuni, ardhi walishapewa wazungu kuchimba dhahabu na watu wa darisalama na kwa sasa wanawake wengi wamekuwa makahaba wa mgodi na mahouse girl
yamebaki mashimo tu pale na hata huduma ya maji hali ni tete, vyanzo vya maji vimeharibiwa na makampuni. Huduma za afya ni masikitiko. Hawa wawekezaji sijui wanafaida gani zaidi ya hasara
 
Geita ilikuwa ya enzi hizo bana kulikuwa na ardhi nzuri sana ya kilimo cha pamba, muhogo, maharagwe, matunda etc lkn siku hizi wasumbwa wamebaki walevi wa pombe za kienyeji, wengine wamekuwa security guards wa mgodi na wengine wengi ni vibarua ambao ni pay per day na hawana mkataba wowote ule na kampuni, ardhi walishapewa wazungu kuchimba dhahabu na watu wa darisalama na kwa sasa wanawake wengi wamekuwa makahaba wa mgodi na mahouse girl
yamebaki mashimo tu pale na hata huduma ya maji hali ni tete, vyanzo vya maji vimeharibiwa na makampuni. Huduma za afya ni masikitiko. Hawa wawekezaji sijui wanafaida gani zaidi ya hasara

Huku zebaki inatumika kuoshea mawe kwenye vyanzo vya maji.Watu wanakufa hovyo,wanaugua kansa.
 
Back
Top Bottom