Ununuzi wa luku kwa Mpesa kero tupu

kiyeyeu

Member
Jan 7, 2011
38
1
Hii kampuni ya voda bado haijajipanga vizuri kupitia huduma yake ya MPESA, unanunua umeme saa hizi unakuja kutumiwa tokeni kesho yake na kama umeme umeisha ndio unalala giza lol!
 
Nilidhani ni Voda hapo mwanzoni nikambiwa kuwa kuna kampuni tatu ziko involved hapo, unanunua LUKU through M-pesa interface ikitoka hapo inapitia kampuni inaitwa Paynetops hawa server zao ziko Kenya, ikitoka huko ije kwa Selcom ya Tanzania then itue TANESCO kwenye sever zao chovu ichukue hizo Token halafu irudi tena kuppitia mtiririko huo huo. Tanesco wana server ziko very slow yaani extreme slow na za kizamani hawataki ku upgrade, wakitaka ku upgrade lazima ufisadi upite hapo so mkuu si Voda kama unavyofikiria lkn TANESCO ndio chanzo cha hayo matatizo yooooote unayoyapata!
 
Hii kampuni ya voda bado haijajipanga vizuri kupitia huduma yake ya MPESA, unanunua umeme saa hizi unakuja kutumiwa tokeni kesho yake na kama umeme umeisha ndio unalala giza lol!

kiyeyeu,

Nenda tu kanunue LUKU kwenye vituo - MPESA inaweza kukulaza giza siku 2.. Ni similar case kwa DAWASCO, e.t.c
 
Kumbe ndio maana nikinunua umeme kupitia M-pesa naliwa almost tho thirds ya hela yangu na inayobaki ndio inanunulia umeme! Nimelaani kweli mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia hiyo. 5000 kwa mfano inapata umeme wa 2200, tena wanaandika kila kitu bayana, wanyang'anyi hawa na wala sio wezi.
 
Pole mi tangia nimejua M pesa kwa swala la Luku na DSTV sijapata shida yoyote na nimekuwa naitumia kwa muda mrefu inaweza kuchelewa lakini some few hours, sema huwa sisubirii mpaka iishe na kwa kuwa nimeshajua consumption yangu kwa mwezi inanisaidia kuto kulala giza.

Ila kwa Dawasco sijawahi kujaribu maana hata uki depost Bank wanachelewa ku receipt ila wanawahi kukata maji kwa hiyo ni bora niende ofisini kwao nipate receipt kuliko ku deposit au kutumia M pesa.
 
Back
Top Bottom