Ununuzi wa kiwanja Morogoro

Cassava

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
282
36
Heshima kwenu wadau,

Si watu wote wanaonunua viwanja mara tu vinapopimwa na manispaa husika, hii hutokana na kukosa pesa wakati huo, kutokuwa na habari au kuwa mbali wakati upimaji unapofanyika hivyo kutokutuma maombi. Kwa maana hiyo basi inapelekea kununua ki (vi)wanja kwa mtu aliyepimiwa na manispaa kwa bei ya juu kidogo.

Sasa wadau wa mji kasoro bahari (MOROGORO) au wale wenye ufahamu wa mji huu, naomba kuhabarishwa ni njia ipi sahihi ambayo mtu hawezi kuingizwa mjini akinunua kiwanja kilichopimwa kwa mtu mwingine, hapa morogoro mjini. Manake viwanja huwa na migogoro sana, unaweza kuuziwa kiwanja walichokwisha uziwa watu wengine ikawa soo. Naomba kuelekezwa njia sahihui nisije lia manake pesa ya siku hizi imekuwa ngumu mno na kununua kiwanja ni kujibana.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom