University of Dodoma - Photos !

Wewe acha mawazo ya kifisadi, fisadi Mkapa hahusiki na chochote UDOM
TzPride, Give the praise where it belongs!!! It was Mkapa's Job man!!! Mot of us know about except you!!! Or you are trying to blind yourself. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!!
 
kusema ukweli jamaa hapo amejitahidi, unajua Watanzania lazima tuwe wepesi wa kukubali jambo jema na baya kama lipo, kusema ukweli kuhusu chuo cha Dom hata mwenyewe JK namfagilia, amepanua wigo wa elimu Tanzania, si tu kubanana pale mlimani, elimu ya mlimani yenyewe imepitwa na wakati, kukaririshana tu-----huu sio wakati wa mwanafunzi kukariri, tunahitaji elimu ya vitendo, kama research tufanye reasearch na kama course work basi iwe hivo

Big Up JK, na aje raisi mwingine atujengee chuo kikuu kingine, at least baada ya miaka 40 mingine Tanzania iwe na wasomi asilimia 65 ya wakaazi wote, elite group iongezeke na hatimaye tupate mapinduzi ya kiucchumi na kisiasa.
 
TzPride, Give the praise where it belongs!!! It was Mkapa's Job man!!! Mot of us know about except you!!! Or you are trying to blind yourself. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!!

Mkuu Nanu, sasa unataka kuudanganya umma kuwa lilikuwa wazo la Mkapa. Hili ni wazo la Kikwete na kafanikiwa kulitekeleza, na hata katika Ilani ya CCM halikuwepo, bali aliahidi katika mikutano yake akiwa Rais atajenga Chuo Kikuu kingine Dodoma. Na kalitimiza hilo, sijui unataka kumdanganya nani.
 
Aliyepiga picha hizi sio mtaalamu japo kajitahidi, ilitakiwa kila picha iwe na maelezo ya kijiografia kuwa hapa ni eneo gani nk, sio kupachika tu mipicha haieleweki,
 
Kweli Dodoma kuna ukame na pia wanafunzi wengi wa huko wanasema kuwa wao wanapata maji kwa siku mara 2 hivi sasa hapa ndio kuna kazi kubwa sana katika ujenzi wake

...kuna ukame lakini sio sababu ya kukosa maji,ni uzembe wa hali ya juu kutokuwa na maji kwa chuo kama hiki,cheap & simple tech ya sasa inaweza kuwapa maji 24/7....ni uzembe tuu na hakuna excuse hapo!
 
Jaribu kutazama katika vyuo vingi sana Taifa la Israel kuna ukame ila maji yapo, kutokuwa na maji ni uzembe wetu sisi mwenyewe
 
Aliyepiga picha hizi sio mtaalamu japo kajitahidi, ilitakiwa kila picha iwe na maelezo ya kijiografia kuwa hapa ni eneo gani nk, sio kupachika tu mipicha haieleweki,
Itafaa sana kama siku moja na wewe ukapigapichs ns kuleta hapa na sisi tuone
 
Mbona kinafanana na vyuo vya kichina? Hata mabasi ni ya China YUTONG.... Je, kitatoa degree feki za kichina china?
 
Simaanishi kuwa china kuna vyuo au vyuo vyake vinatoa degree feki
Hahahah ni kweli kabisa, Wajenzi wakubwa sana kule ni kutoka China na pia hata tender yenyewe walishinda wachina na kupewa kazi ya kujenga, mifumo mingi sana ya maji taka sio mizuri sana
 
Mkuu Nanu, sasa unataka kuudanganya umma kuwa lilikuwa wazo la Mkapa. Hili ni wazo la Kikwete na kafanikiwa kulitekeleza, na hata katika Ilani ya CCM halikuwepo, bali aliahidi katika mikutano yake akiwa Rais atajenga Chuo Kikuu kingine Dodoma. Na kalitimiza hilo, sijui unataka kumdanganya nani.
Alichukua kutoka kwa Freeman Mbowe, wa CHADEMA rejea kwenye mikutano yale Dodoma mwaka 2005 aliyasema haya kabisa juu ya kufanya Dodoma uwe mji wa vyuo vikuu na CCM walichukua toka Dodoma
 
Josh,
Kweli kabisa. Hata hii ya kupitia upya mikataba ya madini ilikuwa sera ya CHADEMA. Ndiyo maana anaifanyia kanyaboya kwa sababu rohoni hana nia ya kufanya mabadiliko yeyote.
 
Mkuu JM, suala sio wapi alichukua hilo wazo. Mimi nilikuwa nawajibu wale waliokuwa wanasema ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ulianzishwa na Mkapa. Ndio nikasema kuna uongo ukizidi haifai kukaa kimya. Kila mtu anajua Kikwete ndio mwanzilishi wa wazo mpaka ujenzi na sasa kuna wanafunzi na kinaendelea jengwa.

Kuhusu kuwa kuwa hiyo ilikuwa sera/wazo la CHADEMA. Siwezi pinga ama kataa. Lakini hata kama ilikuwa ni wazo la CHADEMA huoni kafanya jambo jema. Kwa nchi zenye demokrasia kuna vipaumbele, kwa kila chama kitavifanya hivyo. Sio ajabu kama sera nzuri ikianzishwa na upinzani, chama tawala kuichukua na kuifanyia kazi, hiyo ndio kujali Wananchi na Taifa kwa ujumla. Haimaanishi kuwa chama chochote cha upinzani kikiingia madarakani basi sera zote zilizokuwa zinatekelezwa za CCM wataziacha. Hivyo kama sera ni nzuri, hakuna ubaya alieko madarakani kuifanyia kazi.
 
Kazi ya vyama vya siasa ni kutoa sera mbadala kwa vyama tawala na ni vyama kivuli katika uongozi, Ndio maana katika Mataifa makubwa kuna parties bipartzim kwenye mambo mengi ya msingi na kuamua, Badala ya kuamua chama tawala pekee na vyama upinzani pia wanaamua kwa pamoja, Hilo halina ubishi, Kodi ya kichwa ilifutwa kwa sababu ya Lipumba na sera zao, Halimashauri nyingi sana Tanzania zinafuta sana sera za CHADEMA kule Karatu na sehemu nyingine, Hivyo Sisi kama Watanzania ndio tumepata faidi kwa ajili ya CHADEMA
 
Tusiwe always negative thinkers, kitu kikifanyika tuwe tayari kukubali ni kweli mkuu kwa Dodoma kafanya kweli anahitaji sifa zake na heshima ya juu
 
Ni kweli kabisa yeye amejitahidi sana katika kuweka na kufanya chuo hicho kuwapo na kuwa kamali!! Kazi nzuri sana
 
hapo ndipo watu makini wanakubali kuwa JK kwa hili na chuo kikuu Dodoma alicheza.
chuo hichi kimebadili kabisa mji wa Dodoma.
 
natamani uzuri wa nje wa majengo hayo ungekuwa sawa na ubora wa majengo ya chuo kikuu cha dar es salaam!.....kuna siku watu watakumbuka comments yangu hii niliyoiandika leo!.........tuyape miake mitano afu tutasema kuhusu ubora wake!
 
Those buildings look cheap. I doubt if they gonna last longer.....for the investment to meet sustainability criteria. University is something which should be built to last forever. Hayo majengo ya rangi za kichina hayafai kwa taasisi kama hiyo.

I agree with you.

Tutaomba aliyeleta picha hizi, baada ya miaka mitatu atuletee tena picha atakazopiga wakati huo.
 
Back
Top Bottom