Mkuu hivyo viwango kwa ufahamu wangu mdogo ni kwa wale wanaoajiriwa at international level. Viwango vinavyotumika hapa kwetu sio hivyo. Viwango vinavyotumika hapa kwetu vinawekwa na UNDP baada ya kufanya salary survey kwa kutembelea local entities zinazolipa vizuri. Vile vile kutaja kiasi kidogo au kikubwa kwenye interview akuzuii mtu kupewa kazi kwani mara zote UN wakitangaza kazi wanaweka wazi viwango vya mishahara ambavyo watamlipa successful candidate. Hivyo hata ukisema kidogo, hawawezi kurudi nyuma na kupunguza kiasi ambacho waliishakitangaza au ukisema nyingi hawawezi kulipa zaidi ya kile walichokitangaza.
Kama ulikuwa umelenga kutujuvya juu ya internationally recruited staff salary scales, then tunashukuru sana.
Tiba