Unikome, Sikutaki Tena, kumbe 'Unanichezea Bure'

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
35,999
24,163
Mara nyingi kwenye mahusiano, hasa kwa wadada, unakuta analalamika au anatoa maneno

unikome, sikutaki tena, kumbe unanichezea bure.

Hili suala la mmoja kumchezea mwenzake inakuwaje?

Je ni kweli wanamme tu ndio huchezea wadada?

Au hata mdada anaweza mchezea mwanamme?

Kwa nini isiwe wote wanachezeana?

Hebu nisaidieni kudadavua hili.
 
mi nafikiri labda mwanamke anapoanza uhusiano wa kimapenzi na mwanaume anatarajia kuolewa na mwanaume huyo kwa kipindi kifupi toka waanze uhusiano, akiona mda unazidi kwenda na labda mapenzi ya bf wake hayajamridhisha lazma atakwambia unamchezea na kumpotezea muda, NI MTAZAMO WANGU ILA SABABU ZAWEZA KUTOFAUTIANA
 
Please nisaidie, naenda kutoa mada mahali fulani, mwaga mapweint mwali.
Unatolea wapi? ukitoa basi sema source: Mwali wa JF. sawa?

Nadhani mwanamke akisema anachezewa au anapotezewa muda
ni sababu ya mtazamo tofauti ya mahusiano:
Wanawake wengi wanaingia katika mahusiano
huku wakilennga kitu kingine (pesa? nyumba? gari? ndoa?)
Mwanaume anaingia katika mahusiano sababu anataka
mapenzi na sex (hasa sex), na si zaidi ya hapo at first.

Sasa pindi mwanamke anapoona kua hakuna kitakacho kuja
zaidi ya mapenzi ya siku kwa siku (kwenda out, ku-do etc)
wakati yeye alikua katika investment akitegemea a high return ambayo haiji,
Wakisha korofishana na kila mtu kuweka nia yake wazi
ndio husema alikua 'anapotezewa muda', wanamchezea (kuchezea mwili)
inaonekana mmoja alikua anapata anacho kitaka, mwenzie 'anachezewa'.

Natangulia kusema kua sio wanawake wote wanaingia katika mahusiano
kwa kulenga something more out of it. wengine hu-enjoy kila dakika
Na sio wanaume wote wanataka sex na outing tu, kuna wanao taka more pia.
 
Hivi kwenye mahusiano inatangulia ndoa au upendo na compartibility kati ya wahusika?

Mnaweza kuanza mahusiano tu, mkajikuta mmeendana kiasi cha kuanza fikiria kuoana

au mnaweza anza mahusiano, mkakuta hamwezi kaa pamoja.

mi nafikiri labda mwanamke anapoanza uhusiano wa kimapenzi na mwanaume anatasajia kuolewa na mwanaume huyo kwa kipindi kifupi toka waanze uhusiano, akiona mda unazidi kwenda na labda mapenzi ya bf wake hayajamridhisha lazma atakwambia unamchezea na kumpotezea muda
 
Mara nyingi kwenye mahusiano, hasa kwa wadada, unakula analalamika au anatoa maneno

unikome, sikutaki tena, kumbe unanichezea bure.

Hili suala la mmoja kumchezea mwenzake inakuwaje?

Je ni kweli wanamme tu ndio huchezea wadada?

Au hata mdada anaweza mchezea mwanamme?

Kwa nini isiwe wote wanachezeana?

Hebu nisaidieni kudadavua hili.

Baadhi ya maswali yako, kama sio yote, yanaweza kujibiwa na hii article.

Si wanawake tu, hata wanaume nao huchezewa na kuachwa! Part 1

RAFIKI zangu leo nimekuja kivingine kabisa, nataka kuzungumza na wanawake kuhusu vilio vya wanaume. Yap! Ni kweli, nao pia wanalia kama wanawake wanavyolia. Wanateseka kama wanavyoteseka. Wanapata tabu na matatizo ya moyo sawa na wanawake. Hata hivyo, wengi hawapati nafasi ya kuwaelezea. Leo ni zamu yao.

Kwa utamu wa mada na jinsi nilivyo na haraka, nimesahau hata kuwasalimia...mambo marafiki? Mko poa? Bila shaka mtakuwa wazima wa afya njema na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku. Karibuni tujifunze katika mada yetu ya leo.

Imekuwa ni kawaida sana kusikia wanawake wakilalamika baada ya kuachwa au kuachana na wapenzi wao, kwamba wamepotezewa muda, wamechezewa n.k. Hizi zimekuwa kauli za kawaida kabisa katika jamii, lakini ukitazama kwa upana dhana hii ina matatizo kidogo.

Hebu tujiulize pamoja, kuchezewa ni nini haswa? Kwanini wanawake wamekuwa na tabia ya kulalamika kwamba wamechezewa? Ni kweli kwamba wanaume nao hawawezi kuchezewa na kuachwa? Bila shaka yoyote, majibu ya maswali haya utayapata katika mada hii ambayo itakuongezea jambo fulani kichwani mwako.

DHANA YA KUCHEZEWA

Inawezekana kila mmoja akachambua kwa mtindo wake, lakini mwisho maana inabaki katika mlengo mmoja tu, kupotezewa muda, kutumika kimapenzi! Hiyo ndiyo maana ya moja kwa moja.

Kama ndivyo, mwanaume ana kitu gani cha tofauti katika mwili na moyo wake, ili aondolewe kwenye kipengele cha kuchezewa na kuachwa? Wapo wanaume kadhaa ninaowafahamu ambao maisha yao yamebadilika baada ya kuachana na wapenzi wao waliowapenda.

Hawana furaha tena, hawana uwezo wa kufanya kazi sawasawa, wameathirika kisaikolojia na kila kitu katika maisha yao kimeharibika! Tuwaiteje nao hawa? Si kwamba wamechezewa na kuachwa?

"Maisha yangu yamebadilika kaka Shaluwa, sina mbele wala nyuma, yule mwanamke nilikuwa nampenda sana, lakini ndiyo hivyo nimelazimika kuachana naye kwa sababu nimegundua ni msaliti.

"Siku zote nilikuwa namtegemea yeye, nilimwamini kwa kila hali, nikampa moyo wangu wote, lakini hakuridhika, akanisaliti. Nimedumu naye kwenye mapenzi kwa miaka minne, sikuwahi kumsaliti hata mara moja.

"Nimefanya naye mambo mengi sana, tulikuwa na mipango mikubwa sana katika maisha yetu, lakini kila kitu kimezimika. Kila mtu yupo kivyake, moyo wangu una simanzi sana.

"Siwezi kufanya kazi vizuri na hivi ninavyokuambia, nina barua mbili za onyo kutoka kwa bosi wangu, akinitaka nibadilike. Nashindwa kumweleza ukweli wa mabadiliko yangu kikazi, maana atanifukuza.

"Sina la kufanya, muda wote namuwaza Betty mwanamke ambaye niliamini angekuwa wangu wa milele, kumbe nilikuwa najidanganya," alisema Moses, ambaye alifika ofisi kwangu wiki iliyopita kwa ajili ya ushauri.

Moses ni mfanyakazi katika kampuni moja jijini Dar es Salaam. Alikuja kuniomba ushauri baada ya kuachana na mpenzi wake miezi miwili iliyopita. Baada ya tukio hilo, ambalo kimsingi ni yeye aliyeliamua, hivi sasa anaishi maisha ya wasiwasi, akitumia muda mwingi kufikiria jinsi alivyokuwa akiishi na mpenzi wake huyo.

Kwa hakika alikuwa katika hali mbaya sana, nikapata wasaa wa kuzungumza naye kwa muda mrefu sana. Aliondoka akiwa na mahali pa kuanzia, nikiwa na maana kwamba, tatizo lake linahitaji muda, hupona taratibu kulingana na masharti niliyompatia wakati nikimshauri.

Hapo ndipo mada hii ilipozaliwa. Umejifunza nini kupitia Moses? Kwamba hata wanaume nao huteswa, huteseka na hushindwa kufanya mambo mengine, pindi wanapochukua uamuzi mgumu wa kuachana na wale ambao wanawapenda kwa dhati.

HISIA

Rafiki zangu, naomba niwatoe mchanga machoni kuwa, hisia za mapenzi ni zile zile. Haina maana kwamba, mwanamke ana uwezo wa kupenda sana kuliko mwanaume, la hasha! Kikubwa ni hisia kuwa za kweli.

Kwamba mwanamke kama atakuwa hajampenda mwanaume kwa dhati, kadhalika na mwanaume naye akiwa hajampenda mwanamke kwa dhati, itabaki kuwa hivyo, lakini kama wote watakuwa na mapenzi ya kweli, hali hiyo itaendelea kuwa hivyo kwa wote.

KUWEKEZA MAPENZI

Kama ulikuwa hujui, anza sasa kuingiza jambo hili kichwani mwako, kama wafanyabiashara wanavyowekeza katika sehemu mbalimbali, ndivyo ilivyo pia katika mapenzi. Mwanaume kama alivyo mwanamke, akipenda kwa dhati huhifadhi moyo wake kwa mwanamke huyo.

Mapenzi ni kuwekeza na ukishafanya hivyo, inakuwa vigumu sana kuuondoa moyo wako. Hapo sasa ndipo yanapokuja maumivu na dhana ya kuchezewa na kuachwa! Rafiki zangu, natamani sana kuendelea, lakini nafasi yangu ni ndogo. Wiki ijayo nitamalizia sehemu iliyosalia. Nawapenda sana!

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Let's Talk About Love vilivyopo mitaani. Unaweza kumtembelea kwenye mtandao wake; www.shaluwanew.blogspot.com au jiunge naye kwenye facebook.

Chanzo: Si wanawake tu, hata wanaume nao huchezewa na kuachwa! - Global Publishers
 
Hivi kwenye mahusiano inatangulia ndoa au upendo na compartibility kati ya wahusika? Mnaweza kuanza mahusiano tu, mkajikuta mmeendana kiasi cha kuanza fikiria kuoana au mnaweza anza mahusiano, mkakuta hamwezi kaa pamoja.
kinachotangulia kwanza ni upendo then ndoa kama mtaridhiana
 
@Mwali
Sitasahau ku-acknowledge source.

Kwenye kuchezea mwili, mie nadhani ni wote wanachezeana, au huwa mmoja anatulia tu mwingine achezee?

Pia Alhamis hii iliyopita, kuna mdada mke wa mtu alikuwa analalamika hawala yake anamtumia, nikamwambia kwa umri wako hutakiwi kulalamika hivi hadharani, ni aibu, wewe ni mtu mzima unajua unalofanya.

Je hata nyumba ndogo ya kike au ya kiume inachezewa/tumiwa???
 
@Mwali

Kwenye kuchezea mwili, mie nadhani ni wote wanachezeana, au huwa mmoja anatulia tu mwingine achezee?
Mmoja anatoa kwa kusubiri malipo (reward)
wakati mwengine anaji-enjoy full time.
Ikiwa ni mapenzi ya kweli na wote wana-enjoy,
huwezi sikia msichana akilalamika kua alichezewa
 
Mara nyingi mgogoro unakujaga unapomtoa bikra binti then baadae unakula kona kwenda kumtoa mwingine...
Huko nyuma ndo hayo maneno hufuata....
 
Mmoja anatoa kwa kusubiri malipo (reward)
wakati mwengine anaji-enjoy full time.
Ikiwa ni mapenzi ya kweli na wote wana-enjoy,
huwezi sikia msichana akilalamika kua alichezewa
Kimwili wote wanafurahia sana tu...ila km hakuna future ndo mmoja anakuwa kachezewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom