Ungepata fursa ya kuongea na Rais wa nchi,kwa niaba yetu ungemweleza nini?

J.K.Rayhope

JF-Expert Member
Oct 26, 2011
316
31
Wanajamii forum wenzangu,najua kila mmoja wetu ana mtazamo wake.Tuweke itikadai zote pembeni,bado utabaki MTZ na mzalendo.Sasa,imetokea kama bahati Uso kwa Uso na Rais.Labda tu amekuita au amekuchukua njiani baada ya kuona unanyeshewa mvua,ndio mmekaa pale White house mnapata kahawa ya Maziwa ktk kuondoa baridi.Pengine yakaja maswali kwako,mf.Watu wanauzungumziaje uongozi wangu? Au,Una ushauri/maoni gani kuhusu Uongozi wangu?.Na mengine ambayo Mkuu huyo angeona yanafaa.JE WEWE UNGEMSAIDIAJE KIONGOZI WAKO HUYU KWA NIA NJEMA KABISA?Naomba kuwasilisha WanaJF
 
Kama ni MUSEVENI ningemshauri aanzishe utaratibu mzuri wa kuwakopesha wanafunzi wa elim ya juu kama ilivyo tz.Kama ni KIKWETE ningemshauri aendelee kusimamia sheria bila kuangalia ubunge n.k.na kama mtu anataka kuwa juu ya sheria apelekwe gerezani akany.e nd.o
 
1. Elimu: Ningemweleza mheshimiwa rais kuhusu kero wanayopata watoto maskini wanaosoma katika shule za kata zisizokuwa na walimu, vitabu, maabara pamoja na miundo mbinu mibovu kufanya maamuzi magumu kwa kuhakikisha vijana wote walio vyuo vikuu kusaidia kazi ya kuwafundisha hawa watoto wakati wanapokuwa likizo. Vifaa vya maabara, ningemkumbusha ahadi yake ya kujenga kiwanda haraka cha kutengeneza hivyo vifaa ili kukidhi mahitaji yaliyo mhimu zaidi. Na jambo jingine ni vyuo vikuu kutunga sheria kuwa wawekezaji wote kwenye sekta ya madini kuhakikisha wanajenga vyuo vikuuu katika mikoa waliyowekeza (angalau kimoja katika kipindi cha miaka 3). Na vyuo vikuu vyote vya sayansi kuhakikisha vinapata fedha vya kutosha kwa ajili ya kufanya tafiti na matokeo yake kuisaidia jamii tofauti na hapo, mtu jela.

Pamoja na kutumia technolojia ya habari kuwasaidia wanafunzi wasiokuwa na waalimu mfano kuwepo na television ya elimu 24hours a day, 7days a week masomo yote yawe yanafundishwa kupitia TV na kila shule za kata iwe na miundo mbinu ya TVs kwa ajili ya kunasa hivi vipindi.

2. Umeme: Shirika hili la umeme liachwe lijiendeshe, na kama kuna makampuni au mashirika mengine basi yapewe rungu la kupambana na tanesco ili kuboresha huduma ya nishati hiyo kwa wananchi. Pamoja na kuwekeza kwenye umeme-jua, upepo (zanzibar wana upepo wa kutosha kabisa). Na pengine ningemshawishi aangalie namna ya kuboresha huduma ya umeme vijijini.


Ni mengi, muda wangu umenitupa mkono.
 
Ningemwambia hivi ulipoapa kwamba utayalinda na kuyatetea maslahi ya Tanzania na Watanzania ulikuwa unafikiri kitu gani kichwani mwako? Je tangu uingie madarakani miaka sita iliyopita ni mara ngapi umeyatetea na kuyalinda maslahi ya Tanzania na Watanzania? Nakuomba ujiuzulu haraka sana ili kuiepusha Tanzania katika janga kubwa la kuwa na Rais kama wewe ambaye hajui atendalo kama Rais wa nchi.
 
Nitamwambia yafuatayo,
1. KATIBA YA NCHI haijatoa nafasi kwa Mke wake kuzunguka nchi nzima kukagua shughuli za kimaendeleo akitumia KODI ZA WANANCHI, kwani familia yake si sehemu ya watendaji wa serikali. Hivyo, amkataze mke wake mara moja mke wake kutumia kodi zetu.
2. Nchi inaelekea kubaya sana kwasababu ya uongozi wake na watendaji anaowateua kama mawaziri, wabunge wa kuteuliwa, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi mbalimbali, n.k. kwani mara nyingi ueuzi wake haujaangalia UWEZO WA MTU bali umelenga JINSIA, UDINI, FAMILIA, NA URAFIKI.
3. Ningemwomba awajibike katika serikali yake kwa kupunguza yafuatayo; safari nje ya nchi, kutokuwa serious na mambo ya msingi, n.k
4. NITAMWOMBA AJIUZULU ILI UCHAGUZI UFANYIKE UPYA, kwani hata yeye naamini anatamani sana kupumnzika kwasababu hawazi na ameshindwa kuleta mabadiliko yoyote ya maana katika uchumi wa Tanzania na badala yake amezidi kutuweka pabaya hasa kiuchumi na kimahusiano kama Watanzania kwa kupandikiza CHUKI ZA UDINI.
5. Mwisho nitamwambia kuongoza nchi si suala la majaribio. Inahitaji watu wenye VISION, kitu ambacho hana na hawezi kuwa nayo sasa; hivyo ni vizuri aachie madaraka, kwani SI TU AMESHINDWA KUONGOZA NCHI, BALI HATA CHAMA-CCM NDIYO MAANA MIGOGORO KILA KUKUICHA. Yote hii ni dalili za kushindwa.

NB: Nitamshauri, akafanye shughuli aliyokuwa/anayoimudu anaimudu zaidi akifanya tathmini yeye mwenyewe.
Ahsante.
 
Ningemuuliza yeye kama raisi anachukuliaje thamani ya ela (shiling) kuporomoka kila kukicha?
 
ningemwambia..IKULU NI MAHALI PATAKATIFU,KIKWETE HUKUCHAGULIWA NA WANANCHI WA TANZANIA KWENDA KUPA GEUZA KUA PANGO LA RIZONE........
 
Ningempa za macho tu, kuwa huku kitaa machizi hawakumaindi kivile sana
Kwamba mshua maisha hayaeleweki we unakula pipa deilee
Kwamba Rais, mambo mengi ya kitaa umegonga kimya sana
Kwamba wananchi kitaa wanataka kusikia kauli yako kuhusu Dowaniz, kushuka kwa madafu na kazalika
Kwamba kitaa wanaona unawazingua tu, unaogopa kuwafukuza watendaji wabovu unawachekea tu, hasa bwa umeme
Kwamba mkulu huku kitaa kimenuka, wanaona kila mtu kwenye gavamenti yako ni mropokaji kaa bar hakuna dispilin kivile sana
 
Ningejikuta nabubujikwa machozi and after 5min NINGEJIKUTA NIMEMUWASHA KIBAO RAIS WANGU PASIPOKUKUSUDIA,BAADA YA HAPO NINGEMWAMBIA ATUBU MBELE ZA MUNGU WAKE KWA 5MIN THEN AWAITE VYOMBO VYA HABARI KISHA ATUBU NAKUWAOMBA RADHI WATANZANIA WOTE. VILE TULIMTEGEMEA NAKILE AMEKIFANYA ANAPASWA HUKUMU PASIPO MASHITAKA,WATU WANAITAFUNA NCHI NAKUIMALIZA KWA MIKATABA MIBOVU ILA YEYE ANATABASAMU. Hakika Rais wangu umewaongopea wa tanzania nanina hakika b4 2015 kunatukio litatokea ambalo litaitikisa ikulu na nchi kwa ujumla. Ikiwa Rais wangu unasoma makala hii juwa nilazima ujivuwe gamba kwakuwatundika mahakaman watu walio tufikisha hapa no way lazima ukumu ipite na kama utawahurumia MUNGU HATOKUURUMIA WEWE WALA WATU WA NYUMBAN KWAKO WALA WASHAURI WAKO ATAHUKUMU AND YOU NAME WL NEVER EVER BE REM KTK HISTORIA.
 
Ningemuuliza kama anakumbuka ahadi alizotoa wakati wa uchaguzi na kama anakumbuka gharama za kuzitekereza ahadi zile
 
ningemwambia achague sehem za kucheka cheka, sio hata kwenye misiba ye anacheka tu...afu ajitahidi kupunguza kigugumizi na kurusha mikono kila anapoongea kingereza bila kusoma mahala, cha mwisho, ningemrudisha kidato cha kwanza akajifunze elimu ya uraia...
 

Ningemweleza jinsi alivyotumainisha watz na jinsi alivyowadissapoint. Ningemtaka ajiuzulu kwani watz hatuna imani naye wala chama chake kwa sababu ya uongozi wake mbovu na kukosa kwake priorities na , kuangusha uchumi, kuwa mwongi kupitiliza, kuonea aibu marafiki zake mafisadi, kuifanya ikulu ni ya salma na ridhiwani, kushindwa kwake kuchukua hatua yoyote kwa watendaji wake, safari zake za nje zinakotupeleka na kwa kuwa ameshindwa, waingereza wameamua kumtupia kila aina ya misaada kwa sharti la kutopiga vita ushoga...kiujumla huenda ningemtemea mate kwa kushindwa kwake kuwa na soni hata kidogo hasa pale anapobofoa
 
Ningemweleza jinsi alivyotumainisha watz na jinsi alivyowadissapoint. Ningemtaka ajiuzulu kwani watz hatuna imani naye wala chama chake kwa sababu ya uongozi wake mbovu na kukosa kwake priorities na , kuangusha uchumi, kuwa mwongi kupitiliza, kuonea aibu marafiki zake mafisadi, kuifanya ikulu ni ya salma na ridhiwani, kushindwa kwake kuchukua hatua yoyote kwa watendaji wake, safari zake za nje zinakotupeleka na kwa kuwa ameshindwa, waingereza wameamua kumtupia kila aina ya misaada kwa sharti la kutopiga vita ushoga...kiujumla huenda ningemtemea mate kwa kushindwa kwake kuwa na soni hata kidogo hasa pale anapobofoa

Simpendi mwongo huyu!!!!?
 
Back
Top Bottom