Ungekuwa wewe ungemfanya nini mlevi huyu?

Jamaa alikuwa amelaa na mkewe. Saa tisa ya usiku wakaamshwa na mtu akipiga hodi mlangoni kwao. Wakabishana nani akafungue, hatimae mume akiwa usingizini kaenda na kufungua mlango.

Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao:

MUME: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.

Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia,
MLEVI: Okay nisukume basi..


hapo lazma achezee kchapo had akili ikae sawa!
 
Ningefurahi kwakua amenipunguzia kazi maana nibora kumsukuma mtu alie kwenye bembea kuliko alie kwenye gali. kazi rahis kuliko nilivyo fikiria.
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom