Ungekuwa wewe ungemfanya nini mlevi huyu?

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
8,315
7,731
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe. Saa tisa ya usiku wakaamshwa na mtu akipiga hodi mlangoni kwao. Wakabishana nani akafungue, hatimae mume akiwa usingizini kaenda na kufungua mlango.

Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao:

MUME: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.

Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia,
MLEVI: Okay nisukume basi..

 
namwambia subiri, naenda kumuita wife, namwambia haya msukume... me narudi zangu kulala
 
ningemsukuma ili kwa kila hali wakati anarudi agonge mti kwa nyuma ..! lazima pombe ingeisha tu..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom