Ungekuwa wewe ndo Mume unge.....

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Jamaa karudi home usiku wa manane.Moja kwa moja akazama chumbani,akafunua blanketi,akaiona miguu minne badala ya miwili aliyozoea.Jamaa akafunika blanketi taaratibu,akachukua bonge la rungu,akaitwanga ile miguu kwa nguvu zote halafu akaelekea sebuleni kutuliza hasira.Kutahamaki akamkuta mkewe amejipumzisha sebuleni.Mkewe akamwambia:Wazazi wako wamekuja leo kututembelea,nimewaachia chumba chetu walale,sisi tutafanya maarifa mengine!
 
Mkuu heri usingizie hujaona watu ila ulimwona nyoka juu ya kitanda
 
nimewaachia chumba chetu walale,sisi tutafanya maarifa mengine!

Kwa desturi zetu za kiafrika ni aibu wakwe kulala kitanda ambacho watoto wao hujipumzisha.

Anyway, nita apologise lakini watakuwa wamepata funzo pia.
 
Kwa desturi zetu za kiafrika ni aibu wakwe kulala kitanda ambacho watoto wao hujipumzisha.

Anyway, nita apologise lakini watakuwa wamepata funzo pia.
Kuhusu maadili ni kweli mkuu but we are just joking?
 
ntarudi kuwaomba msamaha na kuwambia ukweli kua nlikua na dhanna. Lkn na ya huyo mume nae labda alikua chopy, ndo haijui ht miguu ya mkewe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom