Ungefanyaje kama ndio umeambiwa wewe?

VISIONEER

Senior Member
Apr 29, 2011
141
20
Habari ya kwenu wana jf.
Mimi nina rafiki ambaye ni jinsia ya kike alikuja kuniomba ushauri afanyeje anasema kuwa ametokea kumpenda kijana ambaye ni wa mtaani kwao,anasema anampenda kwa dhati na ana malengo ya ndoa pia ikiwa wataelewana, lakini utata upo hapa yeye ni mtoto wa kike na kwa taratibu zetu au sijui mila za mtanzania mwanaume mpaka amtokee mwanamke kwanza,sasa yeye anasema anaogopa kumwambia kwasababu hizo na asije onekana labda malaya.

Mwanamke ana miaka 31,anaishi maisha ya wastani, anafanya kazi na ana kipato cha wastani kilichomwezesha kujenga nyumba moja na ana gari ya kutembelea moja.

Lakini yeye anasema anabahati mbaya kuwa kila mwanamme anayemtaka kumuoa hampendi, ila anaowapenda hawampendi. Na akiangalia umri unazidi kwenda mbele sasa afanyeje amwambie huyo kijana na je ni hali ya kawaida kwa watanzania au ataonekana malaya?

Tunaomba msaada kwa hili wanaume wa tanzania mnalichukuliaje? Kama ndio wewe mwanamke anakutokea kwa malengo mazuri utamchukuliaje.

Msaada plse!
 
but nadhani girls wanambinu nyingi za kuwatega wanaume,ingawa hawawezi kusema direct but kuna ishara,kwahiyo awe na ujuzi wa kumteka kwanza huyo mwanaume anayemtaka kimawazo na ataona anapendwa.
 
Tatizo lipo kwa mwanaume anaweza akafuatwa direct then yeye akajua binti hajatulia ila kama wewe unamfahamu vyema huyo kijana na vizuri kupanga kukaa mahali alafu binti anakuja kwa staili fulani na bila kuonyesha dalili na hii itasaidia mawasiliano kujengengeka katika hali ya kawaida kabisa
 
ushauri umetulia nashukuru mkuu kwa mchango wako.

Tatizo lipo kwa mwanaume anaweza akafuatwa direct then yeye akajua binti hajatulia ila kama wewe unamfahamu vyema huyo kijana na vizuri kupanga kukaa mahali alafu binti anakuja kwa staili fulani na bila kuonyesha dalili na hii itasaidia mawasiliano kujengengeka katika hali ya kawaida kabisa
 
Habari ya kwenu wana jf.
Mimi nina rafiki ambaye ni jinsia ya kike alikuja kuniomba ushauri afanyeje anasema kuwa ametokea kumpenda kijana ambaye ni wa mtaani kwao,anasema anampenda kwa dhati na ana malengo ya ndoa pia ikiwa wataelewana, lakini utata upo hapa yeye ni mtoto wa kike na kwa taratibu zetu au sijui mila za mtanzania mwanaume mpaka amtokee mwanamke kwanza,sasa yeye anasema anaogopa kumwambia kwasababu hizo na asije onekana labda malaya.

Mwanamke ana miaka 31,anaishi maisha ya wastani, anafanya kazi na ana kipato cha wastani kilichomwezesha kujenga nyumba moja na ana gari ya kutembelea moja.

Lakini yeye anasema anabahati mbaya kuwa kila mwanamme anayemtaka kumuoa hampendi, ila anaowapenda hawampendi. Na akiangalia umri unazidi kwenda mbele sasa afanyeje amwambie huyo kijana na je ni hali ya kawaida kwa watanzania au ataonekana malaya?

Tunaomba msaada kwa hili wanaume wa tanzania mnalichukuliaje? Kama ndio wewe mwanamke anakutokea kwa malengo mazuri utamchukuliaje.

Msaada plse!

Kwa kawaida mwanamke ndie anayemuanza mwanaume. Mwanaume hatamwa-approach mwanamke kama amemgeuzia mgongo. nafikiri umenielewa. Mwanaume anafanya move pale anapoana signal ya "you may come". No signal, no move. Halafu hapo kwenye red, mwambie apunguze speed kwanza asije akaishia pabaya. Hapo kwenye blue naye awe tayari kwa hilo. Kwa vile "anampenda" huyo mwanaume, kuna uwezekano pia huyo mwanaume hampendi. Lolote linaweza kutokea. Kama wanaishi mtaa mmoja inawezekana jamaa ameshamwona huyo rafiki yako mara nyingi tuu lakini labda sio size yake? Pia mshauri awe anacheki cheki na mtaa wa pili pia, you never know. Pia wanaume we're flattered tunapotongozwa pia. Wanaishi mtaa mmoja, ana gari na hajawi kumpa hata lift?
 
Ila asizidishe mitego otherwise mshkaji anaweza akamuona malaya au mshkaji asije akategeka kwasababu demu anazo kiasi fulani,si unajua wengi wetu tunapenda kulelewa siku hizi.aoneshe interest kiutuuzima au ikiwezekana waunganishe wawe marafiki wa kawaida kwanza,am sure kama jamaa ana interest na huyo demu atamtokea mwenyewe
 
Ebu tuachane na fikra za zamani eti mwanamke atongozi!, kwanini asitongoze ikiwa tuna preach haki sawa kijinsia? nenda kamwambie hisia zako kwake kama atakuchukulia tofauti he was meant not to be yours acahana naye songa mbele kupenda hakuishi utapata mwingine utakeyempenda akakupenda pia.
 
Unajua wanawake wengi wangeweza kuwatokea wanaume lakini nadhani wanahofu ile ya kutangazwa kwa mamen wengine na pia wasijeonekana malaya.

Ila hili suala la mwanamme atongoze kwanza linawanyima haki wanawake mi nadhani sasa tubadilike tukubaliane kuwa hata wanawake wanahisia pia.
 
[CODE]Lakini yeye anasema anabahati mbaya kuwa kila mwanamme anayemtaka kumuoa hampendi, ila anaowapenda hawampendi. Na akiangalia umri unazidi kwenda mbele sasa afanyeje amwambie huyo kijana na je ni hali ya kawaida kwa watanzania au ataonekana malaya?[/CODE]

Jibu ni kwenye rangi nyekundu...................ya kuwa kila mwanaumme aliyemtaka hakumpenda yeye sasa ni lipi litufaye kufikiria njemba hii itakuwa tofauti?
 
NI kama ilivyo wewe si kila mwanamke ungependa awe mpenzi wako ndio maana kuna baadhi tu ndio unawatokea sio? sasa na kwa wanawake hivyohivyo si kila mwanamme anayemtokea anataka awe mpenzi wake.

na ukweli hili tatizo limewakuta wanawake wengi na kufikia hatua wanaolewa kwasababu umri umekwenda lakini hawajawapenda wanaume wao. Jaribu kutafuta rafiki yako wa kike muulize hivi ni kweli kuna wanawake wanaolewa na wanaume wasiowapenda? akiwa mkweli atakuambia

[CODE]Lakini yeye anasema anabahati mbaya kuwa kila mwanamme anayemtaka kumuoa hampendi, ila anaowapenda hawampendi. Na akiangalia umri unazidi kwenda mbele sasa afanyeje amwambie huyo kijana na je ni hali ya kawaida kwa watanzania au ataonekana malaya?[/CODE]

Jibu ni kwenye rangi nyekundu...................ya kuwa kila mwanaumme aliyemtaka hakumpenda yeye sasa ni lipi litufaye kufikiria njemba hii itakuwa tofauti?
 
Kama anafahamu uelewa wa huyo kijana mimi namshauri amfuate akae nae chini amueleze hisia zake!Sipendi kukubaliana na hii hoja kwamba mwanamke akieleza hisia zake kwa mwanaume basi ataonekana malaya!Lakini awe tayari kukubaliana na matokeo kwani si kila umpendae nae atakupenda kama alivyosema yeye kua kuna wanaume waliompenda ila yeye hakuapenda!
 
Tatizo letu wanadamu ni kuwa huwa tunajipangia matokeo ya jambo fulani na kuyaogopa hayo matokeo kama vile ni kitu halisi,kumbe ni mawazo yetu tu,mwambie aende akamwambie huyo kijana suala kuwa ataonwaje sio lake ni la huyo kijana hata kama atamuona malaya ni ujinga wa huyo kijana,mwambie atumie nafasi iliyopo vizuri asije kijana akaondoka akabaki akijilaumu,mwanamke kumpenda kma nkisha kumwambia sio aibu ni ushujaa mkubwa wala sio dhambi,mwambie ajiamini
 
31 ni mtu mzima mbona,na najua watu wazima wanaelewa vizuri haya masuala ya mahusiano,hawez kukuita malaya kisa umemtongoza,labda kama zamani ulikuwa malaya kweli.mwanaume akikuchunguza na kujua upo clean na kakupenda,atakukubali tu.ndoa asiwaze kabisa mapema,wachunguzane kwanza.kama aliweza pata gari na nyumba yake binafsi,hawez shindwa kupata mume wa ukweli.
 
Kama alichotaka ni ushauri nadhani hayo maneno yanatosha Mkuu! Kule Nigeria wanasema "You have spoken well".

Kwa kawaida mwanamke ndie anayemuanza mwanaume. Mwanaume hatamwa-approach mwanamke kama amemgeuzia mgongo. nafikiri umenielewa. Mwanaume anafanya move pale anapoana signal ya "you may come". No signal, no move. Halafu hapo kwenye red, mwambie apunguze speed kwanza asije akaishia pabaya. Hapo kwenye blue naye awe tayari kwa hilo. Kwa vile "anampenda" huyo mwanaume, kuna uwezekano pia huyo mwanaume hampendi. Lolote linaweza kutokea. Kama wanaishi mtaa mmoja inawezekana jamaa ameshamwona huyo rafiki yako mara nyingi tuu lakini labda sio size yake? Pia mshauri awe anacheki cheki na mtaa wa pili pia, you never know. Pia wanaume we're flattered tunapotongozwa pia. Wanaishi mtaa mmoja, ana gari na hajawi kumpa hata lift?
 
mmmmmmh pole cna bt unajua dunia imebadilika w2 wte naw daiz wana haki ya kupenda na kupendwa ,, lakini kuna kitu kimoja napenda nijue je unajua kama unampenda?
 
Habari ya kwenu wana jf.

Mwanamke ana miaka 31,anaishi maisha ya wastani, anafanya kazi na ana kipato cha wastani kilichomwezesha kujenga nyumba moja na ana gari ya kutembelea moja.

Kwa ukweli wa maisha ya mtanzania huyo mwanamke ni matawi ya juu. Naona umejaribu kushusha uhalisia, lakini kimtazamo huyo mwanamke ni ana hela na kwa sisi uswahili yeye ni tajiri..ana gari, na ana nyumba, kwa miaka 31 tu..

Huenda maisha yake ndio yanayowafanya wanaume wajiulize mara mbili mbili...Inawezekana anaonekana kama 'mmarekani' fulani hivi..na unakuta ofisini au mtaani anapokaa, kuna wanaume wenye maisha ya kawaida..

Aanze kujichanganya sehemu zenye watu wa status yake..
 
hahahaha umenifurahisha mkuu,yawezekana kweli anaonekana tajiri fulani hivi

Kwa ukweli wa maisha ya mtanzania huyo mwanamke ni matawi ya juu. Naona umejaribu kushusha uhalisia, lakini kimtazamo huyo mwanamke ni ana hela na kwa sisi uswahili yeye ni tajiri..ana gari, na ana nyumba, kwa miaka 31 tu..

Huenda maisha yake ndio yanayowafanya wanaume wajiulize mara mbili mbili...Inawezekana anaonekana kama 'mmarekani' fulani hivi..na unakuta ofisini au mtaani anapokaa, kuna wanaume wenye maisha ya kawaida..

Aanze kujichanganya sehemu zenye watu wa status yake..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom