Ungefanya nini ukiwa Rais wa Tanzania kwa mwezi mmoja?

Moony

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,599
435
Kila mmoja wetu nadhani kwa njia moja ama nyingine ameguswa na matukio ya kila aina yanayotokea hapa nchini. Watu wengi wamekuwa wakirusha lawama za kila aina kwa mh. JK.
Sasa inawezekana kabisa hapo alipo amezidiwa na hajui afanye nini kwani aidha washauri wake wakuu wanamuangusha ama hawasikilizi au inawezekana pia, wote hawana mikakati yoyote. Inawezekana kabisa wanaona nchi inavyokwenda ni sahihi kabisa.
Sasa je mwana JF, ungefanya nini katika kipindi cha mwezi mmoja tu ambacho ungejaliwa kuwa RAIS wa nchi hii?

Only constructive suggestions and opinions are needed na wala si utani na matusi kwani tunakusanya maoni tuyafanyie
kazi.

KARIBUNI KUCHANGIA.
:welcome:
 
Ziara yangu ya kwanza ingekua kutembelea DEAD SEA kuona na kuhakikisha kama kweli hakuna kiumbe anaeishi humo. Mambo ya kusimuliwa ni wakati ule nikiwa UVCCM na sikupata muda wakati nilipokua waziri wa mambo ya NJE.

Polepole mtanielewa tu!
 
Ningemnyonga padre Wilbrod Peter Slaa, tena pale Mnazimoja na ningefanya siku hiyo iwe ya mapumziko ili watu washuhudie kitendo hiki kwenye TV wakiwa majumbani kwao.
 
Ningemnyonga padre Wilbrod Peter Slaa, tena pale Mnazimoja na ningefanya siku hiyo iwe ya mapumziko ili watu washuhudie kitendo hiki kwenye TV wakiwa majumbani kwao.

UNGEFANYA HIVI KAMA RAIS WETU WA JAMHURI YA MUUNGANO?????:sad::sad:
 
Dah utakuwa rais wa aina yake ,hatuhitaji rais km wewe maana hata ukimnyonga huyo bwana bado matatizo ya watanzania yataongezeka, ningekuwa mimi ningefumua jeshi la polisi na hao ntakaowqchagua nitawapeleka shule wajue nini maana ya democrasia,nitasimamia uchumi kwa kuondoa misamaa ya kodi kwa wawekezaji,nitaagiza waliotunza fedha uswis wakamatwe mara moja, nitavunja baraza la mawaziri la wakereketwa na kuunda baraza la uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kulipunguza ukubwa wake , pia nitafungua mjadala wa namna watanzania wanavyotaka kuongozwa
 
Ningemwagiza mara moja msajili wa vyama vya siasa bila kupoteza muda akifutilie mbali cha CDM.
 
Kwa kuwa muda wa mwezi mmoja ni mfupi mno, ningerekebisha mfumo mzima wa utawala kwa kuufanya uwe wa kiuwajibikaji kwa wananchi zaidi, na kwa ujumla ningefanya yafuatayo:

1. Kwa sababu tuna tatizo kwenye usalama wa raia, ningesuka upya taasisi zinazohusika. Issue current kama ya Mwangosi, ningeagiza IGP awasimamishe kazi RPC na vijana wake woote waliokuwa Nyololo: wawekwe ndani hadi uchunguzi utakapokamilika, na baadaye ningemfukuza kazi yeye mwenyewe kama hatajiuzulu.
2. Ningehamasisha watu watoe maoni yao kwenye mchakato wa katiba, na kuwaelewesha umuhimu wake, na kwamba wajifunze udhaifu wa katiba iliyopo ili makosa hayo yaepukwe kwenye katiba ijayo.
3. Ningewawajibisha viongozi wote ambao maeneo yao ya kazi yanatuhumiwa kwa kutoyashughulikia matatizo
4. Magari yote ya serikali yanayozidi cc 3000 ningeyauza, na kununua yenye uzito mdogo wa injini kupunguza matumizi
5. Ningepandisha viwango vya mrahaba na kodi stahili kwa migodi
6. Ningeagiza teknolojia ya kilimo, ufugaji na umwagiliaji toka Israeli. Kila Halmashauri ingeagizwa kuwa na mfumo huu: mashamba ya vijiji na ukulima wa kisasa wenye kuzingatia vigezo vyote. Pembejeo zingepwea ruzuku kwa kuzingatia mapato yanayotokana na migodi.....na kutakuwa na utaratibu wa kutenga muda wa watu kutumikia mashamba yao kwanza, halafu ya ushirika, hii itasaidia kuwa na usalama wa chakula na kuweza kuuza nje. Pia kutakuwa na kilimo cha kibiashara cha matunda na mboga kwa ajili ya soko la ndani na nje...
7. Ningerejesha nyumba za Serikali, ili watumishi wa umma wanaostahili waendelee kuishi prime areas. Ningeanzisha mchakato wa kujenga nyingine pia.

8.Magareza (Wafungwa) yatatumika kwa uzalishaji mali, kama mashamba na shughuli za umma

9.Nitaanzisha taasisi mpya ya uchunguzi wa makosa makubwa (Serious Fraud), ndogo, yenye wataalam wa hali ya juu watakaolipwa vizuri, itakayofanana na iliyokuwa The Scorpions ya Afrika Kusini ambayo itakuwa inajitegemea (Autonomous)

10. Nitaweka mfumo mzuri wa kuanzisha kampuni ya taifa ya gesi, ambayo itawauzia hisa wananchi na taasisi zingine za umma ili kuwa na umuliki mpana.

11. Nitaivunja Tanesco na kutenganisha kampuni ya kuzalisha umeme, na nyingine ya kusambaza umeme kuongeza ufanisi.

12. Wakuu wa taasisi zote za umma na bodi zote watakuwa wanaomba kazi, na kufanyiwa usaili na makampuni kama Deloitte.

Muda wa siku 30 utakuwa unaishia ishia mkuu...
 
Ningekuwa mimi ningeenda USA kuhuzulia msiba wa mwigizaji Michael Duncan pamoja na kupiga picha na wasanii wakubwa watakaohuzulia msiba huo.
 
Kila mmoja wetu nadhani kwa njia moja ama nyingine ameguswa na matukio ya kila aina yanayotokea hapa nchini. Watu wengi wamekuwa wakirusha lawama za kila aina kwa mh. JK.
Sasa inawezekana kabisa hapo alipo amezidiwa na hajui afanye nini kwani aidha washauri wake wakuu wanamuangusha ama hawasikilizi au inawezekana pia, wote hawana mikakati yoyote. Inawezekana kabisa wanaona nchi inavyokwenda ni sahihi kabisa.
Sasa je mwana JF, ungefanya nini katika kipindi cha mwezi mmoja tu ambacho ungejaliwa kuwa RAIS wa nchi hii?

Only constructive suggestions and opinions are needed na wala si utani na matusi kwani tunakusanya maoni tuyafanyie
kazi.

KARIBUNI KUCHANGIA.
:welcome:

Unatupima akili zetu au,
1. Hakuna RAISI WA MWEZI SEPTEMBER
2. UNAKIUKA IBARA YA KATIBA YA NCHI HII KWA KUTANGAZIA UMMA RAISI WA MWEZI MMOJA.
3. UNADHARILISHA NCHI MAANA RAISI UCHAGULIWA NA WANANCHIA
4. KIPINDI CHA URAISI NI MIAKA 5
6. MODERATOR CONTROL THREAD
 
Alaa kumbe?
 
Back
Top Bottom