Ungamo la kishetani!!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Can this be really? To me, ni ungamo la kiibirisi!!



KAMA WEWE NDIO MUMEO UNAFANYAJE??
Mke wangu mpendwa!
Nimekuwa nikiandamwa na msongo wa mawazo siku za karibuni kwa kuwa sasa nadhani nimefikia mwisho sina budi kukueleza aina ya mume uliyekubali kuwa naye hadi mungu atakapo tutenganisha. Najua wewe ni mpole na mvumilivu lakini ninayokwenda kuyasema ni mazito sana kwa moyo wa mwanadamu hivyo usinionee huruma kwa uamuzi utakao uchukua kwani tayari nimeukubali kabla sijaujua. Sijajua kosa ulilolifanya hadi kupewa adhabu ya mume kama mimi ila ninaamini aliyekuadhibu akiyasikia haya basi atakuandalia pepo yako mbinguni kwa kuwa umekwisha onja kiama hapa duniani, mke wangu:-

1. Yule mtoto wa shangazi yako ninayemsomesha sifanyi hayo kwa mapenzi yangu kwako bali ninaficha ubaya tunaokufanyia, nimekuwa na uhusiano usiofaa na binti huyu tangu alipovunja ungo, miaka nane iliyopita.
2. Msichana wa kazi uliyemfukuza kwa kuwa na ujauzito tukagombana sana na nilikuita majina yote mabaya ni kwa kuwa nilikuwa najaribu kumlinda kwa kuwa sikuwa na uhakika kama hiyo mimba hainihusu kwa kuwa nimetembea naye miezi ile miwili uliyokwenda mafunzo south africa.
3. Nyumba unayoisifia sana aliyopanga shoga yako Suzzy wa Sinza, ninalipia mimi kodi na nimekuwa na uhusiano wa siri na rafiki yako Suzzy tangu mkiwa pamoja chuo kikuu.
4. Ugomvi mara kwa mara ndani ya nyumba yetu mara zote huwa naupanga ili kuficha maovu yangu.
5. Mke wangu sijawaji kukumbuka birthday yako hata siku moja ila ninaambiwa na rafiki yako Suzzy.
6. Hata tabia ya kwenda Bar si kwa sababu ya kukutana na marafiki bali ni tabia yangu mbaya ya kupenda kuwashika shika makalio na matiti ma bar maid.
7. Kinachonipeleka salon kufanya scrub si usafi mke wangu bali ni tamaa ya kushikwa shikwa na kutekenywa na wasichana wadogo wa salon, hii ndio sababu mara zote unaponunu dawa za scrub nyumbani nazipoteza au nasingizia zinanitoa chunusi.
8. Mke wangu mimi sio shabiki kabisa wa mpira bali huwa nasingizia kupenda ili nilpate uhuru wa kutumia muda mwingi nje ya nyumbani.
9. Mke wangu yule personal trainer wa gym nilimuajiri pia kukuangalia, kukuchunguza na pia kukujaribu ili nipate visingizio vya kukuacha tangu miaka miwili iliyopita lakini sikufanikiwa na alichoniambia ndicho kimenifikisha kwenye ungamo hili.
10. Mke wangu pete yangu ya harusi haikupotea bali niliigawa kwa rafiki yako Suzzy
 
It can't be!
ndo pa kuparalaizi mwili na roho hapo....
 
duuuu aiseee hii kali lakini kwa kuwa alivumilia wakati hujaungama kwa nini asikuvumilie sasa!
TENA UTAZIDISHA UPENDO WAKE KWAKO!
 
Haya ndiyo yanayoendelea kwenye familia zetu nyingi sana, japo hapa tunafanya kama kushangaa!
Tena pengine tunafanya mazito zaid ya haya!
Imagine vitendo kama mfano abortion tunazofanya au kusaidia kuzifanya, kufukuzisha kazi wenzetu kwa makusudi, kugombanisha ndoa za marafiki etc!

Bora huyo jamaa ameamua kuweka hadharani aliyoyafanya, nadhani amedhamiria kuyaacha jumla.
Personally nachukulia hili kama ungamo la DHATI!
NAWASILISHA.
 
Lakini nahisi kuna maungamo mengi katika hayo yanatugusa wengi tu, lakini hatujakaa na kutafakari katika muelekeo wa maungamo
 
Asante PJ kwa kusema ukweli huwa siwaelewi binadamu utafikiri huwa kuna viumbe wanatoka sayari nyingine kuja kufanya huu ushetani .

Haya ndiyo yanayoendelea kwenye familia zetu nyingi sana, japo hapa tunafanya kama kushangaa!
Tena pengine tunafanya mazito zaid ya haya!
Imagine vitendo kama mfano abortion tunazofanya au kusaidia kuzifanya, kufukuzisha kazi wenzetu kwa makusudi, kugombanisha ndoa za marafiki etc!

Bora huyo jamaa ameamua kuweka hadharani aliyoyafanya, nadhani amedhamiria kuyaacha jumla.
Personally nachukulia hili kama ungamo la DHATI!
NAWASILISHA.
 
Huyo mume atakuwa na anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama... Kitombicssana ambao unasababishwa na vijidudu wajulikanao kitaalamu kama Nyegelundopacs. Ugonjwa huo unashambulia sana wanaume wenye umri na kipato cha kati na kipato cha juu. Hasa wale wenye elimu zao, nyumba zao, wake zao (tena wenye kazi/kipato) na pesa zao ndo zinawapa jeuri.
Kapuku ni nadra kuugua ugonjwa huu.

Dk. Mwendabure!
 
Dah mie naweza zimia we DC wewe dah ngoja kwanza nivute pumzi halafu nirudi kukwambia ningejibu
 
Back
Top Bottom