Unene na shinikizo la damu

vicent tibaijuka

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
268
57
Unene na shinikizo la damu
Katika dunia ya leo kuna janga kubwa la unene . Karibia - 30% ya watu ni wanene, si ila unene unaesabiwa bali ule wa mafuta mengi mwilini. Kwani kuna unene wa mazoezi kama wanyanyuwa vyuma hauhesabiwii. Unene - si tu ni kiasi cha mafuta kuzidi mwilini bali pia huleta matatizo mengine ambayo nitayataja hapo chini
Watu wengi hasa matajiri , hasa katika miji mikubwa ya nchi zilizoendelea huenda kufanya mazoezi katika sehemu mbalimbali ili kuweza kuepukana na tatizo hili , wakati watu wa nchi za dunia ya tatu wanakuwa ndio kwanza wanashabikia unene kama njia ya kuonyesha kuwa wana utajiri, bila ya kujali madhara ya mbeleni. Hii ina tokana bado na serikali zao kuto tilia mkazo shwara hili . mfano nzuri ni kwetu hapa Tanzania
Unene mara nyingi unazohusiana na magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, mashambulizi ya moyo, kiharusi, dyslipidemia, ai ugonjwa wa kisukari, gout, utasa, ovari lenye uvimbe, "vena thromboembolism Mabonge ya damu katika mishipa ya damu)", "apnea (matatizo ya usingizi)us" kansa, na mengineyo mengi. Uhusino wa mafuta na magonjwa ya moyo unajulikana kwa muda wa miaka mingi lakini serikali zetu zimekuwa hazifuatilii.
Ongezeko la unene kwa Wanaume na wanawake na mara nyingi huandamana na kuongezeka kwa shinikizo la damu, pamoja na uanzishaji wa activation of sympathic nerve, pingamizi la insulin mwilini (insulin resistant) na kusababisha kisukari, uharibifu wa mpangilio wa mafuta mwilini (dyslipidemia atherogenic). Mabadiliko haya huwa na maendeleo na upungufu wa estrogens, tezi homoni. Hivyo, Unene ni moja ya sababu mojawapo kuendeleza kukua kwa shinikizo la damu.
kuongezeka kwa uzito wa mwili (BMI) kutokana na uwiano mkubwa wa mafuta hasa ya tumboni (kitambi) ni sababu kubwa sana inayosababisha ya shinikizo la damu na kisukari. BMI ni uwiano kati yay a uzito na urfu katika mita.(kg/m2). BMI inatakiwa kuwa kati ya 18.5-24.9kg/m2. Zaidi yahapo mtu anahesabiwa kama mnene, na ikiwa zaidi ya 30kg/m2 inamaana huyu mtu tayari anahatari kupata magonjwa.
Mgawanyo wa mafuta ktk mwili wa binadamu umegawanyika katika semumu mbili kiume hasa tumboni (android) na kike katika makalio (glutein, pear like). Unene aina ya kiume ndio mara nyingi huambatana na ugonjwa wa kisukari , moyo, gout na shinikizo la damu hali hii ni hatari zaidi kama uwiano wa mzingo wa tumbo na paja kuwa mkubwa zaidi ya 0.9 ( yaani mzingo wa tumbo/mzingo wa paja >0.9). wastani wa mzingo wa tumbo kwa mwanaume unatakiwa kuwa <102cm na kwa mwanamke <88cm
uhusiano kati ya unene na shinikizo la damu ni kutokana na mabadiliko ya hemodynamic katika mwili kama katika kesi hii kwa wagonjwa unene itakuwa ni kuongezeka damu kiasi na index wa moyo ,
Kwa hiyo watanzania wenzangu tupunguzeni kiti moto, kinywaji, kukaa tu ndani bali tujifunze kufanya mazoezi hata ya kutembea ingawaje ya kuogelea ni mazuri zaidi, tukwepe sukari, tule mboga za majani kwa wingi na tuelimishane mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom