Unazikumbuka timu za mtaani enzi hizo?

KIFILI

Member
Jan 23, 2012
87
20
Nadhani hapa kila mtu anayo kumbukumbu ya timu zilizokuwako mtaani kwake enzi hizo akiwa bado kinda,wengine kwa kuzisikia

wengine kwa kuziona live.Mimi kwetu kijiji zilikuwako za vijiji tu lakini nilikua nakuja dar kwa shejmeji yangu baada ya kumuoa

dadangu hivyo nikawa napata bahati ya kuzishuhudia baadhi ya timu za mitaani hapa dar,hizi ni ninazozifahamu mimi...


1:BOOM na ASHANTI zote za ilala,mtananga wake hatumwi mtoto sokoni


2:KIBOKO MSHELI hii nadhani ilikua ya sehemu za manzese kama sikosei,jamaa walikua wandava ile mbaya


3:DAR FIRE hii ilikua sana sana ya watoto wa Kariakoo huku chini nyamwezi,flat za fire hapa na mitaa hii ya jangwani


4:KUMKOMA NYANI GILADI hii sikumbuki sawasawa ilikua ya wapi lakini pia walikua wandava hawa


5:Manyema Rangers,hii ipo mpaka leo nadhani ilikua premier league wakati fulani


Mdau unaweza kuongezea unazozikumbuka na vituko vya mechi baina ya timu hasimu kama Ashanti na Boom n.k. za mikoni ruksa pia tupeni matukio ya mechi za ndondo,mbeya kulikua na moja ya watoto wa mjini ikiitwa TOWN STARZ na RED ANGES a.k.a VASTA,SMALL STAR ya pale Mafiat n.k...
 
mi chama langu NUNGWI la kariakoo mpaka kesho nasikia linawakilisha,uwanja wetu ulikua kule jangwani ukuta wa yanga kwa mbele kidogo,namkumbuka sana mwanangu Hussein Kibavu aliisha China sijui anaendeleaje yule mwana au sijui ndio wavimba macho washamtia kitanzi i dont know maana hawana simile wale watu.
 
Abajalo-sinza
kweli mwana abajalo nao kitambo mitaa ya sinza wanawakilisha,pia kulikua na sinza star wapinzani wao wa jadi enzi zile,nakumbuka abajalo ilikua na kina kalimangonga Ongala enzi flani hivi.
 
Duh boom na ashanti zilikuwa balaa si Dogo mdogo wa nteze john kachezea boom akacheza simba muda mdogo bita john, Abajalo nyimbo yao Abajalo kona baoooo! Mie nakumbuka Wizard kinondoni block 41 na kambarage na bongoyo zilikipiga magunia Msasani. Ashanti na bomu hakuna jadi kama hizo Karume game ikiisha kama huwezi ngumi au kurusha chupa bora dk ya 80 uwe umeondoka uwanjani.
 
Upande wa Temeke...... Panama, Undundu, British, OPEC, bila kusahau Squadi.
Aaaah!.... Mkenge Majini.
 
Kuna Arusha ilikuwa inaitwa WAYA MKALI wengi walikuwa ni masela na wapigaji wa kitu cha aruchaga hawa jamaa walikuwa ni noma sana.
 
kuna timu ilikuwa inaitwa monchwari mob ya tandale au mwananyamala kama sijakosea walikuwa wezi wavuta bangi, kila walipopita walikuwa lazma waibe, na wakikutana na mtu lazma wamvue nguo zote, then walikuwa wakija na jeneza kwenye mechi, walikuwa wanawaibia mpaka polisi kofia zao, refa alikuwa akichezesha mechi yao na panga! ila mimi nilikuwa nachezea timu moja pale uwanja wa bora kijitonyama iliitwa gonga ilikuwa noma! tulipokuwa tukikutana na timu moja ya mikocheni miko villa! palikuwa hapatoshi, hawa jamaa wote walikuwa waarabu tu. mpira ukiisha lazma zichapwe! umenikumbusha mbali kaka tunatoka knyama kwa miguu mpaka kawe na lugalo kwa ajili ya kucheza mechi. kurudi home saa 3 usiku kwa miguu! namkumbuka shibodingo!
 
manzese kulikua na sifa united ya kina madaraka selemani....kariakoo kulikuwa na TOLOLI,Magomeni kulikua na shefield united,hii ilikua pia ni kijiwe kama saigon ipo mpaka leo kama club tu as saigon,lakini hawana timu,huwa wanakutana wenyewe wanafanya hitma kila mwaka,hii ni timu ya DAU huyu wa nssf ambae ni mtoto wa magomeni pure,Tambwe Hiza a.k.a.Tandika Lazi al maarufu enzi hizo,yeye kwao matemeke huko lakini maskani yake ilikua shefield,temeke anakwenda kulala tu,mungine hapo alikua ni huyu mganga sultan Tamba,huwezi amini yule bwana alikua anajua sana soka enzi zake!zamani ilikua raha bwana,ikifika saa kumi jioni mitaani kariakoo na magomeni hupati mtoto wa kumtuma,watoto wote jangwaniiiiiiii,hapa ambapo siku hizi umekua uwanja wa mahubiri na zinduzi za kampeni za vyama,lakini zamani pale ni soka tu viwanja kibao na kila timu na uwanja wake kuanzia pan,simba,yanga,cosmo mpaka watoto kila mtu na kiwanja chake,ndio maana soka lilikua juu..
 
Kwa wakazi wa kigamboni tulikua na:

1.Nanga FC hapa nyota alikua kachupa
2.Shabab-hapa nyota alikua Mwishee na brother yake aliwahi chezea simba
3.Tipper FC-Hapa star alikua Deo Lucas(aliwahi chezea yanga)
4.Mzizima FC
 
Viungutinguti ilikuwepo moja inaitwa yetu africa,nasikia ilikua ina ka uhusiano na watu wa yanga,iringa kulikua na african wonderers,mbeya kulikua na jogoo basha ya kina marehemu shehe pole na mustafa masikio popo pamoja na mbonde mzee wa msondo ngoma ...
 
Gongoni stars, Tindo Tabora- hii ndio alikotokea Baba Tosha Said Mwamba Kizota (Marehemu, Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake)
 
Faru dume, beach boys, kawe rangers sipati picha enzi za mtoano kinesi cup magomeni, yaani unakuta wachezaji wamekodishwa kuanzia kipa hadi reserve, unakuta kombe la mbuzi but gharama inayotumika kumpata mbuzi ni kubwa mara 20 ya zawadi yenyewe, timu inatumia milion kazaa kwa maandaliz ya kumpata mbuzi au jezi, mitaan raha sana those days
 
Back
Top Bottom