Unazi na Ushabiki wa CCM: chimbuko na siri yake nini?

Basically CCM ilikuwa na sera nzuri na ilikuwa na watu makini ndo maana ikawa inapendwa lakini kumbe mwalimu kama binadamu hakuweza kuwajua watu aliokuwa anawalea na kuwafunza ili watakeover alifikiri somo limetosha na hivi wangeendeleza hizo sera nzuri lakni kumbe haikuwa hivyo hivi jiulize kama yanayozungumzwa juu ya Mkapa ni kweli pana ccm tena,ebu muone Kingunge mtu aliyejitia mjamaa mpaka dini akaasi kumbe si chochote si lolote wote walikuwa wanajipendekeza kwa Mwalimu JKNyerere sasa baada ya mzee kufariki karibu wote wamevua ngozi za mwanakondoo wamekuwa chui (their true colours) kwa maana hiyo CCM in books kwa maana ya sera katika maandiko bado ni nzuri maana waasisi wake walikuwa na nia ya kweli na walikuwa wazelendo wa kweli lakini waliowarithi 90% ni manyang'au na kwa hivi yalioyo kwenye sera ya ccm hayatekelezwi tena kumbumka kauli ya mkapa akiwa M/kiti aliwahi kusema kuwa sera za ccm azitekelezeki!! na kwa hivi kuna kila sababu ya kuwaelimisha umma wa watanzania ambao bado wanafikiri mwelekeo wa ccm ni ule ule wa mwanzo watu wakijua kuwa waliokabidhiwa mikoba wamebadili mambo lakini kimya kimya ccm itadondoka tu!! au basi watabadili watu waliopo sasa hivi ili ccm na nchi kwa ujumla wake wapate watu wapya.
 
Labda nifafanue kidogo, maana ya kujiita CCM mfu.

Wakati CCM ikizaliwa, nilikuwa mdogo, nimekuwa na kujifunza siasa tangu enzi za TANU hata CCM, na kamwe sikuwahi kudhani kuwa kuna haja ya kuwa na chama kingine.

Lakini huko kulikuwa ni kupotoka, kutokana na ufinyu wa kujua kuwa mifumo mingine ya kisiasa na kiuchumi, pia ni bora na inaweza kutumika Tanzania na hivyo kutoa demokrasia ya kweli kwa Tanzania na Watanzania ili watu wawe na uhuru wa kuchagua na si kulazimishwa kuamini imani moja ambayo tumeipokea kutoka kwa watawala.

Mimi ni mfuasi wa Nyerere, pamoja na kuw anatofautiana naye. Nitakiri kweny mvuto wangu wa muda mrefu ni ile Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha pamoja na jinsi viongozi wa zamani walivyojitolea kulitumikia Taifa na kuweka nguvu zao katika kulijenga Taifa.

Nidhamu ya kulitumikia Taifa, na kulijenga Taifa ndio siri ya Ufuasi wangu kwa CCM.

Lakini CCM ya sasa na siku hizi, si CCM yangu niliyokulia. Ndiyo maana nasema nimekuwa mfu, maana hata kama Imani ya CCM na katiba yake hazijabadilika, lakini matendo ya CCM na viongozi wake hayaendani na nia ya kulitumikia na kulijenga Taifa.

Ndio maana nimepokea kwa mikono miwili kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vya upinzani ili kuwe na msukumo wa kuwa na chama au kikundi cha watu ambao wakipewa dhamana ya kuongoza, wataweka maslahi yya Taifa mbele, na hivyo kuhakikisha kuwa safari ya maendeleo na demokrasi aambayo itatoa haki na kulinda utu wetu, itafanyika kwa uwiano na kwa heshima na kwa ajili ya Mtanzania na Taifa lake la Tanzania.

Sasa kama mimi na u CCM mfu kwangu si sahihi, je wanaobakia wakidai CCM ina wenyewe na Tanzania bila CCM ni kiyama, wao nia yao inawiana vipi na utiifu kwa Taifa, Ujenzi na Utumishi kwa Taifa?

Kama ni mazoea kuwa CCM ndio pekee, je ni upofu wa namna gani na kuridhika kwa namna gani ambako kunawafanya wananchiwaendelee kuamini kuwa jawabu la kuliondolea Taifa letu Ujinga, Umasikini na Maradhi liko kwa CCM pekee?
 
hongera kishoka kwa kuleta mada hii mimi nachotaka kusema hiki chama kimepoteza mwelekeo,na sasa hivi watoto wao wanarithishwa vyeo,miaka 10 ijayo watoto wao ndio watakuwa mawaziri na makatibu wakuu wa wizara zetu,sisi tunabaki wafagiaji mfano nenda kwenye baadhi ya mashirika wamejaa watoto wao,na siku CCM ikitoka madarakani itakuwa zilipendwa kama nyimbo za maquize au Uda jazz,wanajidanganya watatawala daima hakuna kitu kama hicho dunia,kuna waflume walitisha leo wako wapi?

Jamani tuwaelimishe ndugu zetu waliolewa mvinyo mbovu wa SiSiM ili mwakani tufanye kweli katika uchaguzi
 
imani ya watanzania kwa ccm ni mazoea tu. Zamani enzi za mwalimu tulikuwa tukiimba ile sloglan, tena kabla ya kipindi cha somo la siasa hakijaanza. Mwalimu akiingia darasani, kiranja wa darasa anapiga kofi paa, wote twasimama na kusema!

Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne
> watu
> ardhi
> siasa safi
> uongozi bora

nadhani kadri siku zinavyozidi kwenda, tunazidi kupungukiwa na hivyo vigezo vinne vya maendeleo. Nachelea kusema kimebaki kigezo kimoja tu "watu".

Kama kuna mapenzi ya kweli na ccm, basi ni mazoea tu!!
kikubwa tunachokosa tanzania ni watu,watu,watu....

Jamani uchawi tunao wenyewe kwani viongozi hawa tulio nao wanatokana na sisi...

Sehemu yenye watu ovyo ovyo pia huwa na viongozi hovyo hovyooooo...
 
Nashukuru Rev. Kishoka kwa kuanzisha thread hii.

Nikianzia kwenye siasa inayofuatwa na CCM. Kwa kweli sidhani kuwa CCM ya sasa inafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, wala Azimio la Arusha. Vyote viwili vimeshafunikwa na hakuna hata kiongozi mmoja anaeweza/thubutu kuviongelea licha ya kuvitekeleza.

Mapenzi ya waTanzania kwa CCM ni mapenzi ya Plastic. Ni mapenzi yanayotokana na uoga, tamaa ya mali (hasa fedha) na kutokuwepo kwa uimara wa vyama mbadala. Vile vile yanatokana na hisia kuwa CCM ya zamani inaweza kurudi tena. Subira yavuta kheri.

Watanzania wengi bado wanaamini kuwa wapinzani hawana uwezo wa kuongoza nchi. Hawaoni kama wapinzani wako makini katika kujenga hoja zinazoweza kuwapa wananchi imani ya maisha bora endapo wataamua kuwapa heshima ya kuongoza Taifa hili. Uoga walionao waTanzania endapo chama kingine zaidi ya CCM kitapewa madaraka unatokana na hofu inayopandikizwa na wanasiasa ndani na nje ya CCM.

Kama wengine walivyosema hapo juu, kuna wananchi ambao wanafaidika kwa namna moja au nyingine kwa CCM kuwepo madarakani. Kuna mambo mengi ambayo CCM huyaachia kufanyika ambayo wananchi wanaona ni udhaifu wenye manufaa kwao. Mambo kama takrima, ujenzi holela, biashara zisizodhibitiwa n.k. yanachukuliwa kama fursa ya maisha ya nafuu kwa wananchi. Hivyo wengi wao kuunga mkono CCM ili hali hiyo iendelee kudumu, nao waendelee kujinufaisha. Vile vile CCM imekuwa ikilazimisha wafanya biashara wakubwa kujiunga nao ili wafanikiwe katika biashara zao. Wale waliojaribu kushirikiana na wapinzani walipata matatizo katika shughuli zao na hatimaye kulazimika kujiunga na CCM ili mambo yao yaendelee kuwa mazuri.

Upinzani pia unachangia kuipa CCM nguvu za kuendelea kupata ushabiki. Upinzani imara bado haujaonekana nchini. Kuna mambo mengi yanayokwenda vibaya ambayo wapinzani hawajayatumia ipasavyo kujijenga kisiasa au kuonyesha njia mbadala inayoweza kufanya kero hizo kuepukika na kuleta ustawi kwa Taifa.

Mtazamo wangu ni kwamba, CCM inatumia njia nyingi zenye kuteka hisia za waTanzania katika kujiimarisha. Inatakiwa vyama vya upinzani navyo kuelewa mahitaji ya waTanzania, na kujibu maswali mbalimbali yanayowakera waTZ ili nao wapate nguvu ya kuweza kuleta challenge inayohitajika. Waswahili wanasema "Wengi wape? Hata kama wanaopewa si sahihi.

Upinzani unatakiwa kubuni mbinu za kupata wananchama wengi zaidi ili kupata nguvu za kushindana na CCM katika kila chaguzi, na hatimaye kuweza kuongoza nchi. Wananchi wengi wanakerwa sana na kauli za vitisho, kejeli na matusi kutoka kwa wanasiasa (hasa wa upinzani). Hii inaipa CCM uhalali kwa kuonekana kuwa ni wastaarabu kuliko wapinzani, na hivyo kuungwa mkono na wananchi wengi.
 
Ni kitu gani basi kifanyike kutoka kwetu kwenda kwa wananchi ili tabia ya mazoea ikome?
 
I've said this before. CCM is not the problem but merely a manifestation of the problem. it was suddenly non existant leo..matatizo yetu yangekuwa pale pale
 
kishoka, ss watu wa kijiweni tumeshatoka tongo za macho zamani huku tatizo letu ni nyinyi huko bara mnafikiri kuwa bado Nyerere yu hai, na CCM aliyoiacha ni ile ile aliyoiasisi.
 
Nashukuru Rev. Kishoka kwa kuanzisha thread hii.

Nikianzia kwenye siasa inayofuatwa na CCM. Kwa kweli sidhani kuwa CCM ya sasa inafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, wala Azimio la Arusha. Vyote viwili vimeshafunikwa na hakuna hata kiongozi mmoja anaeweza/thubutu kuviongelea licha ya kuvitekeleza.

Mapenzi ya waTanzania kwa CCM ni mapenzi ya Plastic. Ni mapenzi yanayotokana na uoga, tamaa ya mali (hasa fedha) na kutokuwepo kwa uimara wa vyama mbadala. Vile vile yanatokana na hisia kuwa CCM ya zamani inaweza kurudi tena. Subira yavuta kheri.

Watanzania wengi bado wanaamini kuwa wapinzani hawana uwezo wa kuongoza nchi. Hawaoni kama wapinzani wako makini katika kujenga hoja zinazoweza kuwapa wananchi imani ya maisha bora endapo wataamua kuwapa heshima ya kuongoza Taifa hili. Uoga walionao waTanzania endapo chama kingine zaidi ya CCM kitapewa madaraka unatokana na hofu inayopandikizwa na wanasiasa ndani na nje ya CCM.

Kama wengine walivyosema hapo juu, kuna wananchi ambao wanafaidika kwa namna moja au nyingine kwa CCM kuwepo madarakani. Kuna mambo mengi ambayo CCM huyaachia kufanyika ambayo wananchi wanaona ni udhaifu wenye manufaa kwao. Mambo kama takrima, ujenzi holela, biashara zisizodhibitiwa n.k. yanachukuliwa kama fursa ya maisha ya nafuu kwa wananchi. Hivyo wengi wao kuunga mkono CCM ili hali hiyo iendelee kudumu, nao waendelee kujinufaisha. Vile vile CCM imekuwa ikilazimisha wafanya biashara wakubwa kujiunga nao ili wafanikiwe katika biashara zao. Wale waliojaribu kushirikiana na wapinzani walipata matatizo katika shughuli zao na hatimaye kulazimika kujiunga na CCM ili mambo yao yaendelee kuwa mazuri.

Upinzani pia unachangia kuipa CCM nguvu za kuendelea kupata ushabiki. Upinzani imara bado haujaonekana nchini. Kuna mambo mengi yanayokwenda vibaya ambayo wapinzani hawajayatumia ipasavyo kujijenga kisiasa au kuonyesha njia mbadala inayoweza kufanya kero hizo kuepukika na kuleta ustawi kwa Taifa.

Mtazamo wangu ni kwamba, CCM inatumia njia nyingi zenye kuteka hisia za waTanzania katika kujiimarisha. Inatakiwa vyama vya upinzani navyo kuelewa mahitaji ya waTanzania, na kujibu maswali mbalimbali yanayowakera waTZ ili nao wapate nguvu ya kuweza kuleta challenge inayohitajika. Waswahili wanasema "Wengi wape? Hata kama wanaopewa si sahihi.

Upinzani unatakiwa kubuni mbinu za kupata wananchama wengi zaidi ili kupata nguvu za kushindana na CCM katika kila chaguzi, na hatimaye kuweza kuongoza nchi. Wananchi wengi wanakerwa sana na kauli za vitisho, kejeli na matusi kutoka kwa wanasiasa (hasa wa upinzani). Hii inaipa CCM uhalali kwa kuonekana kuwa ni wastaarabu kuliko wapinzani, na hivyo kuungwa mkono na wananchi wengi.
sawa braza ukumbuke kuwa na CCM mpaka uchaguzi mkuu ujao itatumia dola kujibakisha madarakani nakuapia kwa jina la mungu yeyeto unaemuabudu kuwa leo hii ama kesho ufanyike uchaguzi huru wa haki bila dola kuingilia matakwa ya wananchi ss huku kijiweni CCM ingekuwa historia kama UNIP ya zambia
 
Watu wanashabikia CCM kwa sababu:

1. Ni viongozi wa CCM na wanafaidi matunda ya uhuru kwa njia ya kujineemesha.
2. Wanawania kupata uongozi ili nao wapate mwanya wa kujinufaisha.
3. Wananufaika kwa namna moja au nyingine kutokana na viongozi kuwa ndugu, jamaa, marafiki au jirani zao.
4. Mataahira, wanataka tu waonekane wapo karibu na wakuu. Yaoni wanakula chakula chao kwa harufu ya mchuzi wa kuku. Wengine hata kula kwenyewe hakupo ni kupata harufu.
5. Ujinga, wanaishi kwa matumaini, wanangoja kesho na kesho haifiki. Katika hao wajinga ni pamoja na wale wanaoshabikia ushindi. Yaani ushabiki wa mpira. Unaishabikia timu na uko tayari hata kupigana, lakini ushindi huo haukupi faida zaidi ya kufurahi kwa muda mfupi.
Tazama katika hadhara yoyote utakayojaaliwa kuiona, uone matumbo ya viongozi na yale ya wanaoongozwa. Utajua nasema nini.
 
Ili tuendelee tunahitaji?

Nakumbuka swali hili lilikua maarufu sana kwenye mitihani ya siasa ya darasa la nne/tano lakini tulikua tukikalilishwa tu mambo haya, ni nani aliyefanya utafiti akagundua kua ili watanzania waendelee wanahitaji vitu hivi? maelezo ya ziada yanahitajika hapa.

Watu-watu wa aina gani? wajinga?wasomi?waaminifu?wezi?

Ardhi-ya aina gani? jangwa?yenye madini? yenye mafuta? yenye rutuba?

Siasa safi- ndio ipi?

Uongozi bora-hili halina option,ila kwenye ngazi gani? kitaifa? ngazi zote mpaka kwenye mashirika?.
 
Last edited:
Je kwa tafsiri nyingine tunaweza kutumia ule usemi wa Shibe mwana malevya na Njaa mwana malegeza kwenye hili la CCM na ushabiki wetu?

Je walioshiba wamelewa kupita kiasi na hawataki hata kuachana na ulevi huu? wale walio na njaa wamelegea wakiwa wamezidiwa hata uwezo wa kufikiri na kuanza kujilisha au kujitutumua ili ulegevu unaowafanya wawe watumwa na wanyonge wa walio na shibe?

Je wote tukiwa tuna shibe, tutaendelea kuwa na uroho au tutaanza kugombania kile kidogo kilichoko alimradi kila mtu antaka ashibe zaidi?
 
Umaskini huu, umaskini huu...Kwa kweli kinachoifanya CCM iwe maarufu ni umaskini wa kupindukia ambao CCM yenyewe imekuwa Muhandisi wake kwa miaka yote iliyokuwa madarakani. Na huu umaskini unaineemesha katika ngazi mbalimbali. Kuna wale "kajamba nani" hawa wanahongwa fulana au kikombe cha pombe lya kienyeji a.k.a wanzuki au mbege halafu kuna wale waliosoma ambao wanajua nafasi za kisiasa zina rushwa na pesa kwa hiyo wanataka kuwa CCM ili wapate neema, mwisho kuna wafanya biashara ambao wanajua kuwa CC kutafanya mambo yawanyooke kwa kukwepa ushuru, kupata tender za serikali katika bei ya kuruka n.k. Unapochambua makundi yote haya ya wahanga utakuta kuwa CCM itaendelea kujikanyagia watanzania mpaka sitaki kusema lini.
Naomba kuwakilisha
 
Back
Top Bottom