Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Kwa nini watu wamelewa mvinyo wa CCM? Je ni kwa ajili ya imani ya siasa za ujamaa na kujitegemea? au ni kwa kuwa CCM ni mtoto wa TANU na ASP waliotupatia Uhuru?
Nikijiuliza falsafa na mrengo wa siasa za Tanzania na hasa CCM, sipati jibu! Najiuliza tena ni vipi CCM iwe na washabiki wengi kiasi hicho ambao ni vipofu wa kutupa?
Sikatai miye ni CCM mfu, lakini siwezi kuendelea kuipepea CCM kuwa ni chama thabiti and ndio chama pekee, huku kutoka kushoto mpaka kulia ni vurugu tupu.
Nilipata kumuuliza Mzee wangu moja (jina siri) kuhusu vyama vya siasa na CCM, akanijibu CCM ndio jibu na chama pekee. nilipomuuliza sababu, nikaanza kuimbiwa historia.
Najiuliza hivi ikiwa tunajianda na chaguzi mbili kubwa, ya kwanza ni ya Serikali za mitaa mwaka huu 2009 na uchaguzi mkuu mwakani wa Wabunge na Urais, je wananchi wataichagua CCM kwa kutumia vigezo gani? Je ni mazoea au?
Nikijikumbusha Unazi wa vyama vya siasa Marekani, kati ya Republicans na Democrats, walau unaweza kujua kuna mambo makuu ambayo wanapingana.
Republicans ni mabepari, wanapenda mfumo huria, Serikali ndogo, kodi nafuu, uhuru wa Bunduki, Udini wa Yesu kwa amri za kupinga Uchoko na U S E N G E, kutoa mimba na hili la Usungusungu tangu 9/11.
Democrats pamoja na Ubepari wao wa kijamaa, ndoa za mashoga ni poa, serikali kubwa ni swadakta, kodi kubwa kwa matajiri na dezo dezo kwa wengine ni kama kawaida, kutoa mimba wanadai ni mwanamke na mwili wake na siku hizi suala la mazingira.
Nikirudi Tanzania yetu najiuliza ushabiki ule wa CCM ni kutokana na nini? Walau hata ule wa CUF na CHADEMA japo tunadai ni spesheli kwa mambo ya Udini au Ukabila, unawafuasi kdhaa ambo tunaweza kuwaona kwa tafsiri hizo za mcaho yetu ambazo si lazime kuwa sahihi za Udini na Ukabila, lakini sielewi ni vipi watu tumelewa mvinyo wa CCM!
Je ni mapenzi yetu kwa Nyerere, Azimio la Arusha, Ujamaa au ni vipi? Mbona Azimio na Ujamaa tunaona ni mchungu sasa hivi na umasikini tulionyo, lakini tumefia kidonda hata tukiambiwa CCM itatuzika hai hatusituki?
Wananchi na wale wanachama wa kawaida, niko tayari kukiri wamepotoka na kulewa mvinyo wa Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha (kama mimi ninavyoendelea kucheua chicha la Azimio na Ujamaa) lakini ukienda kwa Viongozi na Watendaji, hawaendani kabisa na imani za Wananchi na Wanachama wa kawaida.
Viongozi wa CCM wanaimba "wananchi inabidi tule mchunga" lakini ukienda nyumbani kwao, wao wanakula kabichi! Viongozi wa CCM wanalia tunywe togwa, rubisi na chimpumu, wao wanashindilia Joni Woka, Brandy na Mvinyo wa ulaya ulaya!
Sasa najiuliza tena ikiwa tunajua hawa jamaa ni walaghai, kwa nini tunaendela kuwaamini na kukienzi chama na tusikimbilie kwa kina UDP, TLP japo wao hawana lolote na ni alosto kama sisi?
Unazi wetu wa kudai CCM ina wenyewe huku sisi tukiwa wajakazi, taarishi, manamba na makuli tunaupata wapi? ni imani gani kubwa hiyo tuliyonayo kwa CCM kumzidi Tanzania, Yesu na Muhamed?
Nasubiri jibu lenu!