SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,616
- 7,863
Je unawezaje kumwambia mtu 'ananuka 'katika lugha ya kistarabu? iwe ni pafyume mbaya, kikwapa , 'mdomo' nk? Kwa watu wa kupita tu(say kwenye daladala) pengine ni rahisi tu kuvumiulia kwa dakika mbili au tatu, lakini kwa mtu ambaye uponaye karibu kwa muda mrefu (say manafanya kazi wote) inakuwa ngumu kweli.
Niliwahi kupata mgeni, ambaye alikuja mjini na ilibidi nimpe hifadhi nyumbani kwangu kwa takribani miezi miwili. Huyo mgeni alikuwa ana tatizo la kutoa harufu mbaya. Yaani kama alikuwa nje halafu akaingia sebuleni, harufu mbaya itasambaa sebule nzima. Nilipofanya uchunguzi nikagundua kwamba huwa haogi, pamoja na kumkarimu bafu zuri la kuoga likiwa na maji massa 24. Hali hii ilikuwa inaniboa sana lakini tatizo langu ilikuwa ni jinsi gani ninaweza kumweleza bila kumfanya ajisikie vibaya.