Unaweza kuendelea kuishi naye ?

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Kuna muhindi rafiki yangu juzi katika kufahamiana zaidi nikamuuliza kuhusu watoto wake akaniambia anaye mmoja wa miaka mitano,nikauliza mbona umechelewa hivyo si uliniambia ndoa ina miaka 16 akasema tulikuwa na mwingine mke wangu alichanganyikiwa na kumtupa toka ghorofani akiwa na miaka 2.Mke akawekwa ndani lakini baada ya muda madaktari wakathibitisha alichanganyikiwa kwa muda hakujuwa alilofanya ikabidi aachiwe.Nikamuuliza sasa una uhakika gani hawezi tena kuchanganyikiwa na kumtupa huyu akadai anampenda sana na amehamia nyumba ya chini na kuna wafanyakazi wawili anaowaamini hapo nyumbani asipokuwepo.

Nauliza hivi wewe unaweza kuendelea kuishi na mtu wa hivi ?
 
Well inategemea mapenzi baina yenu wawili, ila kwa nchi za wenzetu kwa tendo ulilolifanya unanyang'anywa haki za kumlea huyo mtoto sababu unakuwa not capable enough lakini vilevile kuendelea kushi naye inawezekana ikawa njia mojawapo ya kumuonyesha upendo na kuwa unamjali sema tu ndio hivyo you never know when he/she will change na akafanya kituko kingine kwa kweli hapao uporoto ni ngumu sana.
 
kuchanganyikiwa ni sawa na ugonjwa mwingine, tofauti tu ni ugonjwa unaohusisha akili. Mtu yoyote aweza kuchanganyikiwa inategemea na hali iliyomkuta. Kwanini amuache mkewe na aliapa kushi nae kwa shida na raha? Ni sawa tu akiendelea nae.
naongolea usalama wa huyu mtoto.
 
Mkuu kumuacha mweziwako kwakuwa amechanganyikiwa ni kuonyesha ni kiasi gani humjali na kumsamini wazim ni ugonjwa kwahiyo inategemea na haliyake ikovip na uzuri kumuacha
 
Kuna kuwa na matatizo na huwa yanaisha, sio suala la busara kumwacha mwenzio kisa ugonjwa, fananisha huko kuchanganyikiwa sawa na kupata malaria inayotibika kwa Dawa ya mseto, alichanganyikiwa kutokana na stress lakin alitibiwa akapona. Hakuna tatizo.
 
Unajua ikoje? Inapotokea kuna mapenzi ya dhati, matatizo huo hayaonekani kabisa. Hata ikitokea jambo baya limetokea miongoni mwa wapendanao, huwa wanasameheana kiukweli. Umesahau ule usemi wa 'Akipenda chongo huita kengeza?'
 
Inabidi awe makini but "for better for worse" ndio hapo inadhihirika
 
Kuna muhindi rafiki yangu juzi katika kufahamiana zaidi nikamuuliza kuhusu watoto wake akaniambia anaye mmoja wa miaka mitano,nikauliza mbona umechelewa hivyo si uliniambia ndoa ina miaka 16 akasema tulikuwa na mwingine mke wangu alichanganyikiwa na kumtupa toka ghorofani akiwa na miaka 2.Mke akawekwa ndani lakini baada ya muda madaktari wakathibitisha alichanganyikiwa kwa muda hakujuwa alilofanya ikabidi aachiwe.Nikamuuliza sasa una uhakika gani hawezi tena kuchanganyikiwa na kumtupa huyu akadai anampenda sana na amehamia nyumba ya chini na kuna wafanyakazi wawili anaowaamini hapo nyumbani asipokuwepo.

Nauliza hivi wewe unaweza kuendelea kuishi na mtu wa hivi ?

CW... hii ni moja ya ile situation likikukuta ndio unajua nini utafanya....

Huyo baba anastahili pongezi... hayo Mapenzi hakuna mfano....
 
Kuna muhindi rafiki yangu juzi katika kufahamiana zaidi nikamuuliza kuhusu watoto wake akaniambia anaye mmoja wa miaka mitano,nikauliza mbona umechelewa hivyo si uliniambia ndoa ina miaka 16 akasema tulikuwa na mwingine mke wangu alichanganyikiwa na kumtupa toka ghorofani akiwa na miaka 2.Mke akawekwa ndani lakini baada ya muda madaktari wakathibitisha alichanganyikiwa kwa muda hakujuwa alilofanya ikabidi aachiwe.Nikamuuliza sasa una uhakika gani hawezi tena kuchanganyikiwa na kumtupa huyu akadai anampenda sana na amehamia nyumba ya chini na kuna wafanyakazi wawili anaowaamini hapo nyumbani asipokuwepo.

Nauliza hivi wewe unaweza kuendelea kuishi na mtu wa hivi ?

Duh! inahitaji moyo wa hali ya juu maana hata kufiwa na mtoto kwa hali ya kawaida kunaweza kabisa kusambaratisha ndoa kama wanandoa hawatakuwa makini katika kipindi hicho kigumu kwao.
 
Mimi naweza kuwa nae lakini nitakuwa mwangalifu kwa afya yake na mtoto; kwa upande mwingine ilitokea kwa jirani yangu ambaye ana watoto watatu, mkewe alipatwa na wazimu. Kakaa nae kwa miaka miwili katika hali hiyo mpaka alipopona, kamuacha kutokana na ndugu wa mwanamke ambao waliingiza imani za kishirikina kwa kudai kuwa ni yeye mwenyewe ndio kamfanyia hivyo kwa manufaa yake binafsi ya kibiashara ndio maana kadiriki kukaa nae muda wote huo.
 
Kuna muhindi rafiki yangu juzi katika kufahamiana zaidi nikamuuliza kuhusu watoto wake akaniambia anaye mmoja wa miaka mitano,nikauliza mbona umechelewa hivyo si uliniambia ndoa ina miaka 16 akasema tulikuwa na mwingine mke wangu alichanganyikiwa na kumtupa toka ghorofani akiwa na miaka 2.Mke akawekwa ndani lakini baada ya muda madaktari wakathibitisha alichanganyikiwa kwa muda hakujuwa alilofanya ikabidi aachiwe.Nikamuuliza sasa una uhakika gani hawezi tena kuchanganyikiwa na kumtupa huyu akadai anampenda sana na amehamia nyumba ya chini na kuna wafanyakazi wawili anaowaamini hapo nyumbani asipokuwepo.

Nauliza hivi wewe unaweza kuendelea kuishi na mtu wa hivi ?

Veve kumbe haina siri...mimi dokeza tatizo zangu veve sema kwa forum....mitanzania iko haina fikiria mbaga rahisi yenu...mimi itamtafuta rafiki angu rostam shughulikia veve....
 
Mkuu Uporoto kuna jamaa mmoja kama ulishawahi sikia Kenji wa huko mwanza ana ferries(RIP), aliulizwa na jamaa ake kama veve file uliza hindi..mbona una mtoto mmoja na una mali kibao hivi akifa je? Jamaa akamjibu na kwa nini afe? siku mbili muuliza swali akafariki kwa kugongwa na gari...Lkn khs veve mkuu, huyo mhindi anapenda...huangaliagi picha za KIHINDI wewe? au tu misemo ya kiswahili? "anajifanya kupenda kihindi au kichina" sasa hapo mkuu huna la kuuliza tena...
 
Duh! Siku akinitupa mwenyewe je! Aah!
Kama bado twapendana tutaendelea tu na nitachukua tahadhari. Uporoto usichanganyikiwe ukakatupa kale katoto ketu karembo.
 
Mi ntaendelea kuishi nae coz hata madaktari wamethibitisha kua ulikua uchizi wa muda, kwa sasa atakua ni mzima kabisa, isingekua hivyo madaktari wangenipa angalizo natumai!
 
Hakuna sababu ya kumuacha maana anaweza akachanganyikiwa zaidi,cha muhimu na kuchukua tahadhari tu kama jamaa alipoamua kuhamia nyumba ya chini na kuweka wafanyakazi wawili anaowaamini.
 
Kuna muhindi rafiki yangu juzi katika kufahamiana zaidi nikamuuliza kuhusu watoto wake akaniambia anaye mmoja wa miaka mitano,nikauliza mbona umechelewa hivyo si uliniambia ndoa ina miaka 16 akasema tulikuwa na mwingine mke wangu alichanganyikiwa na kumtupa toka ghorofani akiwa na miaka 2.Mke akawekwa ndani lakini baada ya muda madaktari wakathibitisha alichanganyikiwa kwa muda hakujuwa alilofanya ikabidi aachiwe.Nikamuuliza sasa una uhakika gani hawezi tena kuchanganyikiwa na kumtupa huyu akadai anampenda sana na amehamia nyumba ya chini na kuna wafanyakazi wawili anaowaamini hapo nyumbani asipokuwepo.

Nauliza hivi wewe unaweza kuendelea kuishi na mtu wa hivi ?
kama imethibitika ni mgonjwa tatizo liko wapi?? au ndio unyanyapaa?
 
Sijui Mhindi kasikia Uporoto1 kamwaga hapa kamtupa mwenyewe? maana haonekani tena...mwenye kujua alipo atoe taarifa jamni...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom