Unawakumbuka tatu nane??? hivi hii bendi bado ipo...??!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Kwa wale wapenzi wa muziki kulikuwa na bandi iliyoitwa tatu nane. Bendi hii nilivutiwa na style yao ya muziki pale walipotumia vifaa vya kisasa kupiga nyimbo zenye mahadhi ya kiasili...Ni muda mrefu sijasikia habari zao. Mwenye kufahamu naomba anijuze tafadhari.
 
Rafael Sabuni alishafariki. Vijana wa Mhuto sijui wako wapi hivi sasa. Nami pia nawakumbuka Tatu Nane. Walikuwa wanapiga pale Twiga Stars miaka ya 70 plus.
 
Na Dula sijui yuko wapi jamani kama kuna mtu na ana CD za hiyo bendi atudondoshee humu,pia alikuwepo marehemu Naliene kama sikosei alikuwa anapuliza filimbi kwa kutumia pua
 
Na Dula sijui yuko wapi jamani kama kuna mtu na ana CD za hiyo bendi atudondoshee humu,pia alikuwepo marehemu Naliene kama sikosei alikuwa anapuliza filimbi kwa kutumia pua
..Hawa jamaa ilikuwa ni group ya watu waliokuwa wanajua wana fanya nini ingawa nasikitika hilo kundi halikudumu sana lakini kazi zao zilikuwa makini sana. Kwa kweli hata mimi natafuta CD zao..
 
Tatunane: wengine marahemu wengine wametawanyika.
Naliene marehemu,alikuwa anapiga ngoma na filimbi hadi puani.
Mahdi (Tumbo,nadhani) marehemu alikuwa anapiga gitaa rythm,
Charle Mhuto yuko Ohio,USA, Ted Mbaraka uncle wake ana bedi yake hapo Bongo,
Dulla yuko Denmark, alikuwa anapiga gitaa bass, anaishi pale, wengine sijui.
Hakuna bendi itakayotuweka kwenye ramani ya dunia kimziki kama hawa wanaume, bila kumuacha mzee Marehemu Hukwe Zawose.
Nina album za Tatunane mbili kwenye cd, zile zilidhinda award kule France (walishinda namba moja mbele ya magiwji kama Manu Dibango,m Angela kidjo na Yousson N'dou ) nikipata muda nitaziweka humu, wka wapendi wa African music,
pamoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom