Unawafahamu vizuri madaktari wa muhimbili?

Ama kweli nyoka akikabwa koo!!

Madaktari hawana nafasi ya kukwapua fedha za serikali kama wewe mhasibu au mkurugenzi,
Wateja wao ni wagonjwa,

Wakati wamegoma wakidai kuongezewa mishahara hakuna mwananchi hata mmoja aliyewatetea, nyote mliwaona wajinga na kuwacheka
Sasa wamejua mbinu ya kuzitunza familia zao ndo mnalalamika
Hakuna asiyependa maisha mazuri, wewe kama unaendesha benz, hata daktari anapenda
Kama udaktari ni wito, mbona wewe hukusomea ili uwasaidie ndugu zako?
Kama udaktari ni wito; mara ngapi umepeleka sadaka kwa familia ya daktari kama unavyopeleka kwa mchungaji, padre n.k

Everything has its price my dear, kama huwezi kulipa you know the price you will pay...
Unless we pay them well, this will never stop
We cant have a good health system at the expense of docs, we have to pay for it either way.

So ndugu yangu acha kulalamika. Mbona huongei kuhusu pesa ya barabara uliyoiba?, pesa ya miradi ya maendeleo uliyoiba na kujenga nyumba yako mbezi beach? Mbona huongei kuhusu pesa ya watu uliyochelewa kusaini wakati wameitolea jasho? Mbona huongei kuhusu chek feki ulizosaini ili ujipatie mali? Unajua ni watu wangapi walikufa kwa sababu ya wizi wako?

Acheni kuhukumiana, kwa nchi yetu ilivyo kwa sasa hakuna mtu anayeweza kumnyooshea mwenziye kidole,
Waacheni madaktari watafute chakula ya familia yao kama nyinyi mnavyoiibia serikali kutafuta chakula kwa watoto wenu khaaaaaa!!!!!!!! Mnataka wale polisi???

Wewe kweli ni great thinker and u have said it all
 
Mkitaka msiendelee kufa,boresheni maslahi ya madaktari,boresheni mazingira ya kazi na hospitali zenu kiujumla.Hapo ndipo mtaweza kupata huduma bora.Unaona nongwa daktari kulipwa milioni?milioni nayo hela?Wewe unajua uchungu na shuruba za kusoma medicine?Wabunge mbona wanalipwa mamilioni lakini hampigi kelele?Wanachofanya nini hasa kule bungeni?Watu wengine bwana,hovyo
 
Tuboreshe hadi kiwango gani? Kila daktari apewe nyumba yenye swimming pool? Kila dakatri alipwe milioni 10? Kila hospitali iwe na CT Scan? Mnataka nini, nyie mliojaliwa kusoma? Na hao walimu waliowatoa makamasi na kukufundisha kusoma , nao walipwe nini? Na hao , wafagiaji wanaofagia ofisi zenu ili muwe na mazingira yanayoendana na hadhi yenu, walipwe nini? Sasa kwa vile wabunge wanatudhulumu tusioenda shule basi na wewe unaona unastahili kutudhulumu. Hebu, msomi uliojaaliwa, tufahamishe huo uchungu na shuruba za kusomea udaktari ambazo mhandisi, ngwini, muuguzi, fundi mchundo, wakili, mtapisha choo n.k. hawapitii! Kama mnaona hapawafai, basi heri muachie ngazi na mtuache tujifie badala ya kutumnyanyasa kwa vile tu mmeelimika kuliko sisii. Hivi kile kiapo chenu bado mnaapa? Au na chenyewe kimekuwa nongwa!

Amandla.....
 
Sijawahi chukua rushwa ya mtu, japo ni daktari bingwa. Na hata mtu akitaka kunipa rushwa atataka anipe elfu 5, 10, 50. Itanipa laana tu.
Ni kweli baadhi ya madaktari wanachukua rushwa, ila ni rushwa ndogo ndogo ambazo haziwatoi kimaisha. Lakini watu wengi huwa wanakamuliwa pesa na watu wa cadre za chini, na kwa kuwa uelewa wa watanzania wengi ni mdogo kwao kila mtu ni daktari.
Kila sehemu mambo yameharibika, afya haijapona. Lakini kabla hujalaumu uliza umepanda nini kabla hujavuna, umemlipa nini kabla hujapata huduma, serikali imewekeza kiasi gani katika afya, mazingira ya kufanyia kazi yakoje. Tusilaumu tu, wakati mtu kutoa elfu 10 kwa ajili ya consultation ni shida, ila kunywea beer sio shida. unalaumu mpaka povu lakutoka. Watu afya kwao sio priority. Ataweka budget ya kununua gas na chakula, lakini hakuna ya afya. Unasubiri mpaka uonane na doctor baa ndipo uanze kumwambia unavyoumwa. Kaangalie sehemu madaktari wanapoliwa vizuri, je huwa wanafanya kazi kiasi gani. Msilaumu tu, kwani wewe ofisi kwako huwa wafanya nini kwa wateja wako...
 
Haunijui, sikujui kwa hiyo inabidi nikuamni kuwa kweli ni daktari bingwa. Nyinyi madaktari mabingwa ndiyo wabaya zaidi. Hivi unadhani rushwa ni vile vijisenti wanavyopewa wahudumu ili wasogeze mafaili. Hapana, nyinyi mnaoitwa mabingwa mko more sophisticated. Wengi wenu, kwanza ni miungu mtu. Hampatikani katika hizo hospitali mnazozibeza humu bali mnapatikana huko ambako mnakolipwa inavyostahili. Hivi kweli unatudharau kiasi cha kutuambia kuwa hatujui daktari ni nani wakati wengine wenu ni watoto wetu? Unaishi nchi gani hiyo ambayo mwananchi wa kawaida haoni taabu kunywa bia za alfu kumi lakini anashindwa nauli ya daladala kiasi cha kutembea kwa mguu kutoka mbagala hadi mjini? Na kwa vile wewe elfu kumi si kitu basi unamshangaa mtu ambae hata pesa ya kununua chandarua cha alfu mbili anaposhindwa kukulipa ka-konsaltansi fii ka sh. 10,000! Wewe mtu hela ya kula hana bado unataka aweke pesa kwa ajili ya dharura ya afya! Your arrogance knows no bounds. Sasa, kwa vile mnajua kuna sehemu ambako madaktari wanalipwa vizuri tofauti na huku kwetu basi do us all a favour muende huko badala ya kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Tutakufa, ndio, lakini tutajua kuwa hao ma Medical Assistant na wauguzi watakaobaki wamejitahidi kadri ya uwezo wao. Sio nyie ambao bila shaka hata kutuangalia mnaona kinyaa. Kweli akukanae hakuchagulii tusi.

Chini ya mwembe ninakofanya shughuli zangu nina jitahidi kadri yauwezo wangu kutoa huduma inayostahili. Lakini hata siku moja sitakataa kuwa kuna mafundi mchundo waovu, wezi, wabambikaji n.k.

Amandla......
 
Haunijui, sikujui kwa hiyo inabidi nikuamni kuwa kweli ni daktari bingwa. Nyinyi madaktari mabingwa ndiyo wabaya zaidi. Hivi unadhani rushwa ni vile vijisenti wanavyopewa wahudumu ili wasogeze mafaili. Hapana, nyinyi mnaoitwa mabingwa mko more sophisticated. Wengi wenu, kwanza ni miungu mtu. Hampatikani katika hizo hospitali mnazozibeza humu bali mnapatikana huko ambako mnakolipwa inavyostahili. Hivi kweli unatudharau kiasi cha kutuambia kuwa hatujui daktari ni nani wakati wengine wenu ni watoto wetu? Unaishi nchi gani hiyo ambayo mwananchi wa kawaida haoni taabu kunywa bia za alfu kumi lakini anashindwa nauli ya daladala kiasi cha kutembea kwa mguu kutoka mbagala hadi mjini? Na kwa vile wewe elfu kumi si kitu basi unamshangaa mtu ambae hata pesa ya kununua chandarua cha alfu mbili anaposhindwa kukulipa ka-konsaltansi fii ka sh. 10,000! Wewe mtu hela ya kula hana bado unataka aweke pesa kwa ajili ya dharura ya afya! Your arrogance knows no bounds. Sasa, kwa vile mnajua kuna sehemu ambako madaktari wanalipwa vizuri tofauti na huku kwetu basi do us all a favour muende huko badala ya kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Tutakufa, ndio, lakini tutajua kuwa hao ma Medical Assistant na wauguzi watakaobaki wamejitahidi kadri ya uwezo wao. Sio nyie ambao bila shaka hata kutuangalia mnaona kinyaa. Kweli akukanae hakuchagulii tusi.Chini ya mwembe ninakofanya shughuli zangu nina jitahidi kadri yauwezo wangu kutoa huduma inayostahili. Lakini hata siku moja sitakataa kuwa kuna mafundi mchundo waovu, wezi, wabambikaji n.k. Amandla......
Niambie mwenzangu wafanya shughuli gani zisizokuwa na lawama. Hata makanisani na misikitini pia wana matatizo haya haya. Taja kazi yako pia ili waathirika waseme.Hata Mungu analaumiwa...
 
Mimi ni Fundi Mchundo. Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa hakuna kazi isio na lawama. Kosa lenu ni kuwaona wote wanaolalamika kuwa ni madomo kaya wanaowaonea wivu. Kama vile wanaowalalamika mafundi mchundo, wengi wao wameumizwa na wenzetu katika fani zetu. Mtu kusema mafundi mchundo walaghai, hawaaminiki hakumaanishi kuwa wanammaanisha Fundi Mchundo wa JF (kama yeye ni msafi). Sitawatendea haki nikifanya kama unavyofanya wewe, kuwabeza na kuwaambia kuwa umbumbu wao ndio unaofanya wadhulumiwe. Uovu ni uovu tu, hata afanye nani.

Amandla......
 
Tuboreshe hadi kiwango gani? Kila daktari apewe nyumba yenye swimming pool? Kila dakatri alipwe milioni 10? Kila hospitali iwe na CT Scan? Mnataka nini, nyie mliojaliwa kusoma? Na hao walimu waliowatoa makamasi na kukufundisha kusoma , nao walipwe nini? Na hao , wafagiaji wanaofagia ofisi zenu ili muwe na mazingira yanayoendana na hadhi yenu, walipwe nini? Sasa kwa vile wabunge wanatudhulumu tusioenda shule basi na wewe unaona unastahili kutudhulumu. Hebu, msomi uliojaaliwa, tufahamishe huo uchungu na shuruba za kusomea udaktari ambazo mhandisi, ngwini, muuguzi, fundi mchundo, wakili, mtapisha choo n.k. hawapitii! Kama mnaona hapawafai, basi heri muachie ngazi na mtuache tujifie badala ya kutumnyanyasa kwa vile tu mmeelimika kuliko sisii. Hivi kile kiapo chenu bado mnaapa? Au na chenyewe kimekuwa nongwa!

Amandla.....

Yes kwa jinsi maisha yalivyopanda na ukizingatia umuhimu wao-mshahara wa Daktari(MD)anayeanza kazi walau usiwe chini ya M3.Swimming pools siyo muhimu na unafahamu kuwa siyo muhimu,isipokuwa CT scanning ni muhimu sana kuwepo walau walau hata mngejitahidi katika kila hospitali ya mkoa pawe na hiki kipimo.CT scan umeitaja wewe,lakini pia kuna vipimo vingine muhimu sana(sitavitaja-kuokoa muda),hatunavyo hapa nchini vya kusaidia kufikia true positive diagnosis mapema,hivyo kufanya pia matibabu sahihi yaanze mapema.Unafiki maboresho yangetosha kama unavyojaribu kutetea,Mzee Malecela angekwenda kupasuliwa moyo Uingereza?
Kusema Daktari asilipwe vizuri kwa vile walimu hawalipwi vizuri ni upuuzi.Mbona kwa wenzetu,madaktari wanalipwa vizuri kuliko waalimu au hata nyie watu wa BA na hakuna kelele?kwanini?Huwezi kujua uchungu wa medical school kwa kusimuliwa.Ukisimuliwa utaona ni rahisi tu,utasema mbona hata nyie na kozi zenu za miaka mitatu mitatu huku mnakwenda club kila mwisho wa wiki,mmesoma na mnaujua uchungu wa kung'atwa na mbu na ku sup.Mtu amesotea chuoni miaka karibu 13 kuwa bingwa,na kazi yenyewe ni delicate na bado inamlazimu asome sana pia hata sasa baada ya kumaliza shule kwa faida yenu nyinyi kila Fundimchundo,halafu unampa mshahara sawasawa na mpiga deni wa TRA??Halafu wewe unaona sawa tuu,eti wito,dah!
 
Mkitaka msiendelee kufa,boresheni maslahi ya madaktari,boresheni mazingira ya kazi na hospitali zenu kiujumla.Hapo ndipo mtaweza kupata huduma bora.Unaona nongwa daktari kulipwa milioni?milioni nayo hela?Wewe unajua uchungu na shuruba za kusoma medicine?Wabunge mbona wanalipwa mamilioni lakini hampigi kelele?Wanachofanya nini hasa kule bungeni?Watu wengine bwana,hovyo

Hizi kelele za posho na kadhalika zinazopigwa huzisikii? Hata hapa jamvini zipo kibao. Ama umeziba masikio yako kuhalalisha uuaji?
 
Ulishawahi kuleta thread hapa kupinga posho za wabunge?Au kwavile sasa Zito kasema?
 
Yes kwa jinsi maisha yalivyopanda na ukizingatia umuhimu wao-mshahara wa Daktari(MD)anayeanza kazi walau usiwe chini ya M3.Swimming pools siyo muhimu na unafahamu kuwa siyo muhimu,isipokuwa CT scanning ni muhimu sana kuwepo walau walau hata mngejitahidi katika kila hospitali ya mkoa pawe na hiki kipimo.CT scan umeitaja wewe,lakini pia kuna vipimo vingine muhimu sana(sitavitaja-kuokoa muda),hatunavyo hapa nchini vya kusaidia kufikia true positive diagnosis mapema,hivyo kufanya pia matibabu sahihi yaanze mapema.Unafiki maboresho yangetosha kama unavyojaribu kutetea,Mzee Malecela angekwenda kupasuliwa moyo Uingereza?
Kusema Daktari asilipwe vizuri kwa vile walimu hawalipwi vizuri ni upuuzi.Mbona kwa wenzetu,madaktari wanalipwa vizuri kuliko waalimu au hata nyie watu wa BA na hakuna kelele?kwanini?Huwezi kujua uchungu wa medical school kwa kusimuliwa.Ukisimuliwa utaona ni rahisi tu,utasema mbona hata nyie na kozi zenu za miaka mitatu mitatu huku mnakwenda club kila mwisho wa wiki,mmesoma na mnaujua uchungu wa kung'atwa na mbu na ku sup.Mtu amesotea chuoni miaka karibu 13 kuwa bingwa,na kazi yenyewe ni delicate na bado inamlazimu asome sana pia hata sasa baada ya kumaliza shule kwa faida yenu nyinyi kila Fundimchundo,halafu unampa mshahara sawasawa na mpiga deni wa TRA??Halafu wewe unaona sawa tuu,eti wito,dah!

Umeenda shule lakini haujaelimika. Umuhimu upi huo unaozungumzia wa kusema waanzie milioni tatu? Uwezo wa CT Scan kwa kila hospitali ya mkoa utatoka wapi? Hao mafundi mchundo wa kuzihudumia ili zisiharibike wakati nyie waheshimiwa mkitizumia watatoka wapi? Hata tungeboresha vipi, huyo Mkuu angeenda Uingereza. Hao hata kupima macho wanataka kwenda nje. Hawana tofauti na nyie, sense yao ya entitlement inatupeleka pabaya. Unatambia ukugumu wa shule yako, nenda kamsome Derrida uone kama utaona ndani. Au Hegel, au Foucault. Kila kitu kina ugumu wake. Hata kazi ya utopaz si kila mtu anaiweza.

Wewe ugumu wa hizo fani nyingine unaujua? Inawezekana umesotea shule miaka yote hiyo kwa sababu ni kipunga. Kama kushinda baa ni ishara ya urahisi wa fani, mbona maprofesa wenu hawasehemu zao maalum huko.

Sasa, kama inakuuma kiasi hicho , kulipwa mshahara sawa na mtoza ushuru, si nenda Botswana au marekani ambako utalipwa unavyostahili? Unaogopa nini? Nenda tu, watakaokulilia ni ndugu zako ambao wanafaidi hizo rushwa unazovuta.

Mamlaka ya kuhukumu watu kuwa wameelimika au hawajaelimika,umeyapata wapi?Unauliza uwezo wa CT scan kila mkoa utatoka wapi?Mngekusanya kodi vizuri na kupunguza warsha,makongamano,semina elekezi,mashangingi na matumizi mengine ya anasa,hizo pesa zisingetosha kufanya mambo makubwa ya maendeleo zaidi ya hizo CT scans?Kwanini uwazie kuwa zitaharibika na tutashindwa kuzihudumia?Kwahiyo ni bora magonjwa yachelewe kugundulika au mgonjwa afanyiwe wrong diagnosis kwavile uwezo wa kuwa na CT scan tunao,isipokuwa tu hatuna mafundimchundo wa kuzihudumia zisiharibike,hivyo bora tusiziagize tuu?

Philosophy nimeisoma mkuu.Sema naweza nisiwe na nadharia za kipuuzi kama za hao miungu wako,lakini walau nimeipitia.Tena ilikuwa ni lazima kwenye program yetu kuchukua philosophy,psychology,historia(kwa ajili ya kina Hippocrates,Ibn Sina nk) na sociology.Kila kitu kina ugumu wake,lakini ugumu unatofautiana kulingana na unyeti wa kitu husika.Ndiyo maana udaktari kwa shahada ya kwanza unasomea kwa miaka 5 au 4 kwa US/CANADA kama tayari una shahada nyingine,au 6/7 kwa Urusi nk nk lakini sociology ni miaka mitatu tu,unagraduate.

Sijasota miaka 13 chuoni kusomea shahada ya kwanza ya udaktari kama unavyodhani.Huo ulikuwa mfano tu,kwamba kuna specialization nyingine zinachukuwa miaka hata zaidi ya hiyo ili kuhitimu.Mimi hainiumi kiasi hicho,ila inaniuma kwamba taaluma nyeti kama udaktari haithaminiwi Tanzania.
Na nikufahamishe tu kwamba sina kibarua na serikali ya Tanzania na huko Marekani unakodhani nakuogopa,nilishawahi kusomea vitu fulani na hata kuvifanyia kazi.
 
Mimi si ndio maana nasema umeenda shule lakini haujaelimika? Hii ni kati ya nchi maskini duniani, na hata wakiwabana hao wafanyabiashara wachache, kuuza mashangingi yote yaliyokuwepo, na kuondoa warsha katika msamiati wao wasingweza kuzisambaza hizo CT scan kama unavyodai. Unasema haziotoharibika wakati hizo chache zilizopo, si kwenye hospitali binafsi au za serikali, haziishi kuharibika. Mashine kama hizo zinahitaji mazingira mazuri, umeme wa uhakika na wataalamu wanaojua namna ya kuzitumia na kuzifanyia maintenance za kila wakati. Hao ndio mafundi mchundo unaotubeza. Nadhariia yako ya kuziagiza ili tuwe na bragging rights ndiyo iliyotufanya tuagize Radar system ya ajabu, kujenga mashule bila wlimu wala vifaa n.k. Uzuri wa chombo ni kukitumia na si kukiangalia kama mapambo.

Philosophy inawezekana ulisoma lakini sidhani kama uliiielewa. Ungeielewa usingesema upuuzi huu unaouleta hapa. Mbona hata ma-architecture wanasoma kozi ndefu kama ya kwenu lakini hatuwasikia wakitamba humu? Na urefu, Mkuu, si ishara kuwa ni ngumu zaidi. Hivi utasema mtu anayekimbia mita 400 ana nafuu kuliko anayekimbia mita 3000? Ugumu unatokana na uzito na eneji unayotumia katika huo muda unaofanya hicho kitu. Au Einstein hakufanya kitu kwa sababu ka equation alikokatoa e=mc2? Unakuwa kama maafande ambao nasikia walikuwa wanadhani ugumu wa shule unaendana na wingi wa masomo, kwa hiyo waliochukua kombinesheni za matoto matatu walikuwa vilaza ukilanganisha waliomaliza kidato cha nne ambako masomo yalikuwa zaidi!

Uliyesema umesoma miaka 13 ni wewe na wala sio mimi. Kama haikuhusu kwa nini basi uliitolea mfano. Hivi mnataka mheshimiwe vipi? Mnaanza na mshahara wa juu serikalini kuliko fani yeyote ile. Mnapoanza tu mnapewa stahili ya kupewa nyumba. Tatizo mnajilinganisha na taasisi ambazo zinaendeshwa tofauti. Mbona huko majuu haukuti madaktari wakigoma kwa sababu wacheza mpira wanalipwa mishahara ya ajabu? Kama inakusumbua basi heri acha kazi ya udaktari ujiunge nao kama walivyofanya wenzako walioingia kwenye siasa ili nao wavute vijisenti.

Hicho cha kibarua na serikali na za huko Marekani hayanihusu. Mada hii inazungumzia madaktari wa Muhimbili na by extension wa serikalini na sio wa Aga Khan au wale walio kwenye NGO za Ukimwi!

Amandla.....
 
Mimi si ndio maana nasema umeenda shule lakini haujaelimika? Hii ni kati ya nchi maskini duniani, na hata wakiwabana hao wafanyabiashara wachache, kuuza mashangingi yote yaliyokuwepo, na kuondoa warsha katika msamiati wao wasingweza kuzisambaza hizo CT scan kama unavyodai. Unasema haziotoharibika wakati hizo chache zilizopo, si kwenye hospitali binafsi au za serikali, haziishi kuharibika. Mashine kama hizo zinahitaji mazingira mazuri, umeme wa uhakika na wataalamu wanaojua namna ya kuzitumia na kuzifanyia maintenance za kila wakati. Hao ndio mafundi mchundo unaotubeza. Nadhariia yako ya kuziagiza ili tuwe na bragging rights ndiyo iliyotufanya tuagize Radar system ya ajabu, kujenga mashule bila wlimu wala vifaa n.k. Uzuri wa chombo ni kukitumia na si kukiangalia kama mapambo.Philosophy inawezekana ulisoma lakini sidhani kama uliiielewa. Ungeielewa usingesema upuuzi huu unaouleta hapa. Mbona hata ma-architecture wanasoma kozi ndefu kama ya kwenu lakini hatuwasikia wakitamba humu? Na urefu, Mkuu, si ishara kuwa ni ngumu zaidi. Hivi utasema mtu anayekimbia mita 400 ana nafuu kuliko anayekimbia mita 3000? Ugumu unatokana na uzito na eneji unayotumia katika huo muda unaofanya hicho kitu. Au Einstein hakufanya kitu kwa sababu ka equation alikokatoa e=mc2? Unakuwa kama maafande ambao nasikia walikuwa wanadhani ugumu wa shule unaendana na wingi wa masomo, kwa hiyo waliochukua kombinesheni za matoto matatu walikuwa vilaza ukilanganisha waliomaliza kidato cha nne ambako masomo yalikuwa zaidi!Uliyesema umesoma miaka 13 ni wewe na wala sio mimi. Kama haikuhusu kwa nini basi uliitolea mfano. Hivi mnataka mheshimiwe vipi? Mnaanza na mshahara wa juu serikalini kuliko fani yeyote ile. Mnapoanza tu mnapewa stahili ya kupewa nyumba. Tatizo mnajilinganisha na taasisi ambazo zinaendeshwa tofauti. Mbona huko majuu haukuti madaktari wakigoma kwa sababu wacheza mpira wanalipwa mishahara ya ajabu? Kama inakusumbua basi heri acha kazi ya udaktari ujiunge nao kama walivyofanya wenzako walioingia kwenye siasa ili nao wavute vijisenti.Hicho cha kibarua na serikali na za huko Marekani hayanihusu. Mada hii inazungumzia madaktari wa Muhimbili na by extension wa serikalini na sio wa Aga Khan au wale walio kwenye NGO za Ukimwi!Amandla.....
unajua maana ya amandla?
 
Mimi si ndio maana nasema umeenda shule lakini haujaelimika? Hii ni kati ya nchi maskini duniani, na hata wakiwabana hao wafanyabiashara wachache, kuuza mashangingi yote yaliyokuwepo, na kuondoa warsha katika msamiati wao wasingweza kuzisambaza hizo CT scan kama unavyodai. Unasema haziotoharibika wakati hizo chache zilizopo, si kwenye hospitali binafsi au za serikali, haziishi kuharibika. Mashine kama hizo zinahitaji mazingira mazuri, umeme wa uhakika na wataalamu wanaojua namna ya kuzitumia na kuzifanyia maintenance za kila wakati. Hao ndio mafundi mchundo unaotubeza. Nadhariia yako ya kuziagiza ili tuwe na bragging rights ndiyo iliyotufanya tuagize Radar system ya ajabu, kujenga mashule bila wlimu wala vifaa n.k. Uzuri wa chombo ni kukitumia na si kukiangalia kama mapambo.

Philosophy inawezekana ulisoma lakini sidhani kama uliiielewa. Ungeielewa usingesema upuuzi huu unaouleta hapa. Mbona hata ma-architecture wanasoma kozi ndefu kama ya kwenu lakini hatuwasikia wakitamba humu? Na urefu, Mkuu, si ishara kuwa ni ngumu zaidi. Hivi utasema mtu anayekimbia mita 400 ana nafuu kuliko anayekimbia mita 3000? Ugumu unatokana na uzito na eneji unayotumia katika huo muda unaofanya hicho kitu. Au Einstein hakufanya kitu kwa sababu ka equation alikokatoa e=mc2? Unakuwa kama maafande ambao nasikia walikuwa wanadhani ugumu wa shule unaendana na wingi wa masomo, kwa hiyo waliochukua kombinesheni za matoto matatu walikuwa vilaza ukilanganisha waliomaliza kidato cha nne ambako masomo yalikuwa zaidi!

Uliyesema umesoma miaka 13 ni wewe na wala sio mimi. Kama haikuhusu kwa nini basi uliitolea mfano. Hivi mnataka mheshimiwe vipi? Mnaanza na mshahara wa juu serikalini kuliko fani yeyote ile. Mnapoanza tu mnapewa stahili ya kupewa nyumba. Tatizo mnajilinganisha na taasisi ambazo zinaendeshwa tofauti. Mbona huko majuu haukuti madaktari wakigoma kwa sababu wacheza mpira wanalipwa mishahara ya ajabu? Kama inakusumbua basi heri acha kazi ya udaktari ujiunge nao kama walivyofanya wenzako walioingia kwenye siasa ili nao wavute vijisenti.

Hicho cha kibarua na serikali na za huko Marekani hayanihusu. Mada hii inazungumzia madaktari wa Muhimbili na by extension wa serikalini na sio wa Aga Khan au wale walio kwenye NGO za Ukimwi!

Amandla.....

Nasemaje,wewe huna mamlaka ya kuhukumu nani ameelimika na nani hajaelimika.Kama unadhani umeelimika kwa hizi pumba zako unazozimwaga humu,sahau,kwavile binafsi nakuona kilaza tu unayelazimisha hoja na ukiona unabanwa unakimbilia vifilosofi vyako ukidhani vitawatisha watu.
Huyo binadamu tu anaharibika,sembuse kazi za mikono yake?Hizo zinazoharibika vipi hazitumiki tena baada ya kuharibika?Na zenyewe zinahifadhiwa vipi kama hatuna uwezo na mazingira ya kuzihifadhi?
Nyie ndiyo vizee vinafanya kazi serikalini,tangia enzi za sera za Ujamaa wa Nyerere,hamna mapya,mmebaki kukaa ofisini tu,kufanya urasimu na kukwamisha vijana wenye mawazo mapya na mipango ya maendeleo.

Mfano wako wa miaka mingi darasani na kukimbia mita nyingi ni irrelevant,kwani ugumu wa medical school siyo tu kukaa darasani miaka mingi na ndiyo maana nikasema huwezi kuelewa nitakachoongea kwasababu huijui shuruba yake.Nimesema mshahara walau uanzie M3.Haina maana kuwa medicine ndiyo iwe the most paid profession.Lakini hata ingekuwa,sioni tatizo vilevile.Lengo ni kufanya wayamudu maisha na waache kuhangaikahaingaika kwenye vijizahanati na kupokea virushwa,kusudi huu muda wautumie vizuri kwa ajili ya wagonjwa wao serikalini.Halafu unafananisha wacheza mpira na madaktari,wanaofanya kazi serikalini?dah kweli kazi hipo!Na wapi niliposema nimesoma udaktari miaka 13,kama siyo wewe kuanza kunipakazia?Issue ya Marekani umeianza wewe na umeiandika kana kwamba kwenda huko ni kama kwenda peponi hivi,yaani mpaka uwe na kibali cha Mungu!

Mkuu again huna mamlaka ya kuniamulia nifanye kazi gani.Ni practice medicine or niache,nipractice bongo or kiwanja,this is none of your business.Wewe tetea hoja zako tu na niko hapa kuongea ninaloliamini ni la kweli na kamwe sitachoka kukujibu.
 
Wapi nimebisha kuwa mimi ni kilaza? Wewe ndiye unayetaka kututisha kwa sababu ulisoma miaka 13 kozi ya miaka 5! Nilikwambia pengine uliwasoma hao mafilosofa lakini haukupata kitu. Mimi hapa nimewataja waheshimiwa wachache ambao hao mnaowadharau kwa kuwaita mangwini wanawasoma na wala sikuzumzia filofi zao wala kusema kuwa nimewasoma. Mamlaka ya kusema kuwa wewe umesoma lakini haujaelimika ninayo kutokana na uanachama wangu wa hii Forum. Nisichoweza ni kulazimisha wengine wakubaliane nao. Kazi hiyo unaifanya wewe kwa namna unavyojibu hoja.

Huyo binadamu tu anaharibika,sembuse kazi za mikono yake?Hizo zinazoharibika vipi hazitumiki tena baada ya kuharibika?Na zenyewe zinahifadhiwa vipi kama hatuna uwezo na mazingira ya kuzihifadhi?

Kwa sababu ni kawaida chombo kuharibika basi tupeleke CT Scan Sumbawanga, Tabora au Kigoma ambako mazingira ni magumu? Kwa mtaji huu basi bora ulienda kupasua vyura maana ngwini ingekushinda.

Nyie ndiyo vizee vinafanya kazi serikalini,tangia enzi za sera za Ujamaa wa Nyerere,hamna mapya,mmebaki kukaa ofisini tu,kufanya urasimu na kukwamisha vijana wenye mawazo mapya na mipango ya maendeleo.

Naaaam, kweli mimi ni kizee. Lakini kama mawazo yenyewe ya maendeleo ni ya kila mmoja wenu avute milioni tatu kila mwezi na kupeleka CT Scan kila mkoa bila kutuambia nchi yetu itamudu vipi, basi hayastahili kupewa nafasi maana mtatupeleka kubaya kuliko tulipo sasa.

Mfano wako wa miaka mingi darasani na kukimbia mita nyingi ni irrelevant,kwani ugumu wa medical school siyo tu kukaa darasani miaka mingi na ndiyo maana nikasema huwezi kuelewa nitakachoongea kwasababu huijui shuruba yake.Nimesema mshahara walau uanzie M3.Haina maana kuwa medicine ndiyo iwe the most paid profession.Lakini hata ingekuwa,sioni tatizo vilevile.Lengo ni kufanya wayamudu maisha na waache kuhangaikahaingaika kwenye vijizahanati na kupokea virushwa,kusudi huu muda wautumie vizuri kwa ajili ya wagonjwa wao serikalini.Halafu unafananisha wacheza mpira na madaktari,wanaofanya kazi serikalini?dah kweli kazi hipo!Na wapi niliposema nimesoma udaktari miaka 13,kama siyo wewe kuanza kunipakazia?Issue ya Marekani umeianza wewe na umeiandika kana kwamba kwenda huko ni kama kwenda peponi hivi,yaani mpaka uwe na kibali cha Mungu!

Mimi ndio maana nakwambia ngqwini usingeiweza maana huwezi kutetea hoja. Utasemaje argument yangu ni irrelevant bila kutuonyesha wapi imepungukiwa? Hapa hauongei na mimi peke yangu, ainisha tu hizo shurubu unazotuambia ziko katika masomo yenu na bila shaka kuna wasomi wenzako watakaokuelewe. Ni utetezi wa kiabunuwasi kusema kuwa siwezi kukwambia kwa sababu hautaelewa! Sahihisho kidogo kutoka kwa kilaza," hauwezi ukasema the most paid profession. Ulichotakiwa kusema ni "the most HIGHLY paid profession". Lakini wote tunateleza, hata wasomi kama nyie. Sasa kama si lazima nyie muwe the most highly paid profession, ni nani ambae mnadhani angestahili kulipwa kuliko nyie? Madereva wa mabasi kwa sababu wanabeba roho za watu sitini kila wakikaa nyuma ya usukani? Au wa treni? Au wa ndege? Nani, maana mangwini hamtaki wawapite kimshahara. Kutokana na argument yako basi hata hao wakina vijisenti wasingeangaikia vi 10% kama wangelipwa vizuri? Unaamini kweli kinachowafanya madaktari, majaji, mawakili, wahandisi kuendekeza rushwa ni ugumu wa maisha?

Mfano wa watu kusoma miaka 13 umeutoa wewe. Kama hukusoma wewe basi bila shaka ni mtu unaemfahamu ndiyo maana unatetea aendekeze rushwa kulipia miaka aliyokuwa akikamatwa na maprofesa wanoko.

Nyie ndio mnaodai kuwa kuna nchi ambako taaluma yenu inaheshimiwa. Mimi nikawaambia basi kama ni hivyo basi nendeni huko ambako majani ni kijani zaidi. Botswana na Marekani ni mifano tu. Kama huko unaona hakufai basi wewe chagua tu nchi ambayo itakupa heshima unayostahili, mshahara wa nguvu, CT Scan hadi chooni, hospitalizenye robots kila mahali n.k ili roho yako isuuzike. Kwetu hapakufai. Watakuja kukufunga bure tu kwa kuchukua rushwa kumbe mwenzao unaganga njaa.

Mkuu again huna mamlaka ya kuniamulia nifanye kazi gani.Ni practice medicine or niache,nipractice bongo or kiwanja,this is none of your business.Wewe tetea hoja zako tu na niko hapa kuongea ninaloliamini ni la kweli na kamwe sitachoka kukujibu.

Kweli sina mamlaka ya kukuchagulia wapi pa kufanya kazi. Lakini sitakuacha uje hapa kushabikia uovu wa wenzako ( bila shaka na wewe unahusika) ati kwa sababu mnapunjwa mshahara.

Sijakukataza kunijibu. Ubavu huo sina. Tofauti na wewe, sina kawaida ya ku-suffer fools gladly. Nina limit ya kuvumilia upuuzi. Ukiona kimya basi ujue kiwango hicho kimefika. Don't insult our intelligence kwa kutuletea vi-half baked theories vyenu.

Amandla.......
 
Back
Top Bottom