Unatangaza unauza,ukipigiwa simu na mnunuzi unaanza longolongo

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,837
8,221
Jamani mimi nimekereka kupita kiasi yaani nataka hadi kutapika kwa kukereka huko,siku hizi kuna tabia imezuka watu wanatangaza katika magazeti,mitandao kuwa wanauza vitu kwa mfano simu,kamera ,software n.k na wanaweka namba zao za simu,cha ajabu ukimpigia mtakubaliana kuwa atakuuzia ,sasa ukimwambia tuonane mi nina fungu hapo ndipo longolongo linaanza ,utasikia oh niko mbali tuonane kesho muda fulani ,ukifika huo muda utaona huyo mtu hatokei ukipiga simu utasikia ah nilisahahu kesho basi nitakupigia hapo ndio sahau,na ukimkumbusha utasikia ah,ile kitu kuna ndugu yangu kaimaindi au blahblah kibao.
Sasa ninachojiulize kama huuzi unatangazia nini?na kama basi umeshauza hicho kitu au umefikiria mengine uungwana unatakiwa umwambia huyo mtu kuwa kile kitu siuzi tena au nimempa ndugu yangu,kuliko kusumbuana ati ,mtu unaacha shughuli zako ,unapoteza airtime kwa mambo ambayo unakuwa kama usanii vile,ah nasikia kichefuchefu kweli kwa hiyo tabia
 
Pole mkuu! UNaonaje ukimmwaga hadharani huyo mjingamjinga ili tumkome!?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom